Je Magufuli akisaidiwa Pole×2 atafanikiwa kuirudisha CCM ya Nyerere?

chikundi

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
8,245
2,000
Tumeshuhudia mageuzi kadhaa anayoyafanya Mh Magufuli kama mwenyekiti wa CCM ya matajiri kuirudisha kuwa ya wote kama enzi za Mwalimu.

Hii ndiyo ccm ya Mwalimu

Wanachama/wananchi ndio waliokuwa wanamshawishi mgombea agombee bila kujali kipato chake

Wanachama/wananchi walimchangia mgombea gharama za kampeni kwa kuuza mazao na mifugo yao hivyo hata mgombea kapuku alipata nafasi ya kugombea na kuchaguliwa.

Mgombea hasa wa ubunge alikuwa anaishi kwenye jimbo lake na hata akipata ubunge hakuamia Dar.

Hakukuwa na rushwa ya wazi wazi ya uchaguzi ndani ya ccm na nje ya ccm.

Wabunge na wajumbe wa mikutano ya taifa na mikoa ya ccm walitumia usafiri wa mabus kama wanafunzi na kuhudhuria vikao vya bunge n.k kisha kurudishwa kwenye majimbo ama mikoa yao mara baada ya vikao kwisha.

Haikuhitaji uwe mtoto wa mkubwa au kada wa ccm kupata nafasi ya kugombea na kuchaguliwa katika chama.
 
Macos

JF-Expert Member
May 12, 2008
1,934

Wewe uko katika ndoto. Hivi ulikuwapo hapo CCM ya nyerere ikiwa ya masikini...unawajua walokua viongozi wa CCM wakati wa Mwalimu ?
hebu nitajie aliekua masikini na mkulima
hata katika serikali alishawahi kumchagua mkulima na mfugaji..?
wacheni kasumba hizo...japo mwalimu alikua mjamaa lakini alijaribu kuweka viongozi wennye sifa za elimu , sio ukulima au umasikini. qualification hio haikuwapo.
siasa za wakati ule ni za chama kimoja, amri ya mwenye kiti ya mwisho, chama kilihika hatamu,
mwalimu aliwaweka kina Amir Jamal , Alnoor Kassoum , Rupia, Bomani , Mtei , Kahama, Sokoine, Kawawa, na wengine hawa hawakua masikini . walikua wana uwezo na matajiri na elimu ukimuondoa kawawa hakua na elimu ya kutosha...lakini hakua masikini hivyo.
kuhusu kununua uongozi , basi hapo zamani sifa kubwa ujipendekeze uwe shawishi hivi ndo utapata uongozi..lakini sio kwa kushika jembe,...
ccm inatakiwa isonge mbele zaidi, ifikiri mbele sio nyuma ..
iwe na mawazo ya kimaendeleo iwe na wivu wa maendeleo ...iachane na mambo ya 47...inatakiwa iongozwe na viongozi wapya kabisa wasiokua na mawazo ya kikale...nchi zinatuacha nyuma sisi tunabaki kutafuta kifaru john...au kuzuia wasiongeee,
miji na nchi zinajengwa na wenye nchi na sio kwa ndoto..
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Nyerere alikuwa anawashawishi wananchi, alikuwa na uwezo wa kujenga hoja mpaka watu wanamuelewa, kwa ujumla nyerere alikuwa akili kubwa
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,637
2,000
Rekebisha kichwa cha habari,kada mwenzangu!
mengine yote umepatia!
Pungufu kibao kaandika huyo mwenzio kuhusu hicho chama chenu, halafu mnajisahau na kuanza kupiga propaganda za kizee eti ccm inakubalika kwa kuwa kinachukia rushwa!!! Halafu kukubalika kwenu kunakuwa kuko ndani ya jeshi na tume ya uchaguzi. Shukuruni mpo kwenye nchi ya watu walio kwenye usingizi wa woga na unafiki.
 
Kajolijo

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,383
2,000
Tumeshuhudia mageuzi kadhaa anayoyafanya Mh Magufuli kama mwenyekiti wa CCM ya matajiri kuirudisha kuwa ya wote kama enzi za Mwalimu.

Hii ndiyo ccm ya Mwalimu

Wanachama/wananchi ndio waliokuwa wanamshawishi mgombea agombee bila kujali kipato chake

Wanachama/wananchi walimchangia mgombea gharama za kampeni kwa kuuza mazao na mifugo yao hivyo hata mgombea kapuku alipata nafasi ya kugombea na kuchaguliwa.

Mgombea hasa wa ubunge alikuwa anaishi kwenye jimbo lake na hata akipata ubunge hakuamia Dar.

Hakukuwa na rushwa ya wazi wazi ya uchaguzi ndani ya ccm na nje ya ccm.

Wabunge na wajumbe wa mikutano ya taifa na mikoa ya ccm walitumia usafiri wa mabus kama wanafunzi na kuhudhuria vikao vya bunge n.k kisha kurudishwa kwenye majimbo ama mikoa yao mara baada ya vikao kwisha.

Haikuhitaji uwe mtoto wa mkubwa au kada wa ccm kupata nafasi ya kugombea na kuchaguliwa katika chama.
Inaezekana chumvi kuingia kwny bahari na kurudi na uchumvi ule ule eeh?

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom