Je, mnajua CCM ilishakufa? Kilichopo ni chama tofauti kabisa, Fuatana nami

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Kiuhalisia Chama cha Mapinduzi (CCM) kilishakufa au ndio kinakaribia kukata roho. Kilichopo sasa hivi ni chama kingine kabisa japo wengi wa wanachama na mashabiki wa ccm hawajang'amua hilo.

Kwanza ni jina. Katika zungukazunguka ya Polepole huwa anatambulisha chama chake kama CCM Mpya. Hiki ni chama tofauti.

Pili mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais wa nchi ameteua wasaidizi wengi nje ya chama cha mapinduzi. Mawaziri wengi amewatoa nje ya chama. Wengine hawakuwa na chama. Walichukua kadi za CCM baada ya kuteuliwa. Kwa maneno wengi wa wasaidizi wa Magufuli hawana historia ya kukipigania chama cha mapinduzi. Hawakutoka jasho kwa ajili ya ccm. Wengine walikuwa wapinzani na wakosoaji wakubwa wa ccm.

Asilimia kubwa ya wanaccm waliopambana siku nyingi ndani ya chama wako benji.

Tunaona sasa wapinzani wakubwa wa ccm wakilamba vyeo vikubwa bila kukitokea chama jasho.

Kwa siku za usoni inaonekana mwenyekiti wa ccm amekuwa anavutiwa zaidi na wapinzani kuliko wanaccm wenzake.

Tumesikia taarifa ya Meya wa Ubungo ndugu Jacob akishuhudia jinsi mwenyekiti wa ccm anavyowatamani viongozi machachari wa upinzani mpaka kufikia kuwapigia baadhi simu na kuwaambia anawahitaji kwa gharama yoyote.

Wapinzani wengi wamejiunga ccm kwa muda mfupi na kulamba vyeo. Kina Shonza na Mwampamba wamewakuta wengi huko ccm lakini wao wameula fasta. Wengine kama kina Kitila na Anna Mghwira wao waliula kabla hata ya kujiunga na Ccm. Wengine wakiosmbiwa wanahitajika kwa udi na uvumba na kuitika fasta ni kina Kafulila na Katambi. Hawa watapangiwa kazi muda si mrefu.

Kwa hiyo kimsingi Magufuli ameikacha ccm na kuunda ccm yake. Polepole anaiita ccm mpya.

Swali la kujiuliza ni, je mkakati huu wa Magufuli wa kukikacha chama kilichimpa madaraka aliyonayo na kujiundia chama kingine kinyemela ambacho watendaji wake wengi hawana mizizi ndani ya ccm na wala sio wafia chama ukianzia na Polepole mwenyewe utafanikiwa in the long term?

Na je, ccm itaendelea kuwa moja kama mkskati wa kuua upinzani
Utafanikiwa hasa ukizingatia wakongwe na wafiwa chama hawafurahishwi najinsi wageni wansvyopewa nafasi kubwa kubwa huku wao wakiachwa?
Kwa maana kwamba kinachowaunganisha ccm ukiacha maslahi binafsi ni kule kuwa na upinzani imara. Ina maana kitisho cha kunyanganywa tonge na upinzsni kikitoweka ni wazi wataanza kupingana wao kwa wao . Je hili halitaleta mpasuko mkubwa na ccm kugawanyika kati ya CCM na CCM Mpya? Hii ccm mpya isiyokuwa na miziziitsweza kusimama mbele ya CCM?
 
148af373518e16e3c17f58f97df16b8d.jpg
 
Nina mtazamo tofauti kidogo ndugu MCFM40.

Kwa ufupi sana Mh Magufuli hawezi kuiua CCM (iwe kwa bahati mbaya au makusudi), ukweli ni kuwa CCM itaendelea kuwa hai maana kwa uwezo (akili na madaraka) na staili ya Magufuli ni sawa sawa na mimba iliyotungwa nje ya kizazi tu.

Atapita, anachoweza kuwaachia labda ni matatizo/misukosuko lakini sio kukiua. CCM inaweza kufa (hata mimi ningependa itokee kwa faida ya nchi na vizazi vijayvo) lakini si akili za Mh Magufuli. Kitu kingine CCM ni chama ambacho kimejengwa katika misingi ya unafiki na kimezoea fitna.

Lakini Mh Magufuli anaweza kuua uchumi, anaweza kuua elimu, anaweza kuua upendo na umoja wa Taifa na wananchi wake. Hapo ndipo tunapopaswa kupaangalia kwa umakini na kuchukua hatua.
 
Kwa hiyo kimsingi Magufuli ameikacha ccm na kuunda ccm yake. Polepole anaiita ccm mpya.

Hata katika kampeni zake, kilichomfanya akashinda ni ccm mpya. Si unakumbuka kuna kipindi ulikuwa huwezi vaa kijani ukavuka barabara?? Ile ccm ilikufa. Aliyoingia nayo Faru ni tofauti kabisa na hiyo. Ndo maana hakuna popote aliposema chagua ccm bali chagua Magu
 
Kinachoonekana ni mkakati wa
Nina mtazamo tofauti kidogo ndugu MCFM40.

Kwa ufupi sana Mh Magufuli hawezi kuiua CCM (iwe kwa bahati mbaya au makusudi), ukweli ni kuwa CCM itaendelea kuwa hai maana kwa uwezo (akili na madaraka) na staili ya Magufuli ni sawa sawa na mimba iliyotungwa nje ya kizazi tu.

Atapita, anachoweza kuwaachia labda ni matatizo/misukosuko lakini sio kukiua. CCM inaweza kufa (hata mimi ningependa itokee kwa faida ya nchi na vizazi vijayvo) lakini si akili za Mh Magufuli. Kitu kingine CCM ni chama ambacho kimejengwa katika misingi ya unafiki na kimezoea fitna.

Lakini Mh Magufuli anaweza kuua uchumi, anaweza kuua elimu, anaweza kuua upendo na umoja wa Taifa na wananchi wake. Hapo ndipo tunapopaswa kupaangalia kwa umakini na kuchukua hatua.
Kinachoonekana sasa kuna mkakati wa siri kati ya Magu na watu wake wa karibu kuivunja ccm!
 
Kwa taarifa yako mleta uzi ccm asilia na ccm academia (mpya) zote zinategemea jeshi kuendelea kuwa hai. Na mwenye nguvu kati ya hizo ccm zote mbili ni yule anayeweza kuliagiza jeshi kufanya lolote ili ishinde. Hivyo kwa sasa ccm yenye nguvu ni hiyo mpya. Hiyo ccm asilia haina la kufanya zaidi ya kuigiza na kuleta majungu chinichini maana wanajua hata wakimeguka bado watajikuta hawawezi kufanya lolote maana jeshi halitokuwa upande wao.
 
Asiliamini Jeshi sana. Wakimchoka na wakiona nchi inakwenda ndipo sipo wanaweza wakafanya ya Zumbabwe pia!
 
Kiuhalisia Chama cha Mapinduzi (CCM) kilishakufa au ndio kinakaribia kukata roho. Kilichopo sasa hivi ni chama kingine kabisa japo wengi wa wanachama na mashabiki wa ccm hawajang'amua hilo.

Kwanza ni jina. Katika zungukazunguka ya Polepole huwa anatambulisha chama chake kama CCM Mpya. Hiki ni chama tofauti.

Pili mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais wa nchi ameteua wasaidizi wengi nje ya chama cha mapinduzi. Mawaziri wengi amewatoa nje ya chama. Wengine hawakuwa na chama. Walichukua kadi za CCM baada ya kuteuliwa. Kwa maneno wengi wa wasaidizi wa Magufuli hawana historia ya kukipigania chama cha mapinduzi. Hawakutoka jasho kwa ajili ya ccm. Wengine walikuwa wapinzani na wakosoaji wakubwa wa ccm.

Asilimia kubwa ya wanaccm waliopambana siku nyingi ndani ya chama wako benji.

Tunaona sasa wapinzani wakubwa wa ccm wakilamba vyeo vikubwa bila kukitokea chama jasho.

Kwa siku za usoni inaonekana mwenyekiti wa ccm amekuwa anavutiwa zaidi na wapinzani kuliko wanaccm wenzake.

Tumesikia taarifa ya Meya wa Ubungo ndugu Jacob akishuhudia jinsi mwenyekiti wa ccm anavyowatamani viongozi machachari wa upinzani mpaka kufikia kuwapigia baadhi simu na kuwaambia anawahitaji kwa gharama yoyote.

Wapinzani wengi wamejiunga ccm kwa muda mfupi na kulamba vyeo. Kina Shonza na Mwampamba wamewakuta wengi huko ccm lakini wao wameula fasta. Wengine kama kina Kitila na Anna Mghwira wao waliula kabla hata ya kujiunga na Ccm. Wengine wakiosmbiwa wanahitajika kwa udi na uvumba na kuitika fasta ni kina Kafulila na Katambi. Hawa watapangiwa kazi muda si mrefu.

Kwa hiyo kimsingi Magufuli ameikacha ccm na kuunda ccm yake. Polepole anaiita ccm mpya.

Swali la kujiuliza ni, je mkakati huu wa Magufuli wa kukikacha chama kilichimpa madaraka aliyonayo na kujiundia chama kingine kinyemela ambacho watendaji wake wengi hawana mizizi ndani ya ccm na wala sio wafia chama ukianzia na Polepole mwenyewe utafanikiwa in the long term?

Na je, ccm itaendelea kuwa moja kama mkskati wa kuua upinzani
Utafanikiwa hasa ukizingatia wakongwe na wafiwa chama hawafurahishwi najinsi wageni wansvyopewa nafasi kubwa kubwa huku wao wakiachwa?
Kwa maana kwamba kinachowaunganisha ccm ukiacha maslahi binafsi ni kule kuwa na upinzani imara. Ina maana kitisho cha kunyanganywa tonge na upinzsni kikitoweka ni wazi wataanza kupingana wao kwa wao . Je hili halitaleta mpasuko mkubwa na ccm kugawanyika kati ya CCM na CCM Mpya? Hii ccm mpya isiyokuwa na miziziitsweza kusimama mbele ya CCM?

mkuu ni kawaida sana sana sana sana, kila rais kuwa na timu yake, watu wake...

mabadiliko ya ccm ndio yanayokifanya kuwa na nguvu

mpasuko ccm pia ni wa kawaida sana, ADUI NA MPINZANI MKUBWA wa ccm ni ccm makundi makundi

lowasa na mbowe wasingekuwa na upinzani wa nguvu, lowassa angepita kirahisi; katokea JPM pale ambapo watu walikwa wanavaana

mabadiliko ya ccm ndio uhai wake...... na vyama vingine viige; ulitaka mkapa mpaka leo awe mwenyekiti wa ccm?
 
Kwani mkapa kuwa mwenyekii wa ccm leo kungekuwa na ubaya gani? Si ndio ingekuwa vizuri kwa ajili ya checks and balances? Angalia jamaa anavyokurupuka kwenye baadhi ya mambo wala hakuna mtu huko ccm wa kumwambia kitu. Aha kwamba ni kawaida kwa rais kuacha wanachama wake waliompigania na kuamua kuchukua wapinzani na kuwapa nafasi kubwa kubwa?

Back
Top Bottom