Je, Manabiii wa uongo ni mradi wa Watawala?

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,250
Reaction score
26,639
Ukimya wao kwa maovu ni ushahidi wa kushiriki mpango mchafu

Katika historia ya dini, manabii wa kweli waliitwa kuwa sauti ya Mungu mbele ya mataifa. Walikemea dhambi, walipinga dhuluma, na mara nyingi waliteswa kwa ajili ya kusema ukweli. Lakini kizazi cha sasa kimejaa “manabii” ambao kazi yao kubwa si kuwakilisha Mungu, bali kutumikia ajenda za kisiasa. Wanavaa mavazi ya utakatifu lakini ndani yao wamejaa ujanja, tamaa na hila. Wamegeuzwa kuwa kisingizio cha kuhalalisha uovu kwa jina la imani.

Tofauti na Nabii Nathan aliyemkemea Daudi au Elia aliyekemea Ahabu, manabii wa leo wanafunga midomo kwa makusudi, si kwa sababu Mungu haneni, bali kwa sababu wamekubali kuuzwa. Wamejifunga kwa mikataba ya kimyakimya na watawala. Wanapewa magari ya kifahari, vibali vya bure, ulinzi wa polisi kwenye mikutano, hata misaada ya kifedha ili “wasilete maneno ya kuharibu amani.” Kwa lugha rahisi, wameuzwa na mfumo.

Serikali nyingi hutumia dini kama kifuniko cha dhuluma zao. Badala ya kuwa walinzi wa ukweli, manabii hawa hugeuzwa kuwa walinzi wa hadhi ya watawala. Wanapokandamizwa wakulima, wauguzi, wanafunzi au wafanyabiashara wadogo manabii husema, “Subira, ni mpango wa Mungu.” Lakini huwezi kuitisha subira pasipo haki. Afrika, makanisa na huduma nyingi zinalishwa kimyakimya kwa ardhi, pesa, mikopo au fursa za kibiashara kwa masharti ya kutokemea serikali. Hii si injili ni uoga uliovaa joho la kiroho.

Katika baadhi ya nchi, idara za usalama hushirikiana moja kwa moja na baadhi ya viongozi wa dini. Wengine huwekwa kwenye payroll (mishahara isiyo rasmi), huku wengine wakipewa nyadhifa za heshima kama wajumbe wa tume, mabalozi wa amani, au washauri wa taifa. Lengo ni moja: wasivuruge “status quo.” Na kwa hilo, hawaguswi na mamlaka, wala hawawekwi kwenye orodha za uchunguzi. Huduma zao hulindwa, miradi yao hupitishwa, na jina lao hubebwa na vyombo vya habari kama “watumishi wa kiroho wenye maono.”

Kwa sasa, Tanzania ina zaidi ya watu milioni moja wanaojiita manabii au mitume, lakini ni wachache sana wanaosimama kwa haki au kusema ukweli kwa ujasiri. Wengi ni project za wakubwa, wamepandikizwa ili kuua njozi ya mabadiliko ya kweli. Wanatangaza "miaka ya neema na baraka", ilhali watu wanalia kwa njaa na dhuluma. Wanahubiri “kufunguliwa kwa milango ya mbinguni”, ilhali milango ya hospitali, elimu, haki na ajira imefungwa duniani.

Ni muhimu sana watu wawe makini. Usikubali kila anayesema "Bwana amesema" amesemewa kweli. Dunia ina siri nzito ambazo watu wa kawaida hawajui. Kuna mikakati ya kiintelijensia ya kutumia dini kama silaha ya udhibiti wa watu. Kuna warsha na mafunzo ya namna ya kupandikiza manabii ili kudhibiti upinzani wa kiraia. Kuna miradi ya kisiasa inayotumia miujiza na unabii kama dawa ya kusahaulisha matatizo halisi ya kijamii.

Biblia inaonya wazi juu ya hatari hiyo. Yeremia 23:16 inasema:
“Msisikilize maneno ya manabii wanaowatabiria; wanawapa matumaini ya uongo. Husema maono ya mioyo yao wenyewe, wala si kutoka kinywani mwa Bwana.”
Na Yesu akasema:
“Jihadharini na manabii wa uongo, wanaokuja kwenu wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.” (Mathayo 7:15)

Kwa hiyo, mtu wa Mungu wa kweli hatakiwi kuwa kipofu wa kiroho. Angalia si maneno tu, bali matendo. Angalia si unabii wa madhabahuni, bali msimamo kwa haki. Nabii anayenyamaza wakati taifa linafungwa, watu wanauawa, haki inauzwa si sauti ya mbinguni, bali sauti ya mfumo.

Ukweli huu ni mgumu, lakini ni lazima usemwe. Taifa likiendelea kuwa chini ya manabii wa hila, basi linapoteza nafasi ya kusikia sauti ya kweli ya Mungu. Na hapo ndipo giza linapozidi, si kwa kukosekana kwa ibada bali kwa wingi wa ibada zisizo na ukweli.
 
Muhammad ni zao la Waraq bin naufal
😂😂😂😂 Hii historia kali ndio maana huku mnachezewa sana maana hamna akili
Baada ya miaka 2000 mathayo anasaidiwa kazi na wahuni wenzie

Wakifungiwa makanisa si mnasema wana nyimwa haki ya kuabudu au?
 
Means sio wakristo tu mmebezi upande mmoja pia upande wapili wapo tena matapeli wakubwa sana
Ni manabii au?
Hakuna alie bezi upande mmoja nyimbo inachezwa kutokana na beat

Si unaona mada inazungumzia nini?
Na bahati nzuri hao manabii wamepasishwa na wakristo wenyewe
 
Na hapo ndipo giza linapozidi, si kwa kukosekana kwa ibada bali kwa wingi wa ibada zisizo na ukweli.
Ndio maana yule Shekhe akasema basi wamkate Kichwa huyo nabii wa Uongo
 
Wakifungiwa makanisa si mnasema wana nyimwa haki ya kuabudu au?
Tapeli yule na siku akizinguana na mfumo watachomfanya atakimbia Nchi asirudi tena atakimbilia Zambia huko
 
Ukimya wao kwa maovu ni ushahidi wa kushiriki mpango mchafu

Katika historia ya dini, manabii wa kweli waliitwa kuwa sauti ya Mungu mbele ya mataifa. Walikemea dhambi, walipinga dhuluma, na mara nyingi waliteswa kwa ajili ya kusema ukweli. Lakini kizazi cha sasa kimejaa “manabii” ambao kazi yao kubwa si kuwakilisha Mungu, bali kutumikia ajenda za kisiasa. Wanavaa mavazi ya utakatifu lakini ndani yao wamejaa ujanja, tamaa na hila. Wamegeuzwa kuwa kisingizio cha kuhalalisha uovu kwa jina la imani.

Tofauti na Nabii Nathan aliyemkemea Daudi au Elia aliyekemea Ahabu, manabii wa leo wanafunga midomo kwa makusudi, si kwa sababu Mungu haneni, bali kwa sababu wamekubali kuuzwa. Wamejifunga kwa mikataba ya kimyakimya na watawala. Wanapewa magari ya kifahari, vibali vya bure, ulinzi wa polisi kwenye mikutano, hata misaada ya kifedha ili “wasilete maneno ya kuharibu amani.” Kwa lugha rahisi, wameuzwa na mfumo.

Serikali nyingi hutumia dini kama kifuniko cha dhuluma zao. Badala ya kuwa walinzi wa ukweli, manabii hawa hugeuzwa kuwa walinzi wa hadhi ya watawala. Wanapokandamizwa wakulima, wauguzi, wanafunzi au wafanyabiashara wadogo manabii husema, “Subira, ni mpango wa Mungu.” Lakini huwezi kuitisha subira pasipo haki. Afrika, makanisa na huduma nyingi zinalishwa kimyakimya kwa ardhi, pesa, mikopo au fursa za kibiashara kwa masharti ya kutokemea serikali. Hii si injili ni uoga uliovaa joho la kiroho.

Katika baadhi ya nchi, idara za usalama hushirikiana moja kwa moja na baadhi ya viongozi wa dini. Wengine huwekwa kwenye payroll (mishahara isiyo rasmi), huku wengine wakipewa nyadhifa za heshima kama wajumbe wa tume, mabalozi wa amani, au washauri wa taifa. Lengo ni moja: wasivuruge “status quo.” Na kwa hilo, hawaguswi na mamlaka, wala hawawekwi kwenye orodha za uchunguzi. Huduma zao hulindwa, miradi yao hupitishwa, na jina lao hubebwa na vyombo vya habari kama “watumishi wa kiroho wenye maono.”

Kwa sasa, Tanzania ina zaidi ya watu milioni moja wanaojiita manabii au mitume, lakini ni wachache sana wanaosimama kwa haki au kusema ukweli kwa ujasiri. Wengi ni project za wakubwa, wamepandikizwa ili kuua njozi ya mabadiliko ya kweli. Wanatangaza "miaka ya neema na baraka", ilhali watu wanalia kwa njaa na dhuluma. Wanahubiri “kufunguliwa kwa milango ya mbinguni”, ilhali milango ya hospitali, elimu, haki na ajira imefungwa duniani.

Ni muhimu sana watu wawe makini. Usikubali kila anayesema "Bwana amesema" amesemewa kweli. Dunia ina siri nzito ambazo watu wa kawaida hawajui. Kuna mikakati ya kiintelijensia ya kutumia dini kama silaha ya udhibiti wa watu. Kuna warsha na mafunzo ya namna ya kupandikiza manabii ili kudhibiti upinzani wa kiraia. Kuna miradi ya kisiasa inayotumia miujiza na unabii kama dawa ya kusahaulisha matatizo halisi ya kijamii.

Biblia inaonya wazi juu ya hatari hiyo. Yeremia 23:16 inasema:
“Msisikilize maneno ya manabii wanaowatabiria; wanawapa matumaini ya uongo. Husema maono ya mioyo yao wenyewe, wala si kutoka kinywani mwa Bwana.”
Na Yesu akasema:
“Jihadharini na manabii wa uongo, wanaokuja kwenu wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali.” (Mathayo 7:15)

Kwa hiyo, mtu wa Mungu wa kweli hatakiwi kuwa kipofu wa kiroho. Angalia si maneno tu, bali matendo. Angalia si unabii wa madhabahuni, bali msimamo kwa haki. Nabii anayenyamaza wakati taifa linafungwa, watu wanauawa, haki inauzwa si sauti ya mbinguni, bali sauti ya mfumo.

Ukweli huu ni mgumu, lakini ni lazima usemwe. Taifa likiendelea kuwa chini ya manabii wa hila, basi linapoteza nafasi ya kusikia sauti ya kweli ya Mungu. Na hapo ndipo giza linapozidi, si kwa kukosekana kwa ibada bali kwa wingi wa ibada zisizo na ukweli.
Ndio
 
Waganga wapiga lamli chonganishi? Wanauza makombe na kuloga watu?
Siyo ''lamli'. Wakati mwingine uwezo wa mtu wa kuandika maneno rahisi kabisa unaweza kukufanya ujue uwezo wake wa kiakili. Unakaa darasani miaka zaidi ya saba kujifunza kuandika na ukimaliza unakuwa huwezi kuandika maneno rahisi kabisa?
 
Back
Top Bottom