Je, Israel au Palestina?

Je, Israel au Palestina?

Noel Shao

Member
Joined
Jan 19, 2017
Posts
89
Reaction score
185
[HASHTAG]#Onyo[/HASHTAG] :
Kama haya mambo huna uelewa nayo, nakuhisi usitumie lugha ya kuudhi!

Msimamo wa Marekani ni mmoja, na tayari wamesha tangaza kuhamisha ubalozi wao ulipo katika mji Mkuu wa Israel, Tel Aviv hadi Jerusalem, ambapo pia makao makuu ya Israel yatahama kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.

Ikumbukwe amani ya Mashariki ya kati ipo rehani miaka mingi kutokana na ugomvi kati ya Israel na Palestina.

Mgogoro huo umesha sababisha hadi Mataifa makubwa dunia kuwa na blocks, wengine wakiwa upande wa Israel na wengine upande wa Palestina.

Hatua hii ya Marekani inasababisha Baraza la usalama la Umoja wa maifa " United nation security Council" kuitisha kikao Cha dharura kujadili na kutathimini tamko hilo la Marekani. Pia Umoja wa Jumuiya ya nchi za kiislamu duniani "OIC" baadaye mwezi huu itakutana huko Uturuki kujadili tamko hilo la Marekani.

Sasa katika hatua hii, nasi binadamu tulio na utashi wa fikra, tumejikuta tuna nasa katika mgogoro huo wa Mashariki ya kati.

Wengi wakiunga mkono Israel, kwa mema au mabaya kwa sababu ya " imani" kadhalika kwa upande wa Palestina.

Pia Kuna wengine wapo upande wa Israel ila haawaungi mkono wanayo fanyiwa Palestina. (Wengi hawa ni wanaharakati)

Sasa:-
1. Tunaombeni mtusaidie sisi watu wa imani!

Maandiko yanasema atabarikiwa ataye Ibariki Israel na atalaaniwa yeye atakaye ilaani. Hilo ndilo agano la Mungu.

Pia kitabu cha Zekari 12:9! Kinasema, "Hata itakuwa hivyo nitafuta, kuangamiza Mataifa yote watakao kuja kupiga na Yerusalemu"

Kwa maneno hayo, tuna sababu ya kuungana na Israel, ili tusipingane na ahadi ya Mungu,? tuna sababu ya kuunga mkono Israel ili tukwepe laana? Kuna sababu ya kuwa upande wa Israel ili kuwa salama? (Kama mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla?)

2. Pia watu wa haki za binadamu na wanaharakati wasaidiwe pia, wawe tayari kuona wengine wanaangamia kwa sababu ya taifa la Israel ?

Haya mambo yanahitaji tafakuri ya kina kiimani, kitheologia, kihistoria na kibinadamu.



Ndimi , Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]
 
Huo ni mtazamo wa kikristo nadhan, maana hujatuambia kitabu kitakatifu cha kiislam kinasemaje kuhusu mji huo
 
Back
Top Bottom