Kwa uelewa wangu mdogo, kuna mgongano wa kimasilahi ama kuonyeshana kila mmoja ama kila taasisi na makali / meno yake. Mf;
Anayesimama barabarani kuongoza magari - kisheria ni askari wa barabarani (trafic), sasa mtazamo wangu ni, yakitanua magari ya kijeshi (magereza, jwtz, polisi, usalama), na hizo stk, stl, NW, W, NS, S) kwa mfano huo, trafiki aliye barabarani anayo haki ya kuyasimamisha na kuyaamuru yakae foleni?
Bodaboda imebeba askari wa barabarani ama polisi wa kawaida, dereva wa bodaboda kavaa kofia (helmet), yule askari aliyepakizwa hajavaa, trafiki aliye zamu anayo haki ya kum-fine dereva wa bodaboda?
Daladala limejaza, mlango haufungi, na kati ya waliopo mlangoni ni askari polisi ama magereza, trafiki kalikamata gari hilo, atali-fine ama?
Hapa sijataja vyeo, nimechukulia mtazamo wa jumla.
Mtoa maada, samahani kwa kuingilia post yako, ila nataka sana kuyajua mambo hayo juu.
Ahsante!