Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,430
JE! KUOTA UNAFANYA TENDO LA NDOA NI DHAMBI?
Neno la Msingi:
Yuda 1:8
“Kadhalika na hawa, katika KUOTA KWAO, huutia MWILI UCHAFU, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu.”
Watu wengi wameshindwa kufahamu kwa upana juu ya kuota unafanya tendo la ndoa na kujikuta umechafuka maana yake ni nini?. Kuna madhara gani mtu huyapata kwa kufanya tendo la ndoa katika ndoto. Biblia inasema nanyi mtaifahamu kweli nayo kweli itawaweka huru. Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuufahamu ukweli huu unaohusiana na kuota ndoto za kufanya mapenzi na kujikuta umejichafua au wakati mwingine unakuwa haujajichafua.
Yohana 8:32
“tena MTAIFAHAMU KWELI, nayo hiyo KWELI ITAWAWEKA HURU.”
1. KUOTA UNAFANYA TENDO LA NDOA NI NINI?
Mtu kuota anafanya tendo la ndoa katika ndoto ni kufanya tendo la ndoa na pepo wa mahaba ambao ni viumbe wa kiroho. Ni kwamba mtu huyu hafanyi tendo la ndoa na wanadamu wa kawaida bali anafanya na majini. Hiyo ni dhambi mbaya na yenye madhara makubwa ya kiroho na kimwili kwa mtu anayefanya hivyo.
SI HALALI kwa mtu aliyeokoka awe ni kijana asiyeoa, binti asiyeolewa au mwanandoa kuota ndoto za kufanya tendo la ndoa awapo usingizini. Nyakati za Agano la kale ilikuwa kitendo cha shahawa kutoka katika mwili wako ilikuwa unatengwa hadi jioni kwa kuwa umekuwa najisi.
Walawi 15:16
“Na mtu ye yote akitokwa na SHAHAWA yake, ndipo ataoga mwili wake wote majini, naye atakuwa NAJISI hata jioni.”
Walawi 17:7
“Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale MAJINI, ambao HUWAFUATA ili wafanye UASHERATI nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.”
Kwahiyo namna yoyote ile ya KUOTA unafanya tendo la ndoa iwe ni kwa kijana, binti au mwanandoa ni kufanya mapenzi na majini. Majini wanaweza kuja kwa sura yoyote ile iwe ni ya mume au mke, au mume au mke aliyekufa, au ndugu yako, au mpenzi wako wa zamani.
2. JE! KUOTA UNAFANYA TENDO LA NDOA NI DHAMBI?
Kuota unafanya TENDO la Ndoa na majini ni dhambi kama vile mtu anavyofanya dhambi nyingine yoyote ile. Tena kibaya zaidi mtu wa namna hiyo anafanya dhambi na uchafu na majini mahaba. Ni mbaya mno kuliko unavyofikiri.
Yuda 1:6-7
"Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe (majini), lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. Kama vile Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa kando kando, waliofuata UASHERATI kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya ASILI, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele. Kadhalika na hawa katika KUOTA kwao, huutia MWILI UCHAFU, hukataa kutawaliwa, na kuyatukana matukufu."
Kuota unafanya tendo la ndoa ni dhambi kwa kuwa unafanya tendo hilo na viumbe wa kiroho (majini). Kwahiyo kitendo chochote cha namna hiyo ni HARAMU.
3. MADHARA YA KUFANYA TENDO LA NDOA KATIKA NDOTO
Kuna madhara makubwa sana ya kufanya tendo la ndoa katika ndoto na majini, haya chini ni baadhi ya madhara hayo:-
i). Kutokupata mtoto kwa yule aliyeko katika ndoa
Wako wanawake wengi wenye matatizo ya kupata watoto kutokana na kuwa na mahusiano na majini kwa njia ya ndoto. Wako baadhi ya wanawake wanafahamu hata majini hayo kwa majin yao. Huwezi kupata mtoto ukiwa na mahusiano na majini hayo.
ii). Mikosi, nuksi na balaa
Mikosi, nuksi na balaa huambatana na mtu anayefanya TENDO la Ndoa katika ndoto. Pepo wa mikosi na balaa humfunika mtu wa namna hiyo. Biashara au kazi na mengineyo huingia katika shida kutokana na pepo hao.
iii). Mafarakano katika mahusiano na ndoa
Ndoa nyingi zenye mafarakano ya kudumu hutokana na majini mahaba ambao hufanya kazi pacha na pepo wa mafarakano. Kitu kidogo tu kinaweza kusababisha ugomvi mkubwa sana, hiyo ni kazi ya pepo hao. Kama ni binti yuko kwenye mahusiano ya uchumba pepo wa Mahaba husababisha kuharibika kwa mahusiano hayo.
iv). Hasira za mara kwa mara zisizo na kichwa wala miguu
Mtu ambaye anashiriki Tendo la Ndoa kwa njia ya ndoto huwa na hasira ambazo hazina kichwa wala miguu. Kitu kidogo tu hasira kali ya kutosha. Ulikuwa unamsubiri mume wako vizuri utashangaa baada ya kutokea tu hapo nyumbani, unakasirika bila sababu, hao ni pepo Mahaba.
v). Kutokuoa au kuolewa kwa Kijana au Binti
Shida ya kuoa na kuolewa mtu yeyote ambaye anaota anafanya mapenzi katika ndoto. Pepo hao hudai mhusika ni mume au mke wao. Na wakati mwingine hufikia mtu KUOTA ananyonyesha au mjamzito au wakati mwingine anafunga ndoa, hao ni pepo Mahaba.
vi). Kupungua kwa nguvu za kiume kwa mwanaume
Kwa wanaume kuota unafanya mapenzi katika ndoto husababisha upungufu wa nguvu za kiume na wakati mwingine kukosa uwezo wa kuzalisha ( )
vii). Kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa Wanandoa
Kuota unafanya tendo la ndoa huondoa hamu ya Tendo la Ndoa kwa wanandoa. Kama ni mwanamke unajikuta upo upo tu, hausikii hamu yoyote katika mwili wako. Hisia uhamishwa kutokana na shughuli za pepo hao wa Mahaba.
viii). Kuvunjika kwa ndoa
Kuvunjika kwa ndoa nyingi husababishwa na pepo wa Mahaba ambao wao huwa hawapendi yule wanayemmiliki kuwa na uhusiano na mwanadamu kwa hiyo hutafuta mlango wa kuvunja hiyo ndoa. Wanandoa wanaweza wakawa walikuwa wanapendana sana wakiingia hapo pepo Mahaba ugomvi, mafarakano na hasira hutokeza na mwishowe ndoa kuvunjika.
ix). Husababisha vifo
Hatua isipochukuliwa mapema pepo wa Mahaba husababisha hata mauti kwa mmoja kati ya mwanandoa. Au mtoto anayezaliwa katika Ndoa huweza kusababisha mauti yake. Hawapendi huyu mwanamke wanayefanya naye mapenzi katika ndoto awe na watoto.
x). Kurudi nyuma Kiroho
Mtu anayefanya mapenzi katika ndoto husababisha kurudi nyuma kiroho na mwishowe kufa kabisa kiroho kwa kuacha wokovu. Kitendo cha KUOTA ndoto humkatisha tamaa mpendwa aliyeokoka na hivyo kuamua kufanya dhambi kimwili kabisa.
Hosea 7:8-9
“EFRAIMU AJICHANGANYA na mataifa; Efraimu ni mkate usiogeuzwa. WAGENI WAMEKULA NGUVU ZAKE, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari.”
4. JINSI YA KUFANYA UNAPOOTA HIVYO
i). Kutubu dhambi hiyo na nyinginezo
Ni vema kutubu kila dhambi katika maisha yetu ikiwepo ya kufanya mapenzi kwenye ndoto. Tunapotubu kwa kumaanisha tunapata msamaha wa dhambi na kupewa ushindi. Upoota tu, ukishaamka tubu hiyo dhambi.
Mithali 28:13
“Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.”
ii). Kufunguliwa katika kifungo cha pepo wa Mahaba
Tafuta mtumishi aliyepakwa mafuta na Mungu kwa ajili ya huduma ya "ushauri na kufunguliwa" ili Bwana akufungue katika kifungo hicho cha pepo Mahaba.
Luka 4:18
“Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia WAFUNGWA KUFUNGULIWA KWAO, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,”
iii). Kukemea kila ndoto yenye viashiria vya majini mahaba
Ukishaamka na kutoka katika ndoto hiyo au kabla haujalala kemea kazi zote za pepo wa mahaba.
Yakobo 4:7
“Basi mtiini Mungu. MPINGENI SHETANI, naye atawakimbia.”
iv). Kudumu katika Utakatifu
Kudumu katika utakatifu kutakusaidia binafsi kuishi maisha ya ushindi dhidi ya pepo wa mahaba. Pepo wanaitwa pepo wachafu, kwahiyo wanapoenda sehemu iliyo chafu. Ukidumu katika utakatifu unafunga mlango wa pepo hao kuingia na kukaa ndani yako.
1 Petro 1:15-16
“bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, NINYI NANYI IWENI WATAKATIFU katika MWENENDO wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu."
2 Timotheo 2:21
“Basi ikiwa mtu AMEJITAKASA KWA KUJITENGA NA HAO, atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema.”
v). Kudumu katika maombi
Omba juu ya ulinzi wa Mungu unapokwenda kulala. Jiombee nafsi yako kwamba Mungu akulinde na kazi zote za Shetani.
Zaburi 91:3, 15
“Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;”
vi). Kukaa katika Neno
Kukaa katika Neno ni kukaa ndani ya Yesu. Yesu anatajwa kama Neno la Mungu kwahiyo ukikaa ndani yak ushindi ni lazima. Nyakati hizi watu wengi hawataki kukaa katika Neno la Mungu bali wanataka "kutabiriwa" tu, hiyo ni hatari kwa maisha yako ya kiroho na kimwili.
Yohana 1:1
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”
Yohana 15:7
“Ninyi mkikaa ndani yangu, na MANENO YANGU YAKIKAA NDANI YENU, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”
SALA YA TOBA:
Sema Maneno haya:-
Mungu Baba ninakuja mbele zako, Mimi ni mwenye dhambi. Ninatubu dhambi zangu zote ikiwepo ya kufanya mapenzi katika ndoto, naomba unisamehe. Baba ninakushukuru kwa kuwa umenisamehe na kunipokea kama mwana mpotevu. Asante Baba kwa kuniokoa katika jina la Yesu._
Amina!!!!!!!!!
NIKUTAKIE WAKATI MWEMA