Je hii ndiyo mbinu mpya ya kupata Uteuzi katika Serikali ya Awamu hii ya Tano?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
1. Jipendekeze kwa Rais
2. Msifie Rais hadi Kumkufuru Mungu
3. Mtafute Adui wa Rais kisha uwe unamchafua
4. Jitahidi kila Rais akiwa anasemwa uwe unajitokeza Kumtetea
5. Kila mara sifia Jitihada zake mbalimbali hata kama unajua hakuna moja wapo yenye Umuhimu
6. Ongozwa na Kauli kuwa hakujawahi kutokea Rais kama Yeye
7. Ukikutana nae Mnyenyekee na ukiweza Mlambe hata Miguu yake bila aibu

Namuomba sana Naibu Waziri mpya wa Wizara ya Kilimo baada ya Uteuzi wake asibalike kwa ile Misimamo yake Bungeni.
 
kuna point moja niliwahi kuisoma sehemu. inasema kama wewe uliwahi kushika wadhifa mkubwa ktk awamu ya nne, awamu hii hutakiwi kukaa kimya sana. uwe unajitokeza kwenye vyombo vya habari kumsifia au kukemea wale wanaojaribu kumkosoa.

ukikaa kimya yeye anahisi unapanga mipango mizito ya kumuhujumu. matokeo yake anaweza akakufanyia jambo lolote la kukushughulikia ikiwemo kuporwa mashamba, kutengenezewa kesi nk.
 
Mfalme na watu wake. Sifa na hewala kwa mfalme na amri ndio huenda kwa watu wakiamini wako salama. Anayecheza ngoma vizuri au mpiganaji mzuri hukaa karibu na mfalme. Bila sofa vigumu kumkaribia mfalme
 
Kabisa...

Usisahau na kupongeza juhudu za serikali ya awamu ya...

Hata kama project time line yake ilikua miaka kumi, na mwaka wa kumi wa hiyo project ndiyo umefika leo, usiipongeze kabisa serikali ya awamu iliyopitia... sema hizi ni juhudu za serikali ya awamu hii...

Cc: mahondaw
 
1. Jipendekeze kwa Rais
2. Msifie Rais hadi Kumkufuru Mungu
3. Mtafute Adui wa Rais kisha uwe unamchafua
4. Jitahidi kila Rais akiwa anasemwa uwe unajitokeza Kumtetea
5. Kila mara sifia Jitihada zake mbalimbali hata kama unajua hakuna moja wapo yenye Umuhimu
6. Ongozwa na Kauli kuwa hakujawahi kutokea Rais kama Yeye
7. Ukikutana nae Mnyenyekee na ukiweza Mlambe hata Miguu yake bila aibu

Namuomba sana Naibu Waziri mpya wa Wizara ya Kilimo baada ya Uteuzi wake asibalike kwa ile Misimamo yake Bungeni.
Vipi kuhusu Bashe?
 
Back
Top Bottom