Je, kesi ya mhasibu wa TAKUKURU " itasisimua" kama ile ya Kamanda Zombe?


J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
13,531
Likes
11,365
Points
280
J

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
13,531 11,365 280
Najiuliza tu na hasa nikikumbuka ile kesi ya mauaji ya wafanyabiashara ya madini iliyokuwa inamkabili kamanda Zombe na askari wengine.

Nilimsikia huyu mhasibu wa Takukuru akijieleza jana kupitia ITV na kwa namna anavyojiamini nilimlinganisha kabisa na Zombe alivyojiamini kiasi cha kumuelekeza cha kuongea wakili wake pale mahakamani huku akijitanabaisha kama " kachero aliyebobea".

Mwanzoni sikumtilia maanani sana lakini hukumu ilipotoka nikaamini kweli Zombe ni kachero mbobezi. Ila kwa huyu mhasibu wa Takukuru sina hakika kama yeye pia ni mhasibu mbobezi ambaye kabla auditor hajauliza swali yeye tayari anakuwa na majibu. Ni hayo tu!!
 

Forum statistics

Threads 1,236,005
Members 474,928
Posts 29,243,188