Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
Sujui nikoje, huwa nikiona kitu ni cha bei rahisi sana huanza kukiogopa na kukikimbia kabisa.
Jana nikienda kumtembelea ndugu yangu huko Kitunda Mwanagati kwa Mfipa.
Yeye ni mkubwa sana kwangu. Nilipofika nkapokelewa vyema nikachinjiwa jogoo.
Utamaduni huu wa kuwakirimu wageni kwa kuwachinjia kuku, sii kwamba umetoweka DSM tu, hata vijijini ukienda kibweke utaishia kula mishikaki ya kilabuni.
Tukapiga story, one two, three, then mwenyeji wangu akakaendea kabox kenye rangi ya njano na maandishi mekundu na weupe, DOUBLE KICK.
Akaanza kuponda urasimu, ukiritimba na ubabe sokoni wa Konyagi na K Vant huku akiniambia nionje hilo chuma lenye stimu za fasta kama umeme.
Si mara yangu kuviona hivyo vichupa, vijana wengi huvinywa mitaani na barabarani. Nikasema isiwe taabu, let me have a test.
Kilipofunguliwa nikakutana na harufu kali sana hadi nikapiga chafya kama zote.
Nilipokiweka mdomoni kina ladha mbaya balaa.
Ikabidi niwe muungwana, nikamwambia bro, hii shughuli napenda kunywa na 🍷 wine.
Nkatoka nje, nkaleta box la Overmeer nilikuwa nalo kwenye Kaka yake Bajaj.
Harufu ya wine ni nzito na iko calm, hivyo ikameza harufu yote ya double kick na ladha, ndipo nkaweza kunywa.
Sasa nikiwakumbuka wale jamaa wanakulaga hizo makitu, je huwa wanafuata ladha au mserereko bin mteremko bin Kitonga?
Bure ni gharama