Lucious
Member
- Mar 25, 2011
- 47
- 22
Sifungamani na upande wowote, naogopa kutekwa. Napenda maisha na familia yangu, naipenda Tanzania ya zamani sio ya sasa.
Je, maandamano ni haki ya kikatiba? Ndio swali najiuliza. Je dikteta ni mtu wa namna gani? Je, viongozi wa dini wana haki ya kufanya au kuongelea siasa?
Naanza kuwaza kwa sauti kwa swali langu la 3. Yesu kristo kipindi kile anasaka wanafunzi wake alipita sehemu mbalimbali; kwa wakusanya kodi, mahekaluni na hata akaoshwa miguu yake na malaya.
Kwenye maandamano/mikutano yake alifanya siasa pia. Aliulizwa je, ni haki kulipa kodi? Akawaomba sarafu na kusema mpeni Kaisari vilivyo vyake na Mungu vilivyo vyake. Alijua fika kwenye makutano wanakuja watu wengi, leo misikitini na makanisani sio kosa kukumbusha viongozi wetu kuhusu mienendo au kujisahau sana kwa kulewa madaraka. Wakiomba kura wanaenda makanisani au misikitini au kwa waganga. Imani bila matendo imekufa.
Daudi alianguka kwa kulewa madaraka. Nebukadreza na Wafarao pia. Hekima za Suleiman zinatakiwa. Ukiona dini inaingilia hayo acha kutaka kuombewa au kama neno katubu ni kosa au wakisema ni kosa kisheria rudi kwenye Katiba. Kuombewa sio haki ya kiongozi ni utashi wa mtu. Makanisani au misikitini wanakutana watu so lazima vyote visemwe na kukumbushana.
Swali langu lingine ni je, maandamano ni haki? Katiba yetu inasemaje?
Ibara ya 20(1): Kila mtu anastahili kuwa huru bila kuathiri sheria za nchi, kukutana kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani. Ni haki kiķatiba kuandamana ukisoma sana hakuna sheria inayosema polisi anatoa kibali au anapaswa kuzuia, hakuna mtu aliyeko juu ya sheria hata rais. Ni haki na wajibu wa watu wote kuheshimu utawala wa sheria.
Tatu ninawaza dikteta ni nani? Mwalimu Nyerere alisema, "Katiba yetu inampa rais mamlaka sana na akiyatumia vibaya anaweza kuwa dikteta. Mwaka 1995 Mwalimu alisema "Kuogopwa ni sifa na ada ya madikteta, viongozi halisi hawapendi kuishiriki sifa hii. Kujenga mazoea ya kutii viongozi hata kwenye mambo haramu ni dalili ya woga, ni kukaribisha udikteta"
Leo nimewaza hayo tu, naogopa kutekwa.