Je itungwe sheria itakayowalazimisha viongozi kusomesha watoto wao kwenye shule za serikali ?

Jef Kirhiku

Member
Dec 10, 2016
39
76
Nimejaribu kufuatilia kupata majina ya watoto wa Viongozi na watu maarufu wanaosoma shule za bure mpaka sasa sijafanikiwa .
Kama unajua kiongozi anayesomesha mtoto wake shule za serikali kuanzia msingi mpaka secondary(Elimu bure) hebu nitajie .
Kwa kuwa wanaotunga sera za elimu na kusimamia elimu hasa katika shule za serikali watoto wao hawasomi huko je hii haiwezi kuwa sababu ya wao kutojali ?
Je umefika wakati tuweke marufuku kwa kiongozi kusomesha mtoto wake katika shule binafsi ili uharibifu wanaoufanya katika elimu uwaathiri na watoto wao ?
 
Si mnataka elimu bure halafu kiongozi anakwambia elimu imepanda ubora lakini yeye mwenyewe analipa zaidi ya m8,hakuna kubadilisha sheria tupo kwenye mfumo huria ambapo maslahi binafsi yana nafasi kubwa hivyo akiri kumkichwa.
 
Acha wivu, nawewe peleka wakwako nje nani kakuzuia?;mijitu mingine kichwani hamnazo, linapost uzi wa kipumbavu na kilofa.
Hapo mwanzo nakusaport ila hapo ulpomtukana niko kinyume na wewe, mwenzako katoa mtazamo wake na kuuliza hapa inshu ilikuwa n kukubali au kupinga kwa hoja sasa matusi ya nini mkuu?

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Acha wivu, nawewe peleka wakwako nje nani kakuzuia?;mijitu mingine kichwani hamnazo, linapost uzi wa kipumbavu na kilofa.
Jifunze kujadili,kupinga hata kuwa na mtizamo tofauti kwa kujenga hoja bila kutukana wala kumkashifu mtoa hoja .
Watu wenye uwezo mzuri wa kufikiri hufanya hivyo .
 
Hiyo ndio njia pekee, ila wanaotutungia sheria hii itawaumiza hivyo hawatokubali. Unategemea mtu ambaye analipwa mshahara mkubwa lakini huduma nyingi anapata bure ama kwa gharama za serekali. Hao viongozi wakiwa madarakani utasikia watu wajiajiri lakinj ikitokea wao inabidi wapunguzwe kazi wanakesha kwa waganga wa kienyeji. Lakini tusichoke kupigia kelele hilo hata kama hawatekelezi lakini dhamira zknawasuta. Naomba kuuliza watoto wa Ndalichako wanasoma shule za kata?
 
Elimu bora ni gharama...uchumi bora wa nchi elimu bora ya nchi..ivi Dr Mwinyi alisoma Tz vp Dr. Malecela ?Dr...Nina uhakika wazazi WAP wali invest..
 
Unapopika chakula ukakisifia kuwa ni kitamu, wewe mwenyewe utakuwa wa kwanza kujipakulia. Unapokisifia kuwa ni kitamu, kizuri na kina lishe bora halafu unakiacha na kununua kingine kwa ajili yako ni makosa.

Hiyo sheria imechelewa sana. Watoto wa viongozi wetu wengi wa awamu ya kwanza, including Baba wa Taifa walisoma shule za umma. Nakumbuka Nyerere alipiga marufuku watoto wake kupata upendeleo huko walikokuwa wanasoma!

Tatizo ni kuwa wanaotunga sheria na kuzipitisha ndio watakaoathirika sana hivyo haitawezekana sheria hiyo kutungwa.
 
Back
Top Bottom