Hashim bin Faustin
Senior Member
- Jan 30, 2017
- 177
- 216
Siyo kweli unapotosha! miundo mbinu hiyo tiyari imeshakuwa mali ya SHIRIKA, alichokosa yeye ni subra ya kuwasubiria TANESCO wafanye Installations ya miundo mbinu yao wenyewe kwa kuwa PESA alikuwa nayo na sasa analazimisha FIDIA kitu ambacho hakiwezekani. Labda kama utaratibu umebadilikame nijuavyo watakaohitaj conection itabidi wakulipe
Hakuna kitu kama hicho! Hiyo imeshskuwa mali ya tanesco yeye hana chake tena.me nijuavyo watakaohitaj conection itabidi wakulipe
Duuuh mkuu gharama yote hiyo na bado vifaa ni mali ya tanesco, chamsingi kuliko kulipa pesa yote hiyo toa mil 5 tu itafute solar tu, naamin hiyo solar system utakyoiweka kwa gharam hiyo itakuwa na uwezo mkubwa sana , ambayo itakusaidia mpaka kipind umeme utakapofika karibu na nyumba yakoNdugu wadau,
Kuna jambo linanitatiza katika mpangilio wa ufanyaji biashara wa hili shirika la umeme TANESCO. Mimi nahitaji kuunganishiwa umeme katika nyumba yangu umeme ambao nitakuwa naulipia kwa kadiri ya matumizi yangu. Lakini ninakerwa na huu utaratibu wa malipo ya vifaa vya kuunganishiwa umeme.
Kwa mfano natakiwa nilipie nguzo kadhaa, waya mita kadhaa, Transformer, na kadhalika jumla ya ngarama naambia ni Tshs Mil. 15, eti kwa ajili ya kuweka miundombinu ya kufikisha umeme ndani ya nyumba yangu. Lakini cha kushangaza baada ya kulipia vifaa hivi kwa Mil 15, vifaa husika vinageuzwa kuwa mali ya TANESCO Bila mimi muhusika kufahamishwa au kuombwa na Shirika hili.
Kupitia miundo mbinu hii niliyo nunua kwa pesa zangu za kudunduliza na mikopo, utaona TANESCO wakianza kuunganishia umeme watu wengine jirani yangu kwa bei nafuu bila kuulizwa au kuombwa na wahusika. Je hii ni haki? Shirika kujinufaisha kupitia mpango huu! Au kwa kuwa ni Shirika la Serikali linafanya litakavyo?
Je kujenga miundombinu ya umeme ni kazi ya mlaji au ni kazi ya msambazaji?
Vigezo vya namna hii ni aina ya ukandamizaji, na vipo tu kwa kuwa hakuna namna mbadala wa kupata huduma hii.Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,
Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.
Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
Tatizo kwanini wasisambaze kwa ela yao kama vifaa vya kwao mbona kampuni za simu hazichangishi minara?Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,
Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.
Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
Kun mteja alilishitaki shirika la umeme(TANESCO) kwa kuwaunganishia wateja wengine ktk nguzo alizokuwa kazilipia yeye,huyo mteja alishinda kesi na TANESCO walimfidia zile gharama..!!Mkuu wala hujatapeliwa, watu wengi wavivu kusoma terms and conditions,
Miundo mbinu yote ya TANESCO ambayo umelipia haijalishi thamani yake bado vitabaki kuwa vyao. Hilo limeainishwa wazi kabisa bila kificho.
Wakati mwingine tunalalamika wakati utaratibu upo wazi kabisa
Niwakati wa Kutoka usingizini na kudai Haki na kulaani utapeli huu.Vigezo vya namna hii ni aina ya ukandamizaji, na vipo tu kwa kuwa hakuna namna mbadala wa kupata huduma hii.
Haiingii akilini mtu uambiwe ugharamie kitu ambacho hakikuhusu.