Je, kuna njama kuiuza TANESCO pia?

Je, kuna njama kuiuza TANESCO pia?

voicer

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2020
Posts
5,545
Reaction score
11,943
Tumesikia na pia tulitaarifiwa kwamba serikali ya JMT ilisaini mikataba thelathini huko "UAE".

Inatia Shaka pale tunapoona ghafla mgao wa Umeme ukiwa umerudi kwa kasi nchini bila maelezo wala sababu za kueleweka kutolewa na Serikali.

Ndio pale tunapohofia kwamba isije kuwa kuna njama za makusudi za kuidhoofisha "TANESCO" ili ishindwe kufanya kazi kwa Ufanisi, wake na hatimae ionekane inafanya kazi kwa hasara na hatimae itimizwe ile kauli ya Rais aliyoitoa hivi karibuni jijini Arusha.

kwamba Mashirika yote ya Umma.ambayo yanafanya kazi kwa Hasara na Yasiyo na ufanisi bila kutegemea ruzuku ya serikali.Sasa yatauzwa.

Haiwezekani kwamba umeme unakatika nchini kwa visingizio lukuki,visivyo na ukweli wala uthibitisho Kila uchao.
Huku wahusika pamoja na serikali kwa ujumla wakiwa kimya kama vile hawana taarifa.

Nasema hivyo kwa sababu mabwawa yote ya kufua umeme nchini yako na maji ya kutosha(kwa sababuhatujataariwa na vyombo husika kuwa kuna upungufumpaka sasa). Mitambo ya gesi pia ikiwa inafanya kazi.kwa kiwango kikubwa kabisa.ingawa ndio ilitumika ili ku-establish mgao huu.

Tunajua kwamba Serikali kupitia wizara ya Nishati na Waziri Makamba. Wameingia mikataba ya mabilioni ya shilingi hivi karibuni.kwa ahadi kwamba suluhisho la Umeme wa kudumu na madhubuti ndio sasa lilikuwa linaenda kutatuliwa na Waziri Makamba!

Huku tukiaminishwa na Waziri Makamba kwamba Hayati Magufuli,alikuwa ameichakaza mitambo kwa kiasi cha kutidha.Na sasa wanarekebisha pamoja na kuweka TANESCO katika mifumo bora na ya kisasa zaidi.

Lakini pamoja na matumizi ya mabilioni yote hayo.Bado tunashuhudia nchi ikuwa gizani huku wananchi wakiendelea kutaabika na mgao nchi nzima.

Hayo yote yanatokea,viongozi na serikali wako kimya kama vile hawalioni tatizo hili ambalo ni hatari kwa uchumi wa taifa.

Tumeshuhudia mabadiliko ya baraza la Mawaziri.ikiwemo hiyo ya Nishati.lakimi waziri mpya ameendelea ma ububu huku akiibuka kuomgelea mambo ya ustawi wa jamii badala yamambo ya wizara ya Nishati.

Hizi dalili sio nzuri na huenda ni mkakati mwingine ili kuhalaisha uuzwaji wa TANESCO kama ilivyotokea kwa Bandari zetu.

Chonde chonde!
Serikali sasa ni wakati sahihi wa kutoka na kushughurikia suala la ukosefu wa nishati hii muhimu.
 
Sjasoma yote ila Tanesco wako na shida pahala nmelipia maunganisho ya umeme 320960 wik ya pil wanajibu kiurahs tu hakuna vfaa store kwaajil ya wateja wapya
Pia kuna thread humu mteja analalamika LUKU imegoma kusoma Token,leo siku ya nne bado wanamwambia kuwa wanashughulikia!

Hii inatia Shaka kwamba huenda kuna jambo linapangwa mahala fulani.
 
"Uku akiibuka kuongelea mambo ya ustawi WA jamii badala ya mambo ya wizara ya nishati"
Tulimsikia wote mkuu!
Anaongelea maadili ya watoto kuyowatii wazazi....
 
Inatia Shaka pale tunapoona ghafla mgao wa Umeme ukiwa umerudi kwa kasi nchini bila maelezo wala sababu za kueleweka kutolewa na Serikali.

Ndio pale tunapohofia kwamba isije kuwa kuna njama za makusudi za kuidhoofisha "TANESCO" ili ishindwe kufanya kazi kwa Ufanisi, wake na hatimae ionekane inafanya kazi kwa hasara na hatimae itimizwe ile kauli ya Rais aliyoitoa hivi karibuni jijini Arusha.
Naona JPM aliwaharibu sana na conspiracy theories.... Acheni kuficha ufanisi wenu mdogo kwenye kusingizia "hujuma"!! Unataka useme kabla ya hizo "tetesi" kuliwahi tokea Tanesco kuwa na ufanisi hata siku moja?

CCM mmefeli Kila kitu Bora mpishe wengine watawale ila hii tabia ya Kila failure yenu kusingizia ni hujuma mlianza nayo tokea enzi za JPM, chukueni responsibility ya matatizo yenu na mkiri mmeshindwa kuongoza mtupishe 2025.
 
Katika kipindi chote cha awamu ya Magufuli tuliusahau mgao wa Umeme nchini Tanzania.
Wewe labda ulikuwa Burundi ukiwa umemkimbia Magufuli.
 
...hv nikigombea urais si mtanipa kura? Ntakuwa naskiliza mawazo yenu humu nini kifanyike Na wapi nifanye hivi... CHAGUA RAYNS 2025
 
Katika kipindi chote cha awamu ya Magufuli tuliusahau mgao wa Umeme nchini Tanzania.
Wewe labda ulikuwa Burundi ukiwa umemkimbia Magufuli.
Sio kweli, mgao ulikua hautangazwi tu ila umeme ulikua unakatika sana tu ila haitangazwi. Nakumbuka ilikua kila jumamosi nikiwa home hakuna umeme between 2018-19 na Kuna nyuzi humu nyingi tu zilikua zinauliza kama Kuna mgao wa kimya kimya ngoja ni attacha hapa.

Katika kipindi chote cha awamu ya Magufuli tuliusahau mgao wa Umeme nchini Tanzania.
Wewe labda ulikuwa Burundi ukiwa umemkimbia Magufuli.
Anachomaanisha jamaa mkifeli kutatua matatizo kwa sababu ya uwezo wenu mdogo mnasingizia kuhujumiwa
 
Wauze tuu hata na bwawa lenyewe wachukue , kama kuna kitu kingine wamesahau waotodheshe wajiuze . PONDA MALI KUFA KWAJA.
 
Back
Top Bottom