Je, katika maisha yako ulishawahi kuhisi Mungu anakupendelea kutokana na mambo yanayokutokea?

{True story}
Jana nilienda K.Koo ndani ndani mle nikanunua kitu kisha nikaondoka, sasa nilipokua narudi nikagundua nilichonunua hakinitoshi hivyo nikaamua nikirudishe wanibadilishie. Mimi sio mwenyeji wa hilo soko mitaa siijui wala maeneo hua natembea tu nitapopata nachotafuta ndipo naponunua, hivyo maamuzi yangu ya kurudi kubadilisha kitu hicho yaliingia doa maana duka silikumbuki liko wapi wala mtaa upi..Nikaona leo kijana wa mkoani naingizwa mjini live. Nilivuta pumzi ndefu nikafumba macho kisha nikasem “Eeh Mungu nakukabidhi usukani , Mimi nitatembea ila kichwa kiongoze wewe niweze kupata hapa ninapopatafuta” Nikaanza kutembea. Kwa ajabu kabisa nikiwa nazunguka ndani ya maduka nikajikuta nimetokezea palepale kwenye lili duka nikafanikisha kubadilishiwa. Niliwaza sana maana hata nilipotoka pale nilipasahau tena nisingeweza kurudi..Nilimshukuru Mungu kwa hilo na kuona kanipendelea sana juu ya hili maana naona si msafi ila kanijibu ombi langu kwa haraka sana wakati nikihitaji….Nilipokumbuka lile andiko linalosema Mungu huwanyeshea Mvua wema na wabaya Nikatabasamu!.

Kuna vitu vinaweza kua vinakutokea maishani mwako, ukijiangalia na matendo yako yalivyo unaweza kuona kabisa havifai kukutokea. Labda unajijua matendo yako si mema sana ila kila unapoomba au kuhitaji msaada wa Mungu katika jambo Fulani basi Mungu hukupatia majibu/msaada haraka sana. Kwako wewe maisha yanakunyookea maana kila ukiwa na tatizo basi kwa haraka maombi yako hujibiwa..Mara nyingi watu tukiwa tunakumbwa na hali hii ya kujibiwa kwa uharaka maombi yetu wengi hua tunasema kua mungu anatupendelea pia hua tunaona kua kama tumekua na urafiki Fulani hivi na Mungu! Kiuhalisia Mungu hua hatupendelei kabisa…nitatoa mfano

Kama unakumbuka kipindi ulipokua mdogo kuna kipindi ulikua unaona ukaribu/urafiki wewe na mzazi/mlezi wako ulikua unaongezeka sana hata ukifanaya kosa kuna muda hakupigi au anakutetea na akikutuma wala hukatai unaeenda bila kinyongo. Tena muda mwingi unakua uanatamani kukaa nae mpige stori muda wote, kama uliwahi kuchunguza kipindi unapoona mzazi wa wako amekua rafiki yako hua utii wako unakua kwa kiwango cha juu sana hivyo basi kiuhalisia unakua haujawa rafiki tu kwa mzazi bila sababu, sababu pekee inayoleta hiyo hali ni Utii wa hali ya juu unaokua nao kwa wakati huo ndio maana nae anavutiwa nawe anakua hakupigi wala kukusema vibaya na hivyo ndio mzazi/mlezi na mtoto inapasa waishi..pindi ukiacha kutii basi ule urafiki hutoweka na kubakia ile nafasi ya mazazi.

Kwa mantiki hiyo ile hali tunayoona kua Mungu anatupa msaada kila mara tunapohitaji msaada wake Mungu hua hatupendelei ila NDIO JUKUMU LAKE, jukumu la Mungu ni kuhakikisha anakupatia kila unachomuomba na sisi wanadamu ili tuyapate hayo inabidi tukubali kua YEYE NDIO MSAADA NA KIMBILIO LETU bila yeye hatuwezi. Yaani kiufupi ni kua mwanadamu inabidi akubali kua msaada wake ni Mungu na yeye hawezi kitu, hiyo ndio ghalama pekee ya kupata kila tunachohitaji na kupendelewa kama tunavyojinasibu.

Binaadamu aliumbwa na utashi pamoja na akili yenye uwezo wa hali ya juu katika kukabiliana na mazingira anayoishi, akili yake hiyo imemsaidia kutenda na kutatua mengi maishani. Lakini akili na utashi pekee haumtoshi mwanadamu kuyakabili mazingira yake aliyomo ndio maana akilala hawezi jua kama kesho ataamka,hawezi jua mizunguko ya siku nzima ya kesho,hawezi kujipatia pumzi hii anayovuta. Kwakujua hilo ndio maana Mungu alipomuumba mwanadamu hakumuacha pekee yake ajiongoze maisha yake bado alimwambia kua yupo nae na hatamuacha mpaka ukamilifu wa dahari, atamsaidia na kumvusha katika mambo magumu. Ila ili mwanadamu huyoo apokee msaada huo wa Mungu inabidi alipe ghalama ambayo ni very cheap kila mtu anaweza kuimudu! Ghalama pekee ilikua kumtii Mungu na kukubali kua sisi wanadamu hatuwezi bila msaada wa Mungu, lakini kwa jinsi ya ajabu kabisa kuna watu kama mimi Da’Vinci hawamtii Mungu kama inavyotakiwa ila wanajua kua hawewezi kitu bila msaada wa Mungu hivyo humkumbuka na kuomba Mungu awasaidie,naye si kiziwi mpaka asisikie wala hana mkono mfupi..Hutujibu kile tukiombacho.

Mwanadamu huyo mwenye akili yenye utashi mkubwa nafsi yake inatambua kua Mungu ndio kila kitu bila yeye sisi si lolote, kuna muda akili inatamani inatamani kutumia uwezo wa mungu katika kutatua matatizo yake mbalimbali klakini ile roho ya giza ambayo hua inachochea viburi nafsini mwetu hua inaisonga akili na kusahaulisha akili zetu kua ili tufanikiwe tunamuhitaji Mungu zaidi katika vita vyetu….hapa sasa ndio tunapokuja kumuunga mkono rais wetu kwa hatua ya kwanza kabisa (japo kwakuchelewa kuchukua tahadhari ya kufunga mipaka alibugi) ya kukabidhi janga hili la COVD-19 mikononi mwa Mungu linapokuja kua na mantiki.

Kwanza kabisa watanzania tumekubali kabisa kua sisi hatuwezi hata theruthi kupambana na hili gonjwa kwa kuangalia miundombinu au akili zetu, hivyo tukalikabidhi kwa Mungu kua yeye ndio anaweza kutupambania na kulivuka..kwa wale wanaotumia akili zao wataona ni jambo la kipuuzi ila kwa watu wanaoamini katika mambo ya roho wanajua this was a bold and smart move ever. Hata iweje hatuna uwezo wa kuvuka hili jambo na ninaamini wapo watu kibao wanaumwa mtaani ila wanapona bila kujijua. Tunaweza kusema Mungu anatupendelea waTZ kwakua confirmed case sio nyingi na hata hizo ambazo hazijawa confirmed watu wanaugua na kupona bila kujua siri kubwa juu ya hili ni kwamba tulisha surrender kua hatuliwezi janga hili msaada pekee ni kuchukua tahadhari za kujikinga na kumkabidhi maisha yetu ayalinde yeye sisi hatuwezi.

Kuna watu watakuja kukomenti kua waliokufa huko Asia,America na Europe walikua hawaamini katika Mungu? Mbona hakuwalinda? Jamani kifo ni Fate natamani siku moja nielezee kwa kina zaidi kuhusu Fate/Destiny (hatima) na Contentment (ridhiki)..Naposema kifo ni fatee ni kwamba kama muda wako umefika huwezi kwepa kifo hata iweje, usipokufa kwa korona utakufa kwa lolote ilimradi hatma yako itimie ya kufariki, huwezi kuikwepa fate hata uafanyeje. Kama kweli inabidi watanzania tufe hatutakwepa hata kidogo na haijalishi tutakufaje tunaweza tusife kwa korona njaa au tetemeko likatupukutisha. Ila naamini hatutakufa maana yeye aliyetuumba anatuwazia mema, kama unashadadia kua watanzania tutakufa kama kuku wa kideri basi ni wewe na familia yako. Tuendelee kuchukua tahadhari zifuatwe na tumuachie hatma ya uhai wetu aliyetuumba, hatupaswi kuogopa hata kidogo.

Mungu hatupendelei bali anatimiza jukumu lake kama baba na muumba kwa kutulinda na kutupatia yale tuanayoomba, Tuendelee kumkumbuka na mtangulize yeye kwa kila jamboa kila sehemu unayoona utashi wa akili yako umegonga mwamba usikaze shingo lako, muite Mungu wako unayemuamini akuvushe. Kuomba na kuAdmit kua huwezi bila yeye ndio funguo pekee ya mafanikio ya maisha yako.

Tuwe na tumaini japo kidogo tu, Naamini wote mliosoma hapa tutauona mwaka 2021 tukiwa na afya tele..Amina

-Vinci

Mwenyezi Mungu amejawa rehema tele na fadhili zake ni za milele,Eeh mwenyezi Mungu usinilipe sawasawa na upumbavu wangu bali unifundishe yaliyo mema


Sent using IPhone X
 
Back
Top Bottom