Je mafanikio ya mtoto katika masomo yake hufuata akili ya wazazi wake?

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,519
Ninapenda kuelemishwa kuwa mafanikio ya mtoto katika masomo yake hufuata akili ya wazazi wake?. Mfano kama Baba ni msomi na Mama ni msomi je akili ya mtoto itakuwa kama wazazi wake?.
 
Haya masuala ya shule na usomi ni mfumo tu uliowekwa haujafungamana kwa namna yoyote na undani wa mtu (biologically) ...Maana ilivyo, ili uitwe msomi lazma upitie kwenye mfumo huu...Na wazazi kuwa wasomi haimaanishi na watoto lazma wapitie mfumo huu..... Mimi nina masters lakini mwanangu akishajua mahesabu tu nitamuingiza kwenye kampuni yangu ajifunze vitu practically....Mpaka wewe unamaliza chuo na kuanza kutafuta mtaji (baada ya kukosa ajira) , mwanangu ana experience ya kutosha kuendesha mambo na kashajenga connections za kibiashara nyingi tu.....Wewe utakaa nyumbani unajiita msomi, mwanangu anapiga pesa.....


TAHADHARI: Kufoji vyeti ni hatari kwa afya yako
 
Ninapenda kuelemishwa kuwa mafanikio ya mtoto katika masomo yake hufuata akili ya wazazi wake?. Mfano kama Baba ni msomi na Mama ni msomi je akili ya mtoto itakuwa kama wazazi wake?.
Kuna factor nyingi za mtoto kuperform darasani,mtoto hurithi baadhi ya vitu kutoka kwa wazazi wake hasa uwezo wa kiakili ktk masomo,pia inasemekana mtoto hurithi akili za mama,hivyo mama akiwa mbumbumbu kuna uwezekano mkubwa wa mkubwa wa mtoto pia kuwa mbumbumbu!
 
Kuwa msomi na kuwa na akili ni vitu viwili tofauti.
Mtoto hurithi akili kutoka kwa wazazi wake (baba na mama), hapo hutegemea ni ya yupi imekuwa dominant.
Kuna vizazi vya watu wenye akili ndogo, hata kusoma ni shida lakini watafikia ngazi za juu kwa kukesha, na hata kuweka miguu kwenye maji baridi.
Wapo wenye akili nzuri, wakipata nafasi ya kusoma ni waelewa na hawahitaji muda mrefu kukariri, hawa hata wakiwa na elimu ya daraja la chini bado wanafanya vizuri.
 
Back
Top Bottom