Je, hizi ni kauli za Magufuli ''mmoja''?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,090
114,627
1.Nitashilikiana na maalim seif,dr shein na taasisi zingine kuhakikisha tunatatua mgogoro wa zanzibar mapema sana iwezekanavyo JP magufuli 2015 novemba 20 wakati wa uzinzuzi wa bunge.

2.Siwezi kuingilia mgogoro wa zanzibar anayeona anaonewa aende mahakamani JP magufuli 12 february 2016 alipokutana na wazee wa dar.

3.Mimi ni rais wa watanzania wote ni rais wa ccm ni rais wa ukawa ni rais wa wasiokuwa na vyama JP magufuli 20 novemba 2015
Je hizi ni kauli za Magufuli mmoja?
 
Hizo ni kauli za kushtukiza tu kama alivyo yeye mwenyewe,kwa vile ameapa kuulinda muungano huu kwa gharama yoyote na sisi huku zanzibar tumekwisha kuapa kuitetea na kuilinda zanzibar hata kwa tone la damu.
 
Tanzania yangu itakuwa ya viwanda, Tanzania ya Magufuli itakuwa Na elimu bure, sitowaangusha, msema kweli ni mpenzi was Mungu nitawafikisha kileleni, mzidi kuniombea
 
hili njemba magufuli kuingilia kati kutatua mambo ya mgogoro anasema hayamuhusu maana katiba haimruhusu. Lakini kupeleka jeshi nchi za nje kutatua matatizo yao yuko shwaari yaani... hata msanii mwana F anamuomba aingilie kati mambo ya piracy basi mbio kapiga marufuku fake imports na piracy DVDs/CDs. halieliweki yaani
 
Hilo jambo lazima awe na kigugumizi au atoe kauli zanye utata kwa sababu ukilichokonoa sana linagusa hadi uhalali wa uwepo wake madarakani. Naona kama ameshindwa kabisa au anaona hawezi kufanya chochote, ni bora angenyamaza kulikko hizi kauli zake zisizoeleweka.
 
1.Nitashilikiana na maalim seif,dr shein na taasisi zingine kuhakikisha tunatatua mgogoro wa zanzibar mapema sana iwezekanavyo (JPM Novemba 20, 2015, wakati wa uzinzuzi wa bunge). 2. Siwezi kuingilia mgogoro wa zanzibar anayeona anaonewa aende mahakamani (JPM 12 february, 2016 alipokutana na wazee wa dar). 3.Mimi ni rais wa watanzania wote ni rais wa ccm ni rais wa ukawa ni rais wa wasiokuwa na vyama (JPM, 20 Novemba 2015). Je hizi ni kauli za Magufuli mmoja?
.
Jawabu kwa swali lako ni ndiyo. Sababu: Angalia tarehe hizo ulizozitaja. Ni tofauti. Mtakatifu Paulo anaseje kuhusu hilo? "Nilipokuwa mtoto... Nilipokuwa kijana.... (endelea)."

Tofauti ya muda inahalaisha mabadiliko ya mawazo. Hata waandishi wa vitabu huchapisha first edition, second edition, etc kwa sababu hiyo. Kati ya tarehe moja (t1) mpaka tarehe nyingine (t2), ambapo t1 sio sawa na t2, kunaweza kupatikana ushahidi unaomfanya mtu kubadili mawazo, misimamo, imani, n.k.

Hata katiba ya nchi yetu inatambua uhuru wa mawazo. Uhuru huo ni pamoja na kubadili mawazo yaliyokichwani mwa mtu.

Kwa hiyo, swali linalopaswa kutafutiwa jawabu ni hili: Kwa nini JPM amebadili mitazamo yake mara mbili katika kipindi kifupi namna hii? Inawezekana amegundua watu anaotamani kushirikiana nao mezani hawako tayari.... Lakini sijui!

Tafakari njema.
 
Back
Top Bottom