Je, mahakama ilikosea kumfunga jela mhe. Lijualikali bila kuweka mbadala wa faini?

Livino Haule

Member
Mar 22, 2015
21
22
Tarehe 11/01/2017 ndugu NDAHANI N. MWENDA alipoandika katika ukurasa wake wa facebook taarifa ya Mhe. PETER LIJUALIKALI mbunge wa KILOMBERO kufungwa jela miezi 6 bila kupewa alternative ya kulipa faini kwanza; aliomba ufafanuzi wa kisheria iwapo mahakama ilifanya haki au sivyo! “Naombeni msaada wa kisheria….naombeni ufafanuzi juu ya hili.” Alisema Bw. Ndahani.

Nami nimepata nafasi ya kurejea sheria na kusoma baadhi ya maamuzi ya Mahakama za Juu za Tanzania (Case laws) ambayo yameweka msingi wa namna ya kutoa adhabu ya FAINI au KIFUNGO cha JELA pale sheria inapotamka adhabu hizi mbili kwa kosa fulani.

KWANZA nimejaribu kupitia Sheria inayotafsiri sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The Interpretation of Laws Act) No. 1/1996, specifically PART IX kuanzia kifungu cha 66 hadi 81 seehemu inayoelezea kuhusu MWENENDO NA ADHABU (Procedures and Penalties). Lakini hata hivyo nimegundua Sheria hiyo haijasema lolote kuhusu utaratibu wa mahakama kutoa adhabu ya faini au kifungo cha jela pale sheria za jinai (eg. Penal code/ Kanuni ya Adhabu) zinapotamka adhabu zote mbili kwa mbadala (alternatively).

PILI nimepitia na kusoma Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal code) inayoelezea juu ya masuala ya adhabu mbalimbali (punishments) katika CHAPTER VI hususani kifungu cha 29 kinachofafanua specifically kuhusu FAINI, hata hivyo sheria hiyo haijasema ni adhabu ipi ainze kutolewa kabla ya nyingine pale mahakama inapotaka kumhukumu mtuhumiwa kwa adhabu moja badala ya kutumia zote mbili kwa pamoja.

Kifungu cha 29(b) kimeeleza kwamba uamuzi wa kutoa faini au kifungo jela kwa kosa lililowekewa adhabu hizi mbili kwa mbadala, utakuwa chini ya mamlaka ya mahakama (discretion of the court) yenyewe. Pia kifungu hicho cha 29(c) (i) kimeelezea kwamba kwa mtuhumiwa aliyeshindwa kulipa faini mahakama itaweza kumwelekeza kwa mamlaka yake kutumikia kifungo cha jela kwa muda utakaopangwa na mahakama husika.

TATU nimesoma Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act) hususani PART IX ambayo inaeleza pamoja na mambo mengine, Convictions, judgment na sentences katika mahakama za chini na mahakama kuu. Hata hivyo sehemu hiyo yenye vifungu kuanzia cha 300 hadi 358 haijafafanua juu ya utaratibu wa utoaji wa adhabu ya faini au kifungo jela.
Swali linalo hoji usahihi au uhalali wakumfunga LIJUALIKALI jela bila kumpa nafasi ya kulipa faini, bado halijajibiwa na sheria hizi. The Laws are therefore Silent.

KWA HIYO kutokana na sheria zetu kuwa kimya juu ya kufafanua jambo hilo, Mahakama za Juu (Courts of Records) zimeweka utaratibu mahususi na maelekezo kupitia maamuzi mbalimbali ya kesi za jinai ambapo mahakama za chini zinalazimika kuufuata kama sharia (Case Laws are binding like any other laws of the land). Mhakama za chini (subordinate courts) hufungwa na maamuzi hayo ya mahakama za juu kwakuwa maamauzi hayo huwa sheria katika nchi. Nchini Tanzania mahakama za juu ni MAHAKAMA KUU na MAHAKAMA YA RUFAA.

MAAMUZI YA MAHAKAMA ZA JUU KATIKA KESI MBALIMBALI
Kesi zifuatazo zilizoamriwa na mahakama za juu zimeeleza na kuweka utaratibu ambao Hakimu au Jaji anatakiwa kuufuata, katika kumhukumu mtuhumiwa aliyekutwa na hatia kwa kosa la jinai katika; mazingira ambayo sheria imeweka adhabu zote mbili (faini au kifungo cha jela) kwa kosa husika.

(1) KESI YA SALUM SHABANI v R (1982) Criminal Appeal No.49
Bw. SALUM SHABAN (aliyekuwa kondakta wa gari) alikutwa na hatia katika mahakama ya wilaya bada ya kukubali kosa la kuzidisha mzigo katika gari kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani (Road Traffic Act) No. 30/1973 fungu la 39(2)(3) na (5).

Mahakama hiyo ilimhukumu kifungo jela miezi mitatu (3) bila kutoa option ya faini. Ndipo Salum alikata rufaa kwenda Mahakama Kuu kwa kutoridhika na kunyimwa nafasi ya kulipa faini.
Kesi hii ya Rufaa ilisikilizwa na kufanyiwa maamuzi na JAJI MTENGA Tarehe 07/06/1982, ambaye alitoa mtazamo wake kama ifuatavyo;

“Kazi ya kutoa adhabu kwa mtuhumiwa ni ngumu japo hueleweka kama ni maauzi ya mahakama husika (discretion of the trial court)….Jaji au Hakimu anayeamua adhabu ya mtuhumiwa aliyekutwa na hatia anatakiwa kutumia mamlaka yake kwa haki (judicially).”

Jaji MTENGA anaongeza kwa kusema, kabla ya kutoa adhabu mwamuzi huyo anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo;
• Ukubwa wa kosa (gravity of offence)
• Kama kosa hilo limezoeleka kutendwa mara nyingi katika jamii (prevalence of the offence)
• Maslahi ya jamii husika (interest of the society), na
• Iwapo mtuhumiwa anarekodi ya kuhusika na makosa mengine ya jinai/uzoefu katika kutenda jinai (criminal records of the accused person).

KWA HIYO katika mazingira hayo Jaji MTENGA akatoa mwelekeo kama alivyonukuliwa hapa;
“The option given by the Legislature means that in imposing sentence, the court must ascertain that a sentence of fine should first be imposed and in default of payment of the fine, then a sentence of imprisonment can be given.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi sana naweza kuandika mtazamo huo wa Jaji MTENGA kwa Kiswahili kama ifuatavyo;

“Uchaguzi (katia ya Faini au Kifungo jela) uliowekwa (katika sharia) na Bunge unamaana kwamba katika kumpangia adhabu mtuhumiwa, Mahakama ni lazima ihakikishe kwamba adhabu ya kulipa faini imetolewa kwanza na ikitokea mtuhumiwa ameshindwa kulipa faini hiyo, ndipo adhabu ya kifungo jela inaweza kutolewa dhidi yake.”

NB: Wazo la msingi hapa ni kwamba Mahakama hairuhusiwi kumpangia mtuhumiwa kifungo jela bila kumpa nafasi kwanza ya kulipa faini. Na hii ni lazima kama ilivyosisitizwa na Jaji kwa neno must.

(2) KESI YA MOHANED JUMA v REX. 1TLR 257
Mahakama katika kesi hii iliweka msimamo na utaratibu wa namna ya kupanga faini siyo kwa lengo la kumkomoa mtuhumiwa ashindwe kulipa ili aangukie katika kifungo jela, bali kiwango ambacho mtuhumiwa anao uwezo wa kumudu.
“Ingawa adhabu kali inaweza kutolewa kwa wakosaji wabaadhi ya makosa ya chini ya sharia kadhaa, hata hivyo FAINI inayopangwa katika makosa hayo zinatakiwa kuzingatia mazingira ya uwezo wa mtuhumiwa kumudu kuilipa.”
Wazo hili hata Jaji MTENGA pia aliliafiki katika kesi ya Salum Shabani (iliyoelezwa hapo juu).

(3) KESI YA NYAKULIMA d/o CHACHA v R, 1TLR 341
Hapa Jaji MOHAN alisisitiza pia wazo au takwa la kupanga faini inayolingana na uwezo wa kiuchumi wa mtuhumiwa.
“Kanuni ni kwamba faini inayopangwa inatakiwa kuwa kwa kiwango ambacho mtuhumiwa anategemea kuilipa (anao uwezo wa kuilipa).”
Msimamo huu pia ulikubaliwa na Jaji MTENGA katika kesi ya Salum Shabani.

(4) KESI YA R v BISON s/o MWANGA, 11TLR
Katika kesi hii Jaji MOHAN (aliyetajwa hapo juu) alifafanua kwa ukamilifu na kwa msisitizo juu ya namna bora ya kumpangia mtuhumiwa kulipa faini.

“Mahakama kabla ya kupanga faini inatakiwa kwanza kuuliza (conduct enquiries) kwa mtuhumiwa na kujiridhisha juu ya uwezo wake wa kifedha (financial standing), na hayo yote (maswali ya mahakama na majibu ya mtuhumiwa) yanatakiwa kufanywa sehemu ya kumbukumbu za mahakama (records of the court).”

(5) KESI YA SAMWEL MWENDAMANE v R (1967) HCD 457
Hapa Jaji SAID alisisitiza ukomo wa kiwango cha faini kutokana na kipato cha mtuhumiwa huyo. Jaji SAID alisema kwamba kiwango cha faini dhidi ya mtuhumiwa hakitakiwi kuzidi Theluthi Moja (1/3) ya kipato chake kwa mwezi.

HITIMISHO
Ni msimamo wa kisheria sasa kwamba mahakama inatakiwa kuzingatia mambo kadhaa panapokuwa na adhabu ya faini au kifungo jela, mambo hayo ni kama ifuatavyo;
a) Ni lazima kwanza kumpa mthumiwa adhabu ya faini,
b) Adhabu ya faini ilingane na uwezo wa mtuhumiwa kuilipa
c) Ili kujua uwezo wa kifedha ni lazima mahakama imuulize mtuhumiwa mwenyewe
d) Faini hiyo isizidi Theluthi moja (1/3) ya kipato chake kwa mwezi
e) Mtuhumiwa akishindwa kulipa faini ndipo atapangiwa adhabu ya kifungo jela

GENERAL RULE ni kwamba siyo haki na ni kosa kwa mahakama kumhukumu kifungo jela bila kumpangia faini kwanza mtuhumiwa aliyekutwa na hatia, pale sheria inapotoa uchaguzi wa adhabu hizi mbili.
Jaji MTENGA pia alisisitiza jambo hili kwa uwazi katika kesi ya SALUM SHABANI v R (1982) [Kama ilivyoelezwa mwanzoni kabisa] alipokosoa maamuzi ya mahakama ya wilaya ilyomfunga jela mtuhumiwa bila kumpangi faini;

“In the instant case the appellant was not given his right of option of sentence of fine as stipulated by Legislature in the subsection of the Act….this in my view is wrong and I hold that the trial magistrate did not exercise his discretion judicially in sentencing the appellant.”

Kwa Kiswahili tunaweza kuinukuu kauli hiyo kwa maneno yafuatayo “Katika kesi hii mkata rufaa hakupewa haki yake ya uchaguzi wa adhabu ya kulipa faini kama ilivyoelelezwa katika kifungu cha sharia husika….kitendo hicho kwa maoni yangu ni makosa na natamka kwamba Hakimu aliyeamua kesi hiyo hakutumia mamlaka yake kwa haki katika kumhukumu mkata rufaa.”

Maamuzi hayo ya kumfunga jela SALUM SHABANI badala ya kumpangia faini hayakutarajiwa pia na MWENDESHA MASHTAKA wa kesi hiyo aliyejulikana kwa jina Mrs. SHIYO ambaye hakupenda maamuzi ya Hakimu, hivyo katika Rufaa hiyo Mwendesha Mashtaka huyo alimsaidia Jaji MTENGA kurejea kesi nyingine ya R v JUMA MRISHO (1969) HCD61 ili kufanikisha kutangua maamuzi ya Mahakama ya wilaya na kumtoa mtuhumiwa kutoka jela.

(6) KESI YA R v JUMA MRISHO (1969)HCD61
Katika kesi hii Jaji BRAMBLE alikazia ulazima wa kuanza kutoa hukumu ya faini kwa mtuhumiwa aliyekutwa na hatia kwa mara ya kwanza (first time offender), na kuongeza kwamba isipokuwa adhabu ya kifungo jela itatolewa bila uchaguzi wa faini kwa mtuhumiwa mzoefu au mwenye tabia ysa kurudia makosa.
“Where the legislature has given an alternative of a fine for certain minor offences it would seem more appropriate to inflict this type of punishment rather than peremptory imprisonment. Of course, where there is a continuous flagrant disregard for the law, imprisonment would be the only answer.”

Yaani “Pale Bunge lilipoweka katika sheria mbadala wa faini kwa makosa madogo madogo basi izingatiwe kwamba ni vema zaidi kutoa adhabu hiyo kuliko kifungo jela. Isipokuwa kwa mtuhumiwa mwenye tabia ya kurudia makosa na kutokujali sheria, kumfunga jela ndilo jibu pekee.”

This is therefore the EXCEPTION to the General Rule, kwamba adhabu ya kifungo jela itatolewa bila faini kwa mtuhumiwa aliyerudia kutenda kosa la jinai wakati aliwahi kutiwa hatiani kwa kosa au makosa mengine wakati uliopita.
Kumbuka kuna msemo maarufu husema Every General Rule has Exception.

MTAZAMO WANGU KUHUSU MHE. LIJUALIKALI
1. Kama ni kweli kwamba Mhe. Lijualikali alikuwa na criminal records kwa makosa ya nyuma ambayo yalimtia hatiani na kupewa kifungo cha nje, na kwamba ni kweli aliwashambulia Polisi, basin ni wazi kwamba mahakama haikukosea na isingekuwa na namna nyingine. (Rejea kesi ya R v Juma Mrisho hapo juu).

2. Kama Mhe. Lijualikali hakuwa na criminal records kutiwa hatiani na makosa ya nyuma basi mahakama hiyo ilifanya kosa kumnyima option ya kulipa faini.

3. Kushinda rufaa yake katika mazingira haya kutategemea zaidi hoja mbili za Mhe. Lijualikali na mawakili wake;
(a) Mhe. Lijualikali akithibitisha na Mahakama ikijiridhisha kwamba hakuwa na criminal records, hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote mahakamani; au

(b) Mhe. Lijualikali akithibitisha na Mahakama ikijiridhisha kwamba kesi iliyomfunga ilitungwa tu kwa nia ovu (malicious prosecution with fabricated evidence) kutokana na sababu za kutunga tu, zenye chuki ili kumwangamiza kisiasa.
Hoja hii pia itategemea zaidi uzito wa ushahidi (weight and credibility of evidence) wa upande wowote and not necessarily the truth (ukweli), na pia kwa kushabihiana na uhuru wa Jaji husika au mahakama itakaposikilizwa rufaa ya kesi hiyo.

JAPOKUWA mimi binafsi naiona kesi hiyo katika sura ya kisiasa zaidi na mwendelezo wa michezo ileile iliyowakuta Tundu Lissu, Godbless Lema, na wengine waliokutwa na mkono wachuma wa serikali hii ya awamu ya tano.

By Livino Ngalimitumba Haule (Lingaha)
18/01/2017 Mbeya – Tanzania.
 
Hukumu zinaendeshwa kwa records za hukumu zilizopita badala ya Sheria ? Nadhani hii ni michezo tu... Angelipa fine tu
 
Hukumu zinaendeshwa kwa records za hukumu zilizopita badala ya Sheria ? Nadhani hii ni michezo tu... Angelipa fine tu
Hahahaha sio michezo ni utaratibu wa Common Law Legal system kwamba maamuzi ya mahakama za juu hutusaidia kama sheria hasa katika mazingira ambayo sheria haikufanya "coverage" ya jambo fulani sawa sawa.
 
Inategemea unaiangalia kwa macho yapi. Kama unalitazama kwa kuzingatia maagizo kutoka juu hukumu hiyo ilikuwa sahihi. Lakini ukilitazama kwa jicho la natural justice Siyo sawa
 
Inategemea unaiangalia kwa macho yapi. Kama unalitazama kwa kuzingatia maagizo kutoka juu hukumu hiyo ilikuwa sahihi. Lakini ukilitazama kwa jicho la natural justice Siyo sawa
Hahahaha "agizo kutoka juu" eti. Ni mwendo qa kukomesha na kuwaburuza wapinzani kwelikweli utadhani wao ni wahamiaji haramu au wamefanya jaribio la uhaini. Tuombe Mungu tu aisee!
 
Sikuona mahakama kuwafunga bila fine

1. Yule alietengeneza na kuuza dawa feki za ukimwi

2. Ditopile Ukiwaona Ramadhani mzuzuri...Aliuwa deleva wa daladala .........

3. Waliochepusha bomba la mafuta bandarin nakulibia taifa miaaka kadhaa....wengi walikufa kwa kukosa matibabu nk

4. wezi na waporaji wa twiga wetu, swala nk

Nadhani siasa imeingia mahakamani....sasa hivi mahakimu na majaji hawafuati weledi wa kazi zao bali wanafuata maagizo yakisiasa kufurahisha wanasiasa.

Hili linaweza kutuingiza katika machafuko ya ulipizaji visasi tusipokuwa makini....fungafunga kwa wanasiasa wa upinzani kunaudhi na nichukizo kwa ndugu najamaa zao.....lazima mahakama ijitafakali maana machafuko huanzia popote pale.
 
Sikuona mahakama kuwafunga bila fine

1. Yule alietengeneza na kuuza dawa feki za ukimwi

2. Ditopile Ukiwaona Ramadhani mzuzuri...Aliuwa deleva wa daladala .........

3. Waliochepusha bomba la mafuta bandarin nakulibia taifa miaaka kadhaa....wengi walikufa kwa kukosa matibabu nk

4. wezi na waporaji wa twiga wetu, swala nk

Nadhani siasa imeingia mahakamani....sasa hivi mahakimu na majaji hawafuati weledi wa kazi zao bali wanafuata maagizo yakisiasa kufurahisha wanasiasa.

Hili linaweza kutuingiza katika machafuko ya ulipizaji visasi tusipokuwa makini....fungafunga kwa wanasiasa wa upinzani kunaudhi na nichukizo kwa ndugu najamaa zao.....lazima mahakama ijitafakali maana machafuko huanzia popote pale.
Shida ipo hapa kaka. Mwamuzi ni mtawala sio absolutely mahakama.
 
Hahahaha "agizo kutoka juu" eti. Ni mwendo qa kukomesha na kuwaburuza wapinzani kwelikweli utadhani wao ni wahamiaji haramu au wamefanya jaribio la uhaini. Tuombe Mungu tu aisee!
Hivi hao anaotaka waombewe huko serikalini, kwa nini huwa hawasemi waombewe kitu gani.??
 
Kwa mara nyingine narudia KULILIA na KUJUTA TENA KUKOSA FURSA YA KUSOMA SHERIA. Ipo siku Mungu atafanya njia niwepo kwa nia ya kuwasaidia wanyonge.
 
Pale:

KESI ya MBUZI mwamzi anapokuwa ni FISI huku mshitaki wa MBUZI akiwa ni MBWEHA.

au

KESI YA NYANI ANAPEWA NGEDERE ATOLEE UAMUZI.
 
Hahahaha sio michezo ni utaratibu wa Common Law Legal system kwamba maamuzi ya mahakama za juu hutusaidia kama sheria hasa katika mazingira ambayo sheria haikufanya "coverage" ya jambo fulani sawa sawa.
Ni upuuzi mtupu huo ina maana muache kutumia Sheria na muangalie kesi za wengine ipo siku mtachukua hadi hukumu aliyopewa Yesu kuhukumia mtu mwingine kisa mazingira yanafanana... Hii ndio inaonesha wazi mnaenda Shule ili majiriwe na wenye fedha.. So hamna faida kwa uwepo wenu
 
Kwa mara nyingine narudia KULILIA na KUJUTA TENA KUKOSA FURSA YA KUSOMA SHERIA. Ipo siku Mungu atafanya njia niwepo kwa nia ya kuwasaidia wanyonge.
Bado una muda wa kusoma maadamu upo hai. Make an effort utafanikiwa tu.
 
Ni hatari sana hakimu kuendesha kesi kwa kuamini wapinzani wakosaji na hii itaumiza wengi sana kama thinking ya namna hii ya mahakimu itaendelea.
 
Kwa mara nyingine narudia KULILIA na KUJUTA TENA KUKOSA FURSA YA KUSOMA SHERIA. Ipo siku Mungu atafanya njia niwepo kwa nia ya kuwasaidia wanyonge.
Kwanini ujute wakati hukumu zinatolewa kuzingatia record za hukumu za zamani.. Vitabu vinawekwa kando... Nilistushwa sana kusikia kesi ya Lema nayo imeingia kwenye vitabu vya Sheria its means mtu atakayetenda kama Lema baadae atatiwa ndani bila dhamana na tukae tusubiri hukumu tuendelee kuona vituko vya wapuuzi Wa Sheria wana vyo endekeza matumbo yao mbele katika elimu inayotia aibu wanasheria ndio uozo Wa kwanza rejea mahakama ya mauaji ya Rwanda hadi kagame aliwafokea na kuwambia ni majizi tu na mapumbavu hizo kesi yeye angezimaliza kwa siku chache tu.
 
Haya yoote fafanueni lakini msisahau kuwa maamuzi ya wengi ni maamuzi ya Mungu. Huyu mbunge alichaguliwa na watu wengi na kumbuka kosa lake sio kukwepa kodi, kumuibia mtu au kufumaniwa bali harakati za kisiasa!
Iko siku hata kama ni kizazi kijacho hizi aibu hazitatolewa ufafanuzi bali zitawafuata watu makaburini huko huko. Ni kizazi cha ngapi leo wanakumbuka hadithi za chief Mangungo za kuuza ardhi kwa vipande vya nguo na sukari!? Jiulize wakati akifanya haya alikuwa na umaarufu unaoambatana na hadhi kiasi gani!?
Tukitaka kesho njema ni lazima kutenda haki na kuheshimiana leo, tunavyochelewa kukubali hayo tunachelewesha neema pia.
 
Shida kubwa ni mfumo unaoibuka anayetenda kufuata mfumo wa boss wake promotion kwake grantee bila kuangalia utawala wa sheria.
 
Back
Top Bottom