Je, huu si ni Ufisadi/Uhujumu Uchumi?

Itoye

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
531
1,024
Ujumbe huu natamani sana umfikie Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sarah Msafiri na watendaji wake wote wanaotakiwa kurekebisha hili bila kuwasahau mamlaka ya bandari (TPA).

Picha hii ni eneo linafahamika kwa jina la mtaa wa Tungi na ni sehemu ambayo pia bomba la mafuta la TPA linapita, kwa sababu ya mvua ambazo zimenyesha kwa wingi miezi iliyopita hilo dimbwi kubwa likajitengeneza, lakini tofauti na miaka mingine ambapo msimu wa mvua unapoisha nalo hukauka safari hii halijakauka hata baada ya miezi kadhaa sasa kupita tangu mvua zilipokata.

Kama inavyoonekana ktk picha walijitokeza vijana wakajenga daraja la mbao ili watu wapite kwa kuchangia Tsh 200/- kweli lilikuwa jambo jema na kama sehemu ya kutatua dharura iliyojitokeza ya mawasiliano ya barabara kukatika kwa sababu ya dimbwi hilo.

Tatizo linaanza hapa, baada ya mvua kukatika na maji kwenye dimbwi kuanza kupungua hawa vijana wakaona fursa yao ya kupata fedha inaenda kutoweka hivyo wakaamua kuchepusha maji yanayotoka bwawani (bwawa la boko) kuelekea baharini wao wakatengeneza kimtaro kidogo kinachoendelea kuleta maji kwenye hili dimbwi masaa 24 siku 7 za wiki hivyo kupelekea kutokauka kwa hili dimbwi, barabara hii haipitiki kwa magari inabidi kuzunguka huku wao wakiendelea kukusanya Tsh 200/-

Hapa wameendelea kutengeneza tatizo ili wao waendelee kufaidika. Kwa nini tulipe kupita sehemu ambayo hatukutakiwa kulipa, kwa nini tulipe kwa sababu ya hujuma inayofanywa na watu wachache? Cha kushangaza zaidi hili dimbwi liko mbele ya nyumba za watu, je! Wao haliwaudhi? Au huu mradi ni wa nani?

Haya yanafanyika mwenyekiti wa mtaa yupo, mtendaji wa mtaa yupo na viongozi wengine wote, je! ni kweli jambo hili dogo limeshindikana? Hadi kufikia hatua ya kuendelea kuwaachia watu wachache wawahujumu wananchi wengi? Watu wanachezea miundombinu ili kusudi wafaidike na bado hakuna kiongozi anayechukua hatua wakati tumewapa dhamana ya kusimamia maslahi ya walio wengi?

Naomba viongozi wa mtaa huu na wilaya ya kigamboni na mamlaka ya bandari mliangalie hili kwa ukaribu ili kero hii ifike mwisho.

Najua JF ni Platform kubwa na kero yetu itafika tu sehemu husika.

NB:
Picha ya 1: Dimbwi linalozungumziwa

Picha ya 2: mfereji uliochepushwa na ambao unapeleka maji kwenye dimbwi hili.

Picha ya 3: Sehemu ya Bwawa la Boko, ambalo maji yake yanatiririka kuelekea baharini ambayo pia ndio kuna sehemu yamechepushwa ili kulisha dimbwi la maji linalozungumziwa.

IMG_20200719_120416_139.jpg
IMG_20200719_111203.jpg
IMG_20200719_113353.jpg
 
Hujuma, Uzembe wa watendaji ,ubinafsi wa kiwango cha juu. Kwa sasa wako busy kutia nia na michakato mingineyo ya uchaguzi.
 
At first ulikuwa ni ubunifu kweli ila kwa wanachofanya sasa binafsi naona ni ufisadi/hujuma.
Mkuu wao wame redirect maji wapige pesa,Sasa wewe kazibe au badiri njia otherwise they are very clever
 
Back
Top Bottom