Drydon
Senior Member
- Mar 11, 2019
- 125
- 193
Na. Fred Kibano - Arusha
Serikali imesema inaendelea na maandalizi ya mifumo mipya ya ajira na uhamisho ambayo itaondoa changamoto ya uhaba wa watumishi walimu kwenye shule zake za msingi na sekondari hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli, ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha pamoja na Viongozi wa Elimu ngazi ya juu na chini hususani Elimu Jijini Arusha ambapo amesema changamoto iliyopo ya walimu kuhama au kuajiriwa itazingatia uhaba uliopo kwenye shule zilizopo pembezoni.
Mweli amesema mifumo hiyo itaruhusu kufunguka kwa Mikoa, wilaya, Kata na hata Vijiji au Mitaa mahali shule hizo zilipo na kwamba mwombaji wa ajira au uhamisho atalazimika kuomba na kwenda kwenye shule iliyo na nafasi na si vinginevyo.
Mfumo mwingine ambao umeanza kufanya kazi ni ule wa kupokea na kukagua madeni ya walimu ambayo yatahakikiwa na kutunzwa bila kupotea kama ilivyokuwa hapo awali ambapo utunzaji wa kumbukumbu ulikuwa mgumu. Mfumo huu unatarajiwa kuondoa kero na malalamiko ya madeni ya walimu na watumishi wengine kupotea kabla ya malipo.
“nimeongea na Viongozi wa elimu na baadhi ya walimu na kama mnavyofahahamu tumetengeneza mifumo mingi sana, mfumo wa kwanza ni mfumo wa kupokea na kukagua madeni ya walimu pamoja na watumishi wengine na tumeshaanza na mkoa wa Dodoma na sasa tumeshapita na kuwaambia walimu tumeandaa mfumo huu”
Aidha, amesema kumekuwepo na mlundikano wa watumishi hususani walimu kwenye majiji, miji na baadhi ya manispaa na kuyafanya maeneo ya pembezoni kukosa walimu kutokana kupungua kwa idadi ya walimu inayohitaji na hivyo maeneo yenye mlundikano yatapelekewa walimu kwa sababu maalum.
Kwa upande wake Afisa Elimu sekondari Jiji la Arusha Valentine Makuka amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi kutatua kero za walimu kwa kuzingatia haki zao kama mishahara, madaraja, masomo na uhamisho ambapo masuala yote haya yametolewa ufafanuzi kwenye kikao kazi kilichofanyika.
Naye Christina Marandu Mwalimu Halmashauri ya Meru shule ya msingi Kerikenyi mmoja wa washiriki wa kikao ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tatu kwa kuwapatia jumla ya shilingi milioni 60 ambayo imejenga madarasa matatu kwa thamani halisi ya fedha na kuwa mfano wilayani Meru.
“shule yangu imepata shilingi milioni 60 kwa ajili ya kujenga madarasa matatu kwani kila mtu amekuwa akiizungumzia Serikali kuwa ni chachu ya kuleta maendeleo ya wananchi kwenye shule na hata kata yetu na hii imenipa nafasi ya kutembea kifua mbele kwa jinsi Serikali inavyofanya”
Miradi aliyotembelea Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli katika Jiji la Arusha ni shule ya msingi Msasani, sekondari ya Suye na Halmashauri ya Meru shule ya sekondari Kisimiri.