Huwa najiuliza sana Mungu aliumba dunia tu? sayari zingine je? na je kama aliumba ulimwengu na dunia ikiwamo ndani yake, alitumia muda gani? tunaambiwa kwamba kuumba/kutengeneza dunia alitumia siku saba, vipi Jupita alitumia siku ngapi?
Neptune je? kwa maana binadamu hata huko wapo, japo haizungumziwi, na wapo wanaoenda huko na kurudi, na wapo wanaoishi huko, najua hapa kuna watu watapinga lakini huo ndio ukweli, binadamu huko wapo na mchanganyiko na viumbe wengine kama ilivyo hapa Duniani, kwanini dini hailizungumzii hili? je haikujua kwamba Binadamu yupo sayari zote?
Ama walifanya kusudi tu kukausha. na hili la Taifa linaloitwa Israel pia ni utata tu, sidhani kama wana u special huo mbele za Mungu maana kuna mi vitu huko kati ina akili na teknolojia kubwa kuliko hao jamaa..naamini humu wapo pia waotoka nje ya Sayari Dunia na kurudi, waje watupe shuhuda japo kidogo, nna uhakika humu wapo kwa 100% labda wanaamua kukausha tu kwa sababu zao binafsi, lakini suala la dini kuzungumzia, Mungu, Dunia na waisrael pekeyao kuna shida mahali.