Je, Kevin yupo sahihi?

Je, Kevin yupo sahihi?

Mtuache

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
260
Reaction score
707
Kuna attachment hapo chini, because ya out of option nimeshindwa kuiweka kwa hapa juu. Please iangalie alafu ndo tuje tuendelee na huu mjadala

Nimeiona hio picha maeneo mengi mtandao, kuna watu watamuona Kevi miyeyusho sana kwamba mwamba anapenda kulelewa mvivu, anataka kuwa kibenteni ila mimi nakwambia Kevi yupo sahihi kwa 100%

Kwanini nasema hivyo?

Dr. Regnar Wilhelm Nurkse alizungumzia juu ya hoja ya underdevelopment (kutokuendelea) kuwa ni kwa sababu ya vicious cycle of poverty iliyopo kwenye familia zetu ambapo kuna utegemezi mkubwa, uzalishaji hafifu kipato kidogo n.k

Haya ndio hufanya aliye na kipato kutoendelea maana walio chini yake ni wengi na wanataka wale kupitia wewe na hapo utaishia kupata mahitaji ya kila siku tu huwezi kujijenga mwishowe na kizazi chako kinakuja kurithi majina ya ukoo tu.

Nadhani Kevi anaamini ukioa mke masikini na wewe kwenu ni masikini basi ujue mpambano juu ya umasikini ni mkubwa mno. Na matokeo yake ni aidha muendelee kuwa masikini au mfanikiwe kwa kiasi kidogo.

Kutokana na nilivyomuelewa Kevin anataka mpenzi mwenye hela au ambaye kwao wanahela sio amtegemee bali iwe starting point nzuri against umasikini, kwa haraka haraka ni kama jamaa anataka kulelewa ila tujaribu kuangalia kwa upana zaidi.

Angetaka kulelewa asingewaza juu ya watoto wake kwamba watasomaje, nyumba watakayoishi itakuaje, hakuna sehemu ameonesha kwamba anataka dem mwenye ela kwaajili yake. Lengo na focus kubwa ni juu ya watoto wake na familia yake kiujumla.

Ukioa au kuolewa na masikini au jamii masikini ni kwa 90% lazima familia yako iwe masikini tuu. Umasikini hurithiwa, umasikinj ni ugonjwa wa kuambukizwa.

Ukibahatika kuwa na pesa kwenu, mfano kwenu mmezaliwa 6 alafu wewe pekee ndo ukawa na pesa basi tambua mapambano ni makubwa, hujanusurika bado. Walio chini wengi na wana nguvu ya kukuvuta chini zaidi ya waliojuu hivyo ni rahisi wewe kuanguka kuliko kwenda juu

Jamaa anaamini pesa zinatafutwa lakini pia maji hufuata mkondo. Mkioana wote masikini itawabidi muiinue kwanza familia zenu ndo mujiinue na nyie, huwezi somesha watoto wako shule za nzuri za gharama kubwa alafu watoto wa kaka yako wanasoma shule mbaya sana. Utakuwa mbinafsi wa kiwango cha lami.

Huwezi jenga nyumba nzuri ilihali wakwe zako hawaishi poa, hizi zote ni driving forces za kukuzuia kufikia mafanikio mapema.

Kwa asilimia 98% ya watanzania masikini wamerithi umasikini kutoka kwa wazazi wao au walezi wao. Babu yako alikuwa masikini, akamrithisha Baba yako, na Baba yako akakurithisha wewe na iko wazi wewe pia utarithisha watoto wako

Kwenye hii Dunia kuna watu au mambo EXCEPTIONAL. Hawa ni aina ya watu ambao hawafuatu na wanavunja kanuni, desturi au asili aliyokuwepo. Hawa watu ni wachache sana na inahitajika nguvu, juhudi za ziada kua'attaint hii kitu.

Mfano wajaluo ni weusi kwa rangi, na hutambuliwa kutokana na weusi uliokithiri mpaka kumeremeta wakati mwengine. Hivyo sio ajabu mtu akisema Wajaluo ni weusi na watu wakamuelewa ingawaje wapo wajaluo weupe tena pee pee japo ni wachache. Sasa hao Wajaluo weupe wachache ndio tunaita Exceptional yaani wamevunja kanuni ya asili ya weusi.

HAYO NI MAWAZO YANGU EMBU NIPE MAWAZO YAKO. UNAHISI KEVIN YUPO SAHIHI? KWANINI?
1672674041120.jpg

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
 
Mwamba Kelvin nimemkubali sana, however, most victims are the Men
 
Nimeshindwa hata nianzie wapi, ila najuwa wote hayatuhusu🤐🤐
 
Yuko sahihi sana, ila tu hapo kutafuta mwanamke mwenye pesa kaferi.
Men are the victims bora jamaa anajiachia kirahisi tu, kakaza moyo.
 
Kevoo akiendekeza hizo pigo ataziweka sehemu zake hajakubwa matatani
 
Kuna attachment hapo chini, juu ya out of option nimeshindwa kuiweka kwa hapa juu. Please iangalie alafu ndo tuje tuendelee na huu mjadala

Nimeiona hio picha maeneo mengi mtandao, kuna watu watamuona Kevi miyeyusho sana kwamba mwamba anapenda kulelewa mvivu, anataka kuwa kibenteni ila mimi nakwambia Kevi yupo sahihi kwa 100%

Kwanini nasema hivyo?

Mwana natharia anaitwa mmoja Dr. Nurkisy alizungumzia juu ya hoja ya underdevelopment (kutokuendelea) kuwa ni kwa sababu ya vicious cycle of poverty iliyopo kwenye familia zetu ambapo kuna utegemezi mkubwa, uzalishaji hafifu kipato kidogo n.k

Haya ndio hufanya aliye na kipato kutoendelea maana walio chini yake ni wengi na wanataka wale kupitia wewe na hapo utaishia kupata mahitaji ya kila siku tu huwezi kujijenga mwishowe na kizazi chako kinakuja kurithi majina ya ukoo tu.

Nadhani Kevi anaamini ukioa mke masikini na wewe kwenu ni masikini basi ujue mapambano juu ya umasikini ni mkubwa mno. Na matokeo yake ni aidha muendelee kuwa masikini au mfanikiwe kwa kiasi kidogo.

Kutokana na nilivyomuelewa Kevin anataka mpenzi masikini sio amtegemee bali iwe starting point nzuri against umasikini, kwa haraka haraka ni kama jamaa anataka kulelewa ila tujaribu kuangalia kwa upana zaidi.

Angetaka kulelewa asingewaza juu ya watoto wake kwamba watasoma somaje, nyumba watakayoishi itakuaje, hakuna sehemu ameonesha kwamba anataka dem mwenye ela kwaajili yake. Lengo na focus kubwa ni juu ya watoto wake na familia yake kiujumla.

Jamaa anaamini pesa zinatafutwa lakini pia maji hufuata mkondo. Mkioana wote masikini itawabidi muiinue kwanza familia zenu ndo mujiinue na nyie, huwezi somesha watoto wako shule za nzuri za gharama kubwa alafu watoto wa kaka yako wanasoma shule mbaya sana. Utakuwa mbinafsi wa kiwango cha lami.

Huwezi jenga nyumba nzuri ilihali wakwe zako hawaishi poa, hizi zote ni driving forces za kukuzuia kufikia mafanikio mapema.

HAYO NI MAWAZO YANGU EMBU NIPE MAWAZO YAKO. UNAHISI KEVIN YUPO SAHIHI? KWANINI? View attachment 2466875

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
Umekosea jina la mwanafalsafa husika rekebisha.
 
Madem maskini keroo kama umeme wa makambaa big up kev
 
Back
Top Bottom