Je itakuwa sahihi?, ushauri tafadharini

Je itakuwa sahihi?, ushauri tafadharini

truegooner

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2014
Posts
779
Reaction score
339
Habari zenu, naombeni USHAURI wa kumpa rafiki yangu. Ninae rafiki yangu ambaye kapendana sana yaani saaaana na msichana mmoja. Ishu iliyopo ni kwamba huyo msichana aliyependana naye ana dada yake.

Huyu dada yake na msichana amezaa mtoto wa nje na baba wa huyo rafiki yangu. Udada au undugu walinao hawa madada wawili ni kwamba baba zao na hawa wasichana wanashea baba.

Kwa maneno mengine, mmoja wa hawa wasichana anamuita baba wa dadake baba mkubwa. Rafiki yangu na huyo msichana wanaependana nae wanalijua hilo, na msichana yuko tayari kulipuuza, ila ni rafiki yangu aliye njia panda.

Je itakuwa sahihi kwa ujumla wao kuwa pamoja kama wapenzi na baadae labda kuja kuishi pamoja? TAFADHARINI, ushauri.
 
mbona kuna umbali hapo damu,kwanza kitendo walichokifanya baba na dada ni dhambi,na wanachotaka kufanya hao wadogo ni jambo la heri,kwaio dhambi isizuie wema kutendeka.
 
Watu8 Rogie na tayta tunawahitaji hapa mtuletee upembuzi yakinifu kabla hatujachangia!!

Siiamini tena MMU kutoa ushauri hadi nithibitishiwe habari ni mpya!

Nasubiri wadau
 
Last edited by a moderator:
Hakuna shida hapo...kibongo bongo Karibu kila mtu ni ndugu...ukiendekeza utakosa mke
 
Kama ni Waraabu hakuna shida kwa mila za Kiafrika kuna walakini.
 
Hawa watu wangu wa record management ndio watakuja kusema ukweli Watu8 na Tyta
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom