Je, Kikwete atafanikiwa kuikarabati CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Kikwete atafanikiwa kuikarabati CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Feb 23, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Send to a friend Tuesday, 22 February 2011 20:55

  [​IMG]Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete

  Na Nizar Visram
  MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akihutubia kilele cha chama tawala kutimiza miaka 34 mjini Dodoma, alisema wakati umefika sasa kwa chama kufumuliwa na kuundwa upya kutokana na maadili yake. Kama vile mageuzi ya Ulaya mashariki yalivyoilazimisha CCM kuruhusu vyama vya upinzani, inawezakana mara hii Kikwete ameshawishiwa na matukio mawili

  La kwanza ni haya mapinzuzi ya kidemokrasia yanayoikumba nchi za Kiarabu. Huko Misri na Tunisia vyama tawala vilitupwa kapuni na wananchi wenye hasira, na makada wake wakayeyuka hewani. Mapinduzi hayo sasa yanaenea katika Yemen, Algeria, Morocco, Bahrain, Libya na kadhalika

  Labda Kikwete alishawishika na mapinduzi haya. Yawezekana pia hapa nyumbani alishinikizwa na matokeo ya uchaguzi wa Oktoba mwaka jana. Chama kilichozoea kutumia maneno kama ushindi wa kishindo na ushindi wa sunami sasa kimejikuta kikididimia. Baadhi ya makada waliendelea na jeuri yao kwa kutamba kama walivyozoea. Lakini kada mkuu Kikwete hakuficha ukweli.

  Ukweli ni kuwa katika historia ya nchi hii chama tawala hakijawahi kupata pigo kama la Oktoba 2010. Mara ya kwanza chama kilipata kura chache na upinzani kuongeza kura zake pamoja na viti bungeni. Mara ya kwanza wananchi wengi hawakujitokeza kupiga kura. Haya tumewahi kujadili katika safu hii Sasa Kikwete ameona umuhimu wa kufanya mabadiliko katika chama.

  Wakati alipotangaza nia hiyo alitoa mfano wa nyoka anayebadili ngozi yake kila baada ya muda. Akasema na chama nacho pia kinapaswa kubadili gamba lake. Kwa maneno mengine chama kinaiga mfano wa nyoka.

  Hatujui ni mabadiliko gani atakayoyafanya Kikwete katika chama, ila tunajua kuwa hii si mara ya kwanza kutangaza mabadiliko katika chama. Tunakumbuka jinsi alivyotangaza kuwafanya viongozi wachague uongozi au biashara. Wengine tulikumbuka miiko ya uongozi chini ya Azimio la Arusha. Lakini baada ya muda mada hiyo ikasauliwa na hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika uongozi.

  Mara hii pia inawezakana nia yake hiyo ikagonga mwamba. Ni kwa sababu si rahisi kufanya mabadiliko katika chama kilichotekwa nyara na matajiri na mafisadi. Hiki si chama kile cha wafanyakazi na wakulima licha ya nembo katika bendera yake na katiba yake inavyosema. Waonaofikiria bado wanaweza kurudisha uongozi wa chama kama kilivyokuwa zamani wanajidanganya.

  Suali la kujiuliza ni vipi Kikwete atafanikiwa kuunda upya uongozi wa chama ambacho wakati wa kura za maoni mwaka jana kadi feki za uanachama zililizagaa nchini. Kadi hizo feki zilitolewa kwa wapiga kura mamluki. Orodha za wanachama zilipotezwa kwa njama za makusudi na daftari feki zikatayarishwa zikiwa na wanachama mamluki.

  Wanachama halali wakanyimwa haki ya kuwachagua wagombea wanaowataka. Matokeo yake ni kuvurugika kwa kura za maoni katika majimbo mengi. Hiki ni chama ambacho washindi wake waliibuka na ushindi kwa kusajili wanachama bandia ambao wamegawiwa kadi bandia ili waweze kupiga kura. Hivi ndivyo chama kilivyochagua na kuwateua viongozi na wawakilishi wake. Je Kikwete atafanikiwa kufuma upya uongozi wa chama?

  Atafanikiwaje kukirekebisha chama ambacho makada wake wanahongwa bila ya kificho? Unakuta kule Songea mjini kada anadai arudushiwe fedha zake sh 800,000 baada ya kushindwa udiwani. Anatangaza kuwa alitoa fedha hizo kwa viongozi wa chama kwa makubaliano ya kumsaidia kushinda katika kinyang’anyiro.

  Alisema fedha hizo ni za “kuwaweka sawa” wanachama ili wamchague kama mgombea. Lakini fedha zake zikaliwa na viongozi na akaukosa uteuzi kama mgombea. Hiki ni chama ambacho madiwani wake na wabunge ndivyo walivyochaguliwa si Songea tu bali hata kwengineko.

  Haya yalithibitishwa hata na katibu mkuu Yusuf Makamba aliyesema “kila mmoja alihonga ila tu walizidiana dau” akimaanisha kuwa hakuna mgombea aliyekuwa msafi. Yaani chama kiliwapitisha wenye “dau kubwa”.Halafu Kikwete anatuambia anakusudia kukirekebisha chama.

  Atafanikiwaje kuikarabati CCM ambayo makada wake katika wilaya ya Kahama walisusia mkesha wa Mwenge wa Uhuru kwa sababu waliambiwa hakuna fungu la posho lililoandaliwa kwa ajili ya mbio za mwenge mwaka huu?

  Chama ambacho makada wake wilayani wanakimbilia posho kitawezaje kutoa wabunge na mawaziri wanaojituma? Tusishangae kama nao wakidai posho mbili wanapohudhuria kikao kimoja. Tusishangae kama wao wakitumia vyeo vyao kujitajirisha kwa kuvamia ardhi na mali za umma na kudai asilimia 25 wanaposaini mikataba ya umeme.

  Kwani ukweli ni kuwa hata chama chenyewe kimejitajirisha kwa kuvamia mali za taifa kama viwanja na majengo yaliyotokana na jasho la Watanzania wote. Chama hakioni hata aibu kwa “udhalimu” kilioufanya kwa kukwapua na kuhodhi mali za umma. Kama Kikwete anataka kukirekebisha chama basi aanze kwa kurudisha mali hizi kabla ya wananchi kupata ujasiri wa kudai haki zao.

  Atawezaje kufanya ukarabati huo aliouahidi iwapo hata makamo wake wa mwenyekiti, Pius Msekwa, anazungumzia uozo huu kwa kusema eti tatizo la rushwa haliwezi kubebeshwa chama chake kwa sababu ni tatizo la taifa zima! Hawa ni wakuu wa chama waliozoea kutamba na kujivunia mafanikio ya serikali. “Mazuri ni yetu, mabaya ni yao.” Huu ni uhuni ambao Kikwete atakuwa na kazi kubwa kupambana nao

  Si ajabu mbunge wa CCM aliyejiunga na upinzani (akashinda uchaguzi) alisema “Hakuna CCM asilia, iliyopo ni CCM mamboleo iliyovaa joho la CCM asilia.”
  0713-562181
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Defiant Gaddafi vows to fight on

  In televised speech, Libyan leader blames youths inspired by regional events for uprising and vows to die a 'martyr'. ( 23-Feb-2011 )

  SWALI HUMU: UTAMADUNI WA KURITHISHA WATOTO WA WAKUBWA
  UKUBWA TANZANIA CHANZO CHAKE NI WAPI???


  Nani anayejua hasa darasa la huyu King of Kings?

  Kwa mtaji wa hutuba aliyoitao hivi majuzi ni mara mia angjinyamazia tu hivyo tungeendelea kumfikiria mstaarabu fulani hivi. Kwa kujiunga kwake jeshini akiwa na umri wa miaka 12 (child soldier) wala hatuhitaji kuuliza kama 'ALIONEWA SANA YEYE', 'AKADHALILISHWA SANA GADDAFI' hivyo kuja kupata kamwanya wa kuongoza nchi kwa mtindo wake mwenyewe hivi sasa anarudishia ngumi kwa jamii nzima ya Libya.

  Tujifunze kitu basi na sisi hapa kwamba wale tuliowahi kuwaondoa kwenye nyadhifa fulani hapa nyumbani kufuatia kashfa iliyogoma kwisha katikati yetu hadi leo, nao wakija tu kupata urais wa nchi hii mtindo wao wenyewe na tusifikirie matendo yao kutofautiana sana na ya huyu nduli hapa.

  Hakika shule iliomuingia mtu na kutulia ndani mwake ni muhimu zaidi tena sana kuliko shule ya kupitia hata kama madarasa yako ni mengi kimahesabu vidoleni.

  Kanali Gaddafi ajikaanga kwa ulimi wake mwenyewe. Na watoto wake , masikini ya Mungu, ndio kabisaa wanaamini taifa zima la Libya ni kama shamba binafsi la ukoo kwa baba yao.

  Nikitazama ya Ben Ali wa Tunisia, nikamgeukia Hosni Mubarak wa Misri na kumtaza mzee huyu ambaye kimawazo ni 'chipukizi' tu, na mwenendo mzima wa ushiriki wa familia zao katika mambo ya utawala wa nchi, Wa-Tanzania wenzangu NAPATA MAJIBU KUBWA SANA HAPA HAPA NYUMBANI kwamba ni kwa nini kati ya marais wetu wote wanne ni wawili tu kati yao ambao waonekana kupenda saana KUWARITHISHA UKUBWA WA TAIFA HILI kimtindo!!

  Endapo Hussein Mwinyi hatojiuzulu ya Gongolamboto kwa kiburi tu kama ya watoto wa marais niliotangulia kuwataja kaskazini mwa bara hili basi huenda hata UKUBWA WA ZANZIBAR unaotazamiwa kwake ukagoma lakini ya Muungano ndio kabisaaaa wa kusikia tu redioni.

  Je, inamaana wazee wengine akina Salim Ahmed Salim, Sinde Warioba, Mwalimu Nyerere, Phili Mangula, Joseph Rwegasira, Salmin Amour, Seif Shariff Hamad, Duni Haji Duni, Bibi Titi, Mama Mongela, Edith Mnuo, Dr Slaa, Prof Mwandosya, Prof Baregu, Mzee Kisumo, Edwin Mtei, Kambona, na wengine wengi tu ... wao hawana watoto wa kuwea nao kutamani kuwarithisha UKUBWA???

  Katika hili tayari Vijana wa Tanzania TUMEWASOMA MCHEZO MZIMA na majibu tunayo!!!
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Kikwete ameshaiua CCM, sasa hivi anaiandalia mazishi ya kifahari, si mnamjua kulu daba wetu?
   
 4. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  JK don't have the guts to restructure CCM and he certainly know that he can't do that....... Waliomzunguka hawawezi mpa hiyo nafasi kamwe.... wanajua JK amelala wapi, amekula nn, kajipaka nn etc..... Kumbukeni ni mzuri kuongea tena kwa mambo anayoandikiwa bila hata kupitia na kuhariri, lakini utendaji wote mnaujua......
   
Loading...