Je, Kozi kwa njia ya elimu masafa zinatambulika Tanzania?

swagy

Senior Member
Jan 23, 2018
102
250
Wakuu habari za Leo, naomba kufahamishwa juu ya jambo hili.

Ninatamani sana kupata degree yangu kwa njia ya mtandao (online studies) kutoka vyuo vilivyoko nje ya nchi.

Moja ya chuo ambacho kimenivutia sana ni hiki kilichoko Uganda ambacho kinaitwa International university of East Africa- Uganda, chuo hiki kinakozi ambazo zinatolewa kwa njia ya elimu masafa yaani E-learning

Swali langu ni kuwa je nikisomo kozi hizi kwa mfumo wa online na baada ya kuhitimu vyeti vyangu vinaweza tambuliwa hapa nchini na kuniwezesha kupata promotion huku kazini kwangu?

Waliowahi pitia hili jambo naomba msaada wenu wapendwa.
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
2,140
2,000
Usomaji kwa njia ya online haukwepeki kwa karne hii. Utapata materials, vitabu, audio, video +live video conference ambazo hazina tofauti na ukihudhuria darasani.

Wasiliana na TCU ujue vyuo ambavyo wanavitambua.

Mimi nimesoma na ninasoma kozi nyingi sana online. Ila vyuo vyangu ni vya Amerika.
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,745
2,000
Bora usome open university kuliko hivyo vya nje, unaweza kuta unasoma chuo hata waganda hawakifahamu, yani ni chuo kipo kwenye laptop ya mtu.

Bora ukasome Amazon, au Wale wanajiita Wema training institute, utakuwa unaibiwa unajua unaibiwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom