Je, KATIBA ni mali ya nani?

Je, KATIBA ni mali ya nani?

IamPrince George

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2014
Posts
412
Reaction score
168
Katiba ni taratibu, muongozo wa namna watu, kikundi cha watu, taasisi ama shirika wamekubaliana kuzifuata ili kuwawezesha kuishi.
Tanzania iko katika mchakato wa kupaata katiba mpya, na mwezi wa nne katiba pendekezwa kwa mujibu wa sheria itapigiwa kura ya NDIYO/HAPANA.

Swali langu ni je, watanzania wangapi wameipata katiba pendekezwa na kuisoma?, na je serikali imeielimisha jamii kuhusu katiba pendekezwa, na je serikali imefanya jitihada gani kuhakikisha wananchi wanapata nakala ya katiba pendekezwa na kuisoma?
Na je, katiba pendekezwa imekidhi mahitaji ya watanzania?

Nini mtizamo wako juu ya swala hili kwa kuzingatia kuwa katiba ni mali ya wananchi wote na si kikundi cha watu wachache?
 
kukidh matakwa ya watanzania ni kukubaliana rasim ya warioba nje ya hapo ni matakwa ya mafisadi wa ccm
 
Tujikite kwenye katiba ya nchi, ni makubaliano ya wananchi na watawala namna watakavyotawaliwa. Kwa bahati mbaya tz watawala wamehodhi yote, tunaenda kupigia kura mapendekezo ya watawala jinsi watakavyotutawala!
 
naomba kuweka hili swala wazi, Watanzania tunahitaji kuwa na viongozi na si watawala,
Kiongozi anaongoza kwa kuvaa viatu vya wale anao waongoza, kwa kuyafanyia kazi na kutatua matatizo na kushughulikia changamoto zao.

Watawala hufanya kwa kuangalia masilahi yao binafsi, na hata kupindua na kuiweka kando sheria, taratibu, kanuni, jamii ya watu hawa tuiepuke
 
ukomo wa chama tawala haupo wazi ndio maana wana-ignore itikadi za watu wa nje ya chama
 
je katiba pendekezwa tumeisoma na kujua yapi mazuri na mabaya yaliyomo?
 
Back
Top Bottom