mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Kiuhalisia Chama cha Mapinduzi (CCM) kilishakufa au ndio kinakaribia kukata roho. Kilichopo sasa hivi ni chama kingine kabisa japo wengi wa wanachama na mashabiki wa ccm hawajang'amua hilo.
Kwanza ni jina. Katika zungukazunguka ya Polepole huwa anatambulisha chama chake kama CCM Mpya. Hiki ni chama tofauti.
Pili mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais wa nchi ameteua wasaidizi wengi nje ya chama cha mapinduzi. Mawaziri wengi amewatoa nje ya chama. Wengine hawakuwa na chama. Walichukua kadi za CCM baada ya kuteuliwa. Kwa maneno wengi wa wasaidizi wa Magufuli hawana historia ya kukipigania chama cha mapinduzi. Hawakutoka jasho kwa ajili ya ccm. Wengine walikuwa wapinzani na wakosoaji wakubwa wa ccm.
Asilimia kubwa ya wanaccm waliopambana siku nyingi ndani ya chama wako benji.
Tunaona sasa wapinzani wakubwa wa ccm wakilamba vyeo vikubwa bila kukitokea chama jasho.
Kwa siku za usoni inaonekana mwenyekiti wa ccm amekuwa anavutiwa zaidi na wapinzani kuliko wanaccm wenzake.
Tumesikia taarifa ya Meya wa Ubungo ndugu Jacob akishuhudia jinsi mwenyekiti wa ccm anavyowatamani viongozi machachari wa upinzani mpaka kufikia kuwapigia baadhi simu na kuwaambia anawahitaji kwa gharama yoyote.
Wapinzani wengi wamejiunga ccm kwa muda mfupi na kulamba vyeo. Kina Shonza na Mwampamba wamewakuta wengi huko ccm lakini wao wameula fasta. Wengine kama kina Kitila na Anna Mghwira wao waliula kabla hata ya kujiunga na Ccm. Wengine wakiosmbiwa wanahitajika kwa udi na uvumba na kuitika fasta ni kina Kafulila na Katambi. Hawa watapangiwa kazi muda si mrefu.
Kwa hiyo kimsingi Magufuli ameikacha ccm na kuunda ccm yake. Polepole anaiita ccm mpya.
Swali la kujiuliza ni, je mkakati huu wa Magufuli wa kukikacha chama kilichimpa madaraka aliyonayo na kujiundia chama kingine kinyemela ambacho watendaji wake wengi hawana mizizi ndani ya ccm na wala sio wafia chama ukianzia na Polepole mwenyewe utafanikiwa in the long term?
Na je, ccm itaendelea kuwa moja kama mkskati wa kuua upinzani
Utafanikiwa hasa ukizingatia wakongwe na wafiwa chama hawafurahishwi najinsi wageni wansvyopewa nafasi kubwa kubwa huku wao wakiachwa?
Kwa maana kwamba kinachowaunganisha ccm ukiacha maslahi binafsi ni kule kuwa na upinzani imara. Ina maana kitisho cha kunyanganywa tonge na upinzsni kikitoweka ni wazi wataanza kupingana wao kwa wao . Je hili halitaleta mpasuko mkubwa na ccm kugawanyika kati ya CCM na CCM Mpya? Hii ccm mpya isiyokuwa na miziziitsweza kusimama mbele ya CCM?