Kwa uzoefu wa miaka 10 Sasa kwenye hii huduma,herbal clinic nyingi hazina ufanisi.
Suala la mitishamba linahitaji utafiti wa kutosha ili kubaini ufanisi wa dawa Fulani katika kutibu changamoto Fulani,ni asilimia ndogo Sana ya watu wenye weledi na uwezo huo.
Mitishamba huhitaji uangalifu Sana katika uvunaji wake na mpaka ukaushaji wake ili kuepusha ile ingredients ya asili iliyomo ndani yake kupotea( ambayo Ndiyo dawa),mfano ni lazima kufahamu kuwa ni wakati gani mmea uvunwe majani,magome au mizizi yake.Si kila wakati unaweza kuvuna dawa katika mmea.Mathalani huwezi kuvuna dawa kwenye mizizi wakati wa jua Kali( hii ni kanuni ya kawaida ya fotosinthesis).
Wauzaji wengi wa dawa hawaadai wenyewe kulingana na changamoto ya upatikanaji wa mimea tiba.Wengi huuziwa dawa zilizoandaliwa na wao kuzipaki katika vifungashio vyao hata bila kujiridhisha Kama dawa hizo zina ubora,ilimradi tu amekalilishwa kuwa mti huo unatibu gonjwa Fulani.Kwa hiyo wengi wanauza makapi na Wala siyo dawa.Lakini Kama utapata mtu mtaalam anayeweza kuandaa dawa kwa vigezo na ufanisi,ni kweli mitishamba inasaidie Sana magonjwa mengi na watu wanapona.Shida ni pale mtu Yuko Dar anauza dawa ya unga wakati hata siku akikutana na huo mmea njiani hawezi kuutambua.