Je, Makamu wa Rais wa Venezuela ndiye mtu wa ndani mshirika wa CIA aliyeisaidia Marekani kumkamata Maduro?

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
5,705
Reaction score
7,214
Kufuatia Operesheni ya kumkamata Rais Maduro, Serikali ya Marekni ilitoa taarifa kuwa mtu wa ndani ya Serikali ya Venezuela na mshirika wa CIA alisaidia kuwezesha kujua mienendo ya Rais Maduro na kufanikisha kukamatwa kwake.

Ikumbukwe Rais Trump, alitamka kuwa Makamu wa Rais wa Venezuelea Delcy Rodriguez ameongea na Serikali ya Marekani na kuahidi mazungumzo na kutoa ushirikiano kwa kuwa hana namna na anataraji kuapishwa kuwa Rais.

Rais Mteule Delcy Rodriguez ni nani
Mbali ya kuwa Makamu wa Rais lakini pia Idara ya Usalama wa ndani ya Venezuela ( SEBIN) iko chini yake ina inaripoti kwake.

Delcy ni Mtoto wa Jorge Antonio Rodriguez, mwanasiasa wa zamani wa mlengo wa kijamaa aliuawa mwaka 1975 kufuatia kukamatwa na kupitia mateso makali na Idara Usalama wa Taifa wa Venezuelea kipindi hiko (DISIP) kabla haijuvunjwa na kuundwa upya kama SEBIN baada ya kutuhumiwa kumteka mfanyabiashara wa kimarekani William Frank Niehus kuanzia 1976 mpaka 1979.

Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia serikali ya Hugo Chavez ambaye inaripitiwa waliwahi kugombana mara mbili katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kaka yake Delcy, Jorge Rodriguez ambaye Rais wa Bunge la Venezuela, iliripitiwa na gazeti maarufu nchini Marekani Financial Times kuwa alikuwa akifanya mazungumzo na Serikali ya Marekani ili kuruhusu dada yake ambaye ni Makamu wa Rais aruhusiwe kuongoza serikali ya mpito ya Venezuelea ikiwa Maduro atakamatwa.

Zipo taarifa kuwa kulikuwa na amri kwa vyombo vya ulinzi kutoshambulia helikopta na ndege vamizi , licha ya kuwa na mifumo ya Ulinzi iliyowekwa kwa masaa wa Urusi , China na Iran.

Je mtu anayetajwa kuwa mshirika wa CIA ndani ya Serijali ya Venezuela aliyefanikisha kukamatwa Maduro ni Makamu wake wa Rais?
Kutokana na nafasi yake, ukaribu wake na Rais, Utayari wa ushirikiano wake na Marekani, ukaribu na Idara ya Usalama wa Taifa inayoripoti kwake?

Je ni Kaka yake? ni kisasi kwa Venezuela kwa kuuliwa kwa Baba yao na Idara ya Usalama wa nchi yao? Mazungumzo yake na Serikali ya Marekani kuhusu mustakabali wa Venezuela yalileta ushawishi?

Nani alitoa stand down order kwa vyombo vya Ulinzi?
 
Stor za jaba mnaziweza sana
 
Huyo ni kama samuya sulubu na jiwe
 
Naona mnataka kumsema nchimbi wa watu au kwa sababu yeye mkatoliki
 
marekani wamejipatia credit kwamba zana zao imara na mbinu zao imara sasa wajichanganye kwa Putin kule Ukraine watapukutika kama majani makavu
 
marekani wamejipatia credit kwamba zana zao imara na mbinu zao imara sasa wajichanganye kwa Putin kule Ukraine watapukutika kama majani makavu
Wanatuzuga wote hao wanajuana , wamekubaliana kugawana Ukraine na Venezuela

Wote hao wapiga deal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…