MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,997
Hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa jana katika sherehe za uzinduzi wa mwaka wa Mahakama (Siku ya Sheria) zilizofanyika katika uwanja wa Mahakama uliopo Mtaa wa Chimala kama vile imetoa dokezo la sababu ya Profesa Palamagamba Kabudi kuteuliwa kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania.
Rais Magufuli alisikika akisema, ‘’Kwenye ofisi ya DPP na AG kuna matatizo, kwani nani hajui kwamba ofisi hizi zinagombana zenyewe kwa zenyewe, Waziri unafahamu kwamba kuna mgogoro kati ya ofisi ya DPP na ofisi ya AG mbali ya kwamba wote wanatoka katika Mkoa mmoja na inawezekana wanatoka katika wilaya moja’’.
‘’Mtanisamehe ndugu zangu, mimi napenda kusema ukweli. Nataka niyaseme haya ili tutafute njia ya kutatua, tukitoka hapa tumepongezana tu hatutakuwa tunalisaidia taifa. Let us tell the truth’’. Alisema.
Aliendelea kusema, ‘’kwa hiyo nitoe wito kwenye ofisi ya DPP kwa sababu mko hapa na mheshimiwa Waziri, tafuteni njia mbadala ya kutatua matatizo yaliyoko hapo. Kama ni masuala ya madaraka, mbona wote ni wateuliwa wa Rais. Kama ni masuala ya kasma, tengenezeni utaratibu kwa sababu instrument inaniruhusu kufanya mabadiliko yoyote kadri ya utendaji wa kazi. Tusipofanya hivi hata kesi mahakamani tutaendelea kushindwa’’.
Alimalizia kwa kusema, ‘’Nimeambiwa katika ofisi ya Mwanasheria mkuu kuna mawakili sita tu ambao wanawaogopa kwa umahili wao na majina yao ninayajua, wengine wakienda wanajua hapa ni mteremko. Hao mawakili sita hawawezi kwenda kwa kila kesi’’.
Maneno ya Rais ni kama sauti iliyoko nyikani ambayo inatoa ujumbe wa yanayokuja baadaye!
Maneno ya Rais yameibua maswali mengi lakini pia yamedhihirisha tatizo kubwa lililopo katika ofisi za DPP na AG ambazo ni nguzo muhimu sana kwa serikali katika mapambano ya uhalifu mkubwa na mdogo.
Je, kitumbua cha Mwanasheria Mkuu wa serikali, George Mcheche Masaju kiko mbioni kitiwa mchanga?
Je, Dkt. Harrison Mwakyembe yuko mbioni kupewa nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali?
Je, Profesa Palamagamba Kabudi atapelekwa kwenye Wizara ya Katiba na Sheria kama Waziri?