Je, inaruhusiwa mtoto mchanga kupewa maziwa ya ng'ombe?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Habari, kuna mtoto amezaliwa mtaani kwetu, kwa bahati mbaya mama wa mtoto huyo haruhusiwi kumnyonyesha mwanaye kutokana na sababu za kiafya.

Je, anaruhusiwa kupewa maziwa ya ng'ombe au uji mwepesi kama maziwa yaliyoandikwa na Daktari hayajapatikana kulingana na sababu zilizo nje ya uwezo wa familia?

Maana maziwa hayo ya ng'ombe yapo karibu na ndiyo uwezo wa familia.
 
Maziwa ya ng’ombe kwa mtoto chini ya Miaka miwili sio mazuri sana kiafya hasa hawa ng’ombe wa kisasa kutokana na utumiaji wa madawa kwa wingi ili kuongeza maziwa

Mtengenezeeni maziwa ya Soya kwa kuwa ni salama na gharama yake ni ndogo sana (affordable)
 
Maziwa ya ng'ombe siyo mazuri kwa mtoto

√Kwanza, yana protein nyingi,

√Pili, yanasababisha constipation (choo kigumu)

√Tatu, yanakosa vitu kama Omega 3 ambavyo ni vitu muhimu kwa ukuaji wa mtoto, anaweza kuwa mbumbumbu

Tumia maziwa ya unga kwani yana kila kitu kwa kiasi kinachofaa kama Omega 3 n.k
 
duuh nyie wachangiaji hapo juu Mungu anawaona.!

tafuta mama mwingine atakae-mnyonyesha mtoto, hii kitu nilishawahi kuona kwa mama mdogo wangu, alimnyonyesho mtoto wa mdogo wake.
 
Je umejiuliza kwamba watoto wanaofiwa na mama zao pindi wazaliwapo hupewa maziwa yapi?
 
Back
Top Bottom