Wakuu habari za Leo, naomba kufahamishwa juu ya jambo hili.
Ninatamani sana kupata degree yangu kwa njia ya mtandao (online studies) kutoka vyuo vilivyoko nje ya nchi.
Moja ya chuo ambacho kimenivutia sana ni hiki kilichoko Uganda ambacho kinaitwa International university of East Africa- Uganda, chuo hiki kinakozi ambazo zinatolewa kwa njia ya elimu masafa yaani E-learning
Swali langu ni kuwa je nikisomo kozi hizi kwa mfumo wa online na baada ya kuhitimu vyeti vyangu vinaweza tambuliwa hapa nchini na kuniwezesha kupata promotion huku kazini kwangu?
Waliowahi pitia hili jambo naomba msaada wenu wapendwa.
Usomaji kwa njia ya online haukwepeki kwa karne hii. Utapata materials, vitabu, audio, video +live video conference ambazo hazina tofauti na ukihudhuria darasani.
Wasiliana na TCU ujue vyuo ambavyo wanavitambua.
Mimi nimesoma na ninasoma kozi nyingi sana online. Ila vyuo vyangu ni vya Amerika.
Usomaji kwa njia ya online haukwepeki kwa karne hii. Utapata materials, vitabu, audio, video +live video conference ambazo hazina tofauti na ukihudhuria darasani...