kuachana inategemea mliapaje
Hadi mkataba utakapofika mwisho?(serikalini)
hadi talaka 3 ziwatenganishe?
Hadi kifo kiwatenganishe?
Ndio maana, baadhi wanaamua kubebana tu, wanatest kama inawezekana au la.
Ikiwezekana, wanakuja kubariki ndoa badaae.
Lakini pia kuacha kitu chochote huwa tunapima faida na hasara zake. Halikadhalika katika ndoa, kuachana kila mweza anapima faida na hasara. Hasara za kuachana zikiwa kuliko faida mtu anaendelea na ndoa na vice versa.
Kwa hiyo, sidhani kama unaweza weka cut off line kirahisi sababu faida na hasara zenyewe ni subjective.
Mkuu kongosho,..
Hivi haijawahi kutokea watu wakakaa mda mrefu then wakaenda kubariki
ndoa na baada ya hapo ndo wakakosana?....just curious.
Binafsi sidhani kama kuachana ni jambo jema,...niseme tu hivo kwa kifupi
ila ukitaka maelezo yapo kiimani zaidi.
Nadhani ingekuwa vyema kuchukua uamuzi wa kumfahamu mwenzako vyema
kabla hamjaingia kwenye mkataba wa milele,NDOA.
Lakini huku kukutana miezi miwili mna kimbilia kuandaa kadi za michango na
harusi mmmmh,sidhani kama ndoa hizo huwa zinadumu.
Sijao,lakini mchumba wangu tume fahamiana miaka takribani 6 sasa,tunategemea
kufunga ndoa mwakani (hatuishi pamoja,usidhani nipo kwenye category ya wanao enda kubariki ndoa).
Kwa kuwa tumekuwa pamoja mda mrefu,ana nifahamu nikikasirika nakuwa vipi,....ni katika hali gani
naweza fanya something bad na nikiwa kwenye hali hiyo ani face kwa style gani ili nirudi to normal.
Namfaham pia akiwa kwenye mood mbaya kama kukasirishwa anakuwa vipi na anaweza kufanya nini.
Sidhani kama haya yote unaweza kuyajua ndani ya miezi mi3 au 6 then mnakimbilia kuoana.
Ni vigumu sana,kuna vitu toka kwake nime vijua mwaka huu,lakini atleast najua kwamba
kwa vyote ninavyo vijua so far vina vumilika na haviwezi sababisha kuachana.
Nisi iongelee future sana,lakini kufahamiana vyema kunajenga msingi wa future yenu.
Hata mkigombana na ikatokea mwenzako kashindwa kuzihimili hasira zake
na akakuchapa kofi sio kwamba hakupendi,....tena yawezekana akafanya hivyo out of love.
(nimewahi kupigwa kofi,...after that alistuka na kuomba msamaha,na nilikuwa nimefanya kitu kibaya
kweli,.....she did what was right at that moment kuondoa hasira zake).
Lakini kama kupigana ni tabia,kama kule kwetu,........ukikuta hamna ugari unampiga mkeo,..
haja kufulia nguo una mpiga......mmmh,....HIYO NDOA HAIKUWA HIYARI YENU.