Pi Network
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 290
- 319
Subira ya Mohamed Bouazizi ilifikia kikomo mnamo Desemba 17, 2010. Alikuwa mchuuzi wa barabarani nchini Tunisia, mwenye umri wa miaka 26, na alikuwa amekata tamaa kwa sababu ya kukosa kazi nzuri. Pia alijua kwamba maofisa wafisadi walikuwa na zoea la kudai hongo. Asubuhi ya tarehe hiyo, maofisa walichukua mapeasi, ndizi, na matofaa ambayo Mohamed alikuwa akiuza. Walipochukua mizani yake, alikataa, na watu fulani walioshuhudia jambo hilo walisema kwamba alipigwa kofi na mwanamke ambaye ni ofisa wa polisi.
Akiwa amefedheheshwa na kukasirika, Mohamed alienda kwenye ofisi ya serikali iliyokuwa karibu ili kutoa malalamiko yake lakini hakuna aliyemsikiliza. Akiwa mbele ya jengo hilo, inasemekana kwamba alisema hivi kwa sauti kubwa, “Mnataka niiruzuku familia yangu kwa njia gani?” Baada ya kujimwagia petroli, alijiwasha moto. Alikufa kutokana na majeraha ya moto majuma matatu hivi baadaye.
Tendo hilo la Mohamed Bouazizi lilikuwa na athari kubwa kwa watu wa Tunisia na nchi nyingine. Watu wengi wanasema kwamba tendo lake ndilo lililochochea maasi yaliyoipindua serikali ya nchi hiyo, na punde si punde maandamano yakaenea katika nchi nyingine za Kiarabu. Bunge la Uingereza lilimtunukia Bouazizi na watu wengine wanne Tuzo la Sakharov la Uhuru wa Kutoa Maoni, na gazeti The Times la London lilimweka katika orodha yao ya mtu aliyekuwa na uvutano mkubwa zaidi katika mwaka wa 2011.
Kama kisa hicho kinavyoonyesha, maandamano yanaweza kuwa na uvutano mkubwa sana.
Lakini, ni nini chanzo cha maandamano hayo?
Je, kuna suluhisho lingine bora zaidi ya kuandamana?