Dseni
Member
- Aug 13, 2012
- 40
- 51
Je Makonda anajua uonevu huu katika mkoa wake?
Tarehe 29/12/2018 niliondoka na gari la kanisa letu asubuhi nyumbani kwangu Madale kuelekea Mbweni kwa ajili ya kuchukua “lose report” kwa sababu nilipotelewa na simu yangu. Nilipofika Contena nikakumbuka kwamba nahitaji kuchukua barua kutoka serikali za mitaa, hivyo basi nikaamua kupaki gari kwenye duka moja kisha nikaenda serikali za mitaa. Nilifanikiwa kupata barua ya utambulisho; lakini nilipofika kwenye gari nilikuta watu wanne ambao walijitambulisha kwamba wao ni watu wa jiji ambao wanatembea mtaani kukagua magari ambayo yanapaki vibaya. Wakasema kwamba nimepaki gari sehemu ambayo siyo ya kupaki magari. Nikawauliza kwamba, je hapa Kontena (kijijini kabisa) kuna sehemu maalum ya kupaki magari? Gari langu halipo barabarani, liko kando ya duka la kuuza vifaa vya ujenzi. Nikazidi kuwauliza maswali; lakini majibu yao ni kwamba gari haijapakiwa kwenye sehemu sahihi. Kwa madai yao, hata maeneo ya vijijini magari yanapaswa yapakiwe sehemu maalumu. Kwa hiyo ninatakiwa kulipa faini ya shilingi 300,000. Nikakataa kabisa. Baada ya kuona nimekataa, mmoja wa maafsa ambaye sikumbuki jina lake lakini ana namba za simu 0657913006 alimwamuru mmoja wa vijana aliokuwa nao kuingia kwenye gari na hivyo linapaswa lipelekwe yard ya Mwananyamala. Lakini kuna neno alilisema kwamba “naomba umsikilize mchungaji na muelewane vizuri tu.”
Kwa kuwa walikomaa kwamba nina makosa, nikaona isiwe tabu, wacha nitii sheria; lakini niliamini kwamba sikufanya kosa lolote kwa sababu 1) hiyo sehemu haikuwa wrong parking kama walivyodai maana hakuna sehemu maalum ya kupaki magari eneo hilo 2) gari ilikuwa nje kabisa ya barabara na ilikuwa dukani kwa mtu.
Safari ilianza ya kuelekea Mwananyamala mwendo wa kilometer 18 hivi. Yule kijana (afsa) aliyekuwa ameambiwa anipeleke yard akakaa pale mbele. Nikamwambia afunge mkanda wa abiria akakataa kwa madai kwamba yeye hawezi kufunga mkanda kwa sababu ni afsa ambaye amenikamata mimi. Tulihitilafiana hapo kwa sababu ni wajibu wangu kuhakikisha abiria wangu anakuwa salama; ingawa alinikamata lakini alitakiwa atii sheria pia. Hata hivyo hakutii kabisa. Nikakubali tu kuendesha gari na kwenda.
Tukiwa njiani tuliongea na afsa mmoja ambaye alisema yuko ofisini Mwananyamala, akasema kwamba gari langu tayari picha imeshapigwa na iko wilayani, hivyo lazima gari iende yard na nikifika wataniandika warning kwa gharama ya shilingi 20,000. Nilijaribu sana kumwambia kwamba mimi ni mchungaji ambaye kesho nahitaji kuhubiri kanisani kwangu na kuna watu wengi wanahitaji huduma yangu, kitendo cha kunileta Mwananyamala kana kwamba nimefanya kosa la jinai nadhani siyo sawa! Yule kijana akakata simu.
Tulipofika Mwananyamala Yard, tukapaki gari kwa ndani, na nikamuuliza huyu kijana (afsa) anioneshe ofisi nizungumze na bosi wake. Jambo la ajabu lililonishangaza ni kwamba GARI HAIKUANDIKISHWA WAKATI NAINGIA MLE NDANI. Nikapelekwa kwenye kibanda cha getini ambayo ndiyo ofisi yao. Nikauliza warning form iko wapi niandikiwe haraka ili niondoke. Mmoja wa maafsa akasema zimeisha! Yule kijana niliyekuwa naye garini (afsa) akapotea kama dakika 10 hivi, aliporudi alikuwa na form ya faini ambayo tayari imeshajazwa ninapaswa kulipa 300,000 kwa sababu ya wrong parking katika eneo la Madale. Nikamwangalia yule kijana kwa makini sana (jina lake ni John)! Nikamuuliza kwamba “unadhani unaongea na mpumbavu asiyejua kitu? Je unadhani naweza kuonewa mchana kweupe? Je hukuweza hata kufikiri barabarani kwamba mimi ni mtumishi wa Mungu unanifishaje mpaka hapa kwa kosa hili? Je ni kweli unadhani nilipaki sehemu isiyo sahihi? Je unaweza kunionesha eneo la Madale/Contena sehemu ya kupaki magari? Je Madale imekuwa ni kama Posta Mpya au Kariakoo? Je Madale imekuwa kama Tegeta Center? Huyu kijana alishindwa kujibu maswali yangu, na badala yake akaondoka.
Nikaanza kuongea kwa sauti kubwa, maana niligundua kwamba hapa ninataka kuonewa kabisa na lazima nipaze sauti! Baadhi ya watu waliokuwepo hapo walionesha kukerwa na kitendo cha maafsa hao kushindwa kuheshimu maelezo yangu na kuamua kunipeleka Mpaka Mwananyamala! Baadaye kijana huyu (John); ambaye nilitoka naye Madale/ Contena akaja na kunieleza kwamba ataniitia mtu mwingine wa kunisadia.
Ni kweli alikuja afsa mwingine ambaye nilimweleza kwa kina jinsi ilivyokuwa! Akaenda kwenye gari akasoma ni gari la kanisa! Mara akaniambia kwamba subiri kidogo! Baadaye kidogo akaja na kusema kwamba nilipe nusu ya faini. Nilikataa kulipa hata nusu ya faini hiyo! Baadaye alipiga simu kwa muda kama wa dakika 3 hivi, na alipokata simu aliniambia hivi “MCHUNGAJI, NAOMBA UTOE GARI LAKO HAPA UENDELEE NA SHUGHULI ZAKO, POLE SANA KWA USUMBUFU ULIOPATA.” Nikamuuliza swali, iko wapi warning form? Akasema “NAOMBA MCHUNGAJI UTOE GARI LAKO BURE, USILIPE HATA SHILINGI MOJA.” Kwa kuwa nilikuwa nimekaa pale kama saa 2 hivi, sikuamini maneno yake; nikamwambia, ngoja nilete gari langu getini hapa ndipo niamini kama maneno yako ni kweli. Hakika, nikasogeza gari langu getini, na mlinzi alinifungulia nami nikaondoka.
Lakini mpaka hapo nilikuwa nimeshavurugiwa ratiba zangu zote, na pia nilitumia mafuta ya gari vibaya! Ninamshukuru aliyeamuru nitolewe bure, lakini naomba hawa vijana wa jiji wachunguzeni vizuri!
Mwisho wa maelezo yangu
Kwa uelewa wangu binafsi niligundua kuna rushwa kali sana eneo la Kinondoni na hawa watu wanaojifanya watu wa jiji wanaonea sana watu. Sikutaka kabisa kutoa kitu chochote kwa hawa maafsa, nilitaka nione namna watu wanavyoonewa.
Je kama mimi mchungaji wamenifanyia hivyo; hawa watu wa jiji watafanyaje kwa mtu wa kawaida ambaye anatafuta pesa kwa kutumia gari lake?
“Je Makonda anajua uonevu huu? Je anawatuma kukusanya kodi kwa kuwaonea watu vijijini? Nataka nimwambie Mkuu wa Mkoa (Makonda) kwamba kuna watu wachache ndani ya mkoa wake wanaoharibu, mpaka watu wanaichukia serikali. Hivi majuzi nilikamatwa tena na hawa watu wa jiji eti nimeenda mjini na gari tani 2 bila kibali. Nikawaambia hili siyo gari la biashara, ni gari la kanisa, na tumekuja kwa shughuli za kikanisa, walikataa kabisa mpaka tukalipa faini ya shilingi 50,000. Je haya mambo nani ayakemee? Yaani hawa watu wa jiji ni kero juu ya kero!
Mkuu wa Mkoa anza na huyu afsa mwenye namba ya simu 0657913006 Imesajiliwa kwa jina la MAULID BAKARI
Mimi
Mchungaji Daniel John Seni
Presbyterian Church in Tanzania
senishekinah@gmail.com
SAMBAZA UJUMBE HUU MPAKA UFIKE KWA MAKONDA MWENYEWE
Sent using Jamii Forums mobile app