Je, Maandamano ya CHADEMA yana uhalali kisheria?

RABIN GHYOOT

Member
Joined
Sep 17, 2014
Posts
10
Reaction score
2
CHADEMA wanataka kuandamana kwasababu wamekatazwa kufanya mikutano ya hadhara ya kuzunguka nchi nzima.

Swali la msingi la kujiuliza ni je mikutano hii ya viongozi wa CHADEMA kuzunguka nchi nzima baada ya uchaguzi ina uhalali wa kisheria?

Au swali jingine la kujiuliza ni kuna tofauti gani kati ya mikutano hii ya kuzunguka nchi nzima na kampeni?

Tofauti inaweza kuonekana kwenye lengo la kauli zitakazokuwa zinatolewa na viongozi wa chama katika mikutano hiyo.

Kama lengo la kauli zinazotolewa na viongozi katika mikutano hiyo ni kushawishi watu wapigie kura chama chao na wagombea wao katika uchaguzi ujao basi hiyo ni kampeni ya uchaguzi.

Sasa swali la msingi la kujiuliza je wakati huu ni wakati sahihi wakufanya mikutano ya aina hiyo?

Jibu unapata kwamba mikutano ya aina hii uwa inapangiwa ratiba na Tume ya uchaguzi (NEC) na kutangazwa kwenye vyombo vya habari. Tume ya uchaguzi (NEC) ni tume ambayo iko kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Tume ya uchaguzi (NEC) uwa inatangaza ratiba ya kampeni ya uchaguzi wiki chache kabla ya mchakato rasmi kuanza. Muongozo wa maadili kwa ajili ya wagombea na vyama vya siasa unaanza kufanya kazi mara moja baada ya tangazo hilo.

Mchakato mzima wa uchaguzi uwa unachukua kati ya wiki 5 hadi wiki 8. Lakini kampeni rasmi hazichukuwi zaidi ya wiki mbili; zinaanza pale orodha ya wagombea inapotengenezwa na zinaisha masaa 48 kabla ya kusitisha zoezi la kupiga kura.

Wakati wa kampeni vyama vya siasa na wagombea wanatarajiwa kutii muongozo wa maadili uliowekwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) baada ya kukubaliana na vyama vya siasa.

Muongozo wa maadili ni kwa ajili ya kutunza Amani na Utulivu na kuepuka migongano kati ya vyama vya siasa na vile vile kuepuka migongano kati ya wafuasi wa vyama. Muongozo wa maadili unadumu mpaka pale matokeo yanapotangazwa. Ni muongozo huu ndio unaosema chama tawala kisitumie mamlaka yake ya kiserikali kujipendelea.

Lakini katika kipindi hiki ambacho wakati wa kampeni za uchaguzi umekwisha, muongozo huo wa maadili haufanyi kazi, hivyo sitashangaa chama tawala kikijipendelea.

Nchi haiwezi kuwa katika hali ya kampeni kwa kipindi cha miaka mitano (5). Utaratibu uliowekwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) ni; kampeni zinaanza pale orodha ya wagombea inapotengenezwa na zinaisha masaa 48 kabla ya kusitisha zoezi la kupiga kura.

Hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na sheria ya uchaguzi, hasa ukizingatia Tume ya Uchaguzi (NEC) iko kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

Rais wa nchi kama kiongozi mkuu wa nchi anayo haki ya kufafanua maamuzi, mipango na mustakabali wa Taifa, kitendo hiki sio kampeni ya uchaguzi.

Ni upotoshaji kusema haki ya kufanya mikutano ni ya kikatiba, lakini haki ya kuwekea vikwazo vya msingi (reasonable restrictions) hiyo mikutano sio ya kikatiba. Soma Ibara ya 30 (2) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Katiba za mataifa mengi zinatoa haki ya kikatiba kwa dola (polisi) kuweka vikwazo vya msingi (reasonable restriction) kwa haki zote za kikatiba. Na katiba inaenda mbali zaidi wakati wa tahadhari (emergency) inaruhusu dola kusitisha (suspend) haki zote za kikatiba.

Tatizo CHADEMA wakiwa wanataka kutafsiri kipengele cha KATIBA huwa wanakinyofoa na kukitenganisha na vipengele vingine alafu wanakipa maana wanayotaka wao. Wanafanya hivi makusudi wakijuwa wanapotosha.

Maana yakipengele kimoja cha KATIBA mara nyingi inategemea maana ya kipengele kingine cha KATIBA, hivyo kutenganisha alafu kutafsiri ni kupotosha umma.
 
Mimi naona mdahalo unaweza ukawepo juu ya kwamba polisi wameweka vikwazo vya msingi (reasonable restriction)
au sio, lakini hata katika mdahalo huu sioni CHADEMA kama wanaweza kushinda, kwasababu kama chama cha siasa hawana sifa wala nyenzo za kufanya tathimini ya hali ya usalama. Sifa na nyenzo za kufanyia tathimini hali ya usalama wanazo polisi. Sasa watawashinda polisi kwa hoja zipi.
 
NINGEPENDA TUNDU LISSU AJIBU HII
 
CHADEMA wanataka kuandamana kwasababu wamekatazwa kufanya mikutano ya hadhara ya kuzunguka nchi nzima.

Swali la msingi la kujiuliza ni je mikutano hii ya viongozi wa CHADEMA kuzunguka nchi nzima baada ya uchaguzi ina uhalali wa kisheria?

Au swali jingine la kujiuliza ni kuna tofauti gani kati ya mikutano hii ya kuzunguka nchi nzima na kampeni?

Tofauti inaweza kuonekana kwenye lengo la kauli zitakazokuwa zinatolewa na viongozi wa chama katika mikutano hiyo.

Kama lengo la kauli zinazotolewa na viongozi katika mikutano hiyo ni kushawishi watu wapigie kura chama chao na wagombea wao katika uchaguzi ujao basi hiyo ni kampeni ya uchaguzi.

Sasa swali la msingi la kujiuliza je wakati huu ni wakati sahihi wakufanya mikutano ya aina hiyo?

Jibu unapata kwamba mikutano ya aina hii uwa inapangiwa ratiba na Tume ya uchaguzi (NEC) na kutangazwa kwenye vyombo vya habari. Tume ya uchaguzi (NEC) ni tume ambayo iko kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Tume ya uchaguzi (NEC) uwa inatangaza ratiba ya kampeni ya uchaguzi wiki chache kabla ya mchakato rasmi kuanza. Muongozo wa maadili kwa ajili ya wagombea na vyama vya siasa unaanza kufanya kazi mara moja baada ya tangazo hilo.

Mchakato mzima wa uchaguzi uwa unachukua kati ya wiki 5 hadi wiki 8. Lakini kampeni rasmi hazichukuwi zaidi ya wiki mbili; zinaanza pale orodha ya wagombea inapotengenezwa na zinaisha masaa 48 kabla ya kusitisha zoezi la kupiga kura.

Wakati wa kampeni vyama vya siasa na wagombea wanatarajiwa kutii muongozo wa maadili uliowekwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) baada ya kukubaliana na vyama vya siasa.

Muongozo wa maadili ni kwa ajili ya kutunza Amani na Utulivu na kuepuka migongano kati ya vyama vya siasa na vile vile kuepuka migongano kati ya wafuasi wa vyama. Muongozo wa maadili unadumu mpaka pale matokeo yanapotangazwa. Ni muongozo huu ndio unaosema chama tawala kisitumie mamlaka yake ya kiserikali kujipendelea.

Lakini katika kipindi hiki ambacho wakati wa kampeni za uchaguzi umekwisha, muongozo huo wa maadili haufanyi kazi, hivyo sitashangaa chama tawala kikijipendelea.

Nchi haiwezi kuwa katika hali ya kampeni kwa kipindi cha miaka mitano (5). Utaratibu uliowekwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) ni; kampeni zinaanza pale orodha ya wagombea inapotengenezwa na zinaisha masaa 48 kabla ya kusitisha zoezi la kupiga kura.

Hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na sheria ya uchaguzi, hasa ukizingatia Tume ya Uchaguzi (NEC) iko kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

Rais wa nchi kama kiongozi mkuu wa nchi anayo haki ya kufafanua maamuzi, mipango na mustakabali wa Taifa, kitendo hiki sio kampeni ya uchaguzi.

Ni upotoshaji kusema haki ya kufanya mikutano ni ya kikatiba, lakini haki ya kuwekea vikwazo vya msingi (reasonable restrictions) hiyo mikutano sio ya kikatiba. Soma Ibara ya 30 (2) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Katiba za mataifa mengi zinatoa haki ya kikatiba kwa dola (polisi) kuweka vikwazo vya msingi (reasonable restriction) kwa haki zote za kikatiba. Na katiba inaenda mbali zaidi wakati wa tahadhari (emergency) inaruhusu dola kusitisha (suspend) haki zote za kikatiba.

Tatizo CHADEMA wakiwa wanataka kutafsiri kipengele cha KATIBA huwa wanakinyofoa na kukitenganisha na vipengele vingine alafu wanakipa maana wanayotaka wao. Wanafanya hivi makusudi wakijuwa wanapotosha.

Maana yakipengele kimoja cha KATIBA mara nyingi inategemea maana ya kipengele kingine cha KATIBA, hivyo kutenganisha alafu kutafsiri ni kupotosha umma.
Naona hii imewafunga midomo BAVICHA. Inaonyesha wazi jinsi UKUTA unavyotaka unavyotaka kuvunja amri halali ya polisi iliyowekwa kwa mujibu wa katiba.
 
Back
Top Bottom