Nchi hii sasa inaweza kudumaa kimaendeleo, maana kule kuchelewa sasa kumepita ukomo wake wa kawaida!
Awamu hii hadi sasa hakuna masterplan ktk maendeleo ya nchi! Tunaanza upya na mikakati ya kesho haipo, wote tunaishi Jana na juzi! Ni kufukuzana tu, hakuna mipango ya uboreshwaji wa lolote na hata sisi hatuulizi bado tumekamatwa hizi sinema zao kushtukizwa, wote tunapumbazwa badala ya kuweka vigezo vya kitu gani tunahitaji, wote tumekuwa Nyumbu tunashangilia tu hizi comedy!
Kutokuhoji kwa wanachama na wananchi juu ya kila litendwalo na jamhuri kunaifanya hii serikali ya awamu ya 5 iendelee na mtindo huu mpya na mbaya wa uongozi wa kisinema sinema!
Kwanza si jambo la kawaida kwa kila linalofanywa lazima liwe na waandishi wa kulifanyia coverage! Waziri amefanya ziara ya kushtukiza katika idara Fulani umma asubuhi SAA 1-2 hizo media zote zinajuaje? Nani kazileta? Ni dhahiri jamaa huwa wanawaita kwanza, nini mantiki ya kufanya hivyo? Kampeni ndio zinaanza? Au kujiahakikishia nafasi za uwaziri?
Kuna mawaziri wanatoa maamuzi magumu ambayo yalipaswa kufanyia uchunguzi kwanza kabla ya kukurupuka! Hapa tuweke mifano mitatu!
Uvunjwaji wa nyumba za mabondeni!
Bila ya kufanya tathmini na kujenga hoja waziri na team zao wakànza kubomoa nyumba za watu! Katikati ya zoezi wanaamua kusimama! Je kuna nyumba ya mkubwa imeshindwa kuvunjika ikakomboa nyingine? Waziri katonywa serikali ikishtakiwa watalipa fidia? Au huruma imewaingia sasa? Vipi kuhusu wale walioamua kuvunja wenyewe na kuondoka, wakati huu wa sasa mnawaambiaje, warudi wajenge upya hadi hapo mtakapowahamisha tena? Kama mmeamua kutoa fidia wale waliovunja wenyewe mtawafanyia tathmini ipi, mtatumia picha za nyumba zao kabla hawajabomoa?
Elimu bure na ujenzi wa vibanda elimu
Hapa raisi na waziri wake mmeingia cha kike! Hii hoja ccm mmedandia, hakuna
Mipango rasmi ya kushughulikia elimu hii ya bure! Ada za shule huwa sio big deal, shule zinahitaji pesa kwa ajili ya kujiendesha nje ya taaluma! Shuleni huwa pana mali nyingi, ukianzia thamani, vitabu, kompyuta, mabati, milango etc hivi vinazilazimu shule zilindwe na hakuna mji wenye kutoa askari wa kulinda shule, lazima ziajiri zenyewe walinzi, hapa wazazi watachangia! Wahudumu wa shule huwa wanaajiriwa na shule na sio halmashauri, kuna walimu wa part time hasa huku kwa St. Kata!
Kuhusu vibanda elimu; serikali iache kutania watu, hivi vishule vya kata Mimi naviita vibanda elimu, maana vingi vinakosa sifa! Vinapachikwa popote hata ktk masoko au vituo vya mabasi! Angalia shule kubwa kama mkwawa, mzumbe, Azania, forodhani, Jangwani Tambaza kibasila, utaona maeneo zilipokaa zinaruhusu upatikanaji mzuri wa elimu, ukifika shule, mazingira yanaonesha upo sehemu ya watu wanapochota busara, hekma na ujuzi, sio huko kwenye vibanda elimu! Ujenzi holela na kupachika vibanda kila kona ya kata hasa ktk miji mikubwa nako kunafanya walimu wagawiwe kidogo kidogo na hivyo kusababisha kila kibanda kiwe na upungufu!
Kupambana na watoa tiba za asili
Mh, Ummy na Kigwangala hawakuwa na sababu za kupambana na kina mwaka! Wao ni wasomi na wote nasikia wana masters, nadhani wangeweza kutumia taaluma zao kujua njia bora za kulishughulikia tatizo hili! Kigwangala anataaluma ya afya ya jamii lkn hapa ameshindwa kuona tatizo! Wananchi hawaendi kwa mwaka kwa sababu mwaka muongo au anajitangaza! Tiba za hospital hapa nchini zimeshindwa kunufaisha wananchi! Kwa wale wa kale wanamkumbuka tokelo mganga wa jadi aliyekuwa anatoa majini, kuna wanaenda kwenye maombi, wapo waliokuwa wanaenda kwa masheikh, kuna kina Ndodi, na Africa nzima ilishuhudia misululu ya kwa babu wa samunge wakiwemo waheshimiwa! Wizara ya afya kulikoni kuanza kupambana na watu wa tiba asilia na za kiroho, boresheni hospitali, lkn Ummy gharamia vijana wa vyuo vikuu wafanye utafiti ktk health thinking behaviours upate majibu halisi ya kujua why, watu wanaandamana kwa tiba asilia leo karne ya 21!
Mimi nakataa kuwa Nyumbu, naomba watanzania msio na vyama msiwe Nyumbu na Hawa ccm waache huu unyumbu sio mzuri!
Watu wahoji wakipata nafasi, watu wasije jf kusifia tu kila upuuzi!
Waliposema shule bure, mlipaswa kuuliza ni ktk level ipi? Ada na michango mingine yote? Nani atacover other expenses? Bure kwa kila mtu? What about watanzania ambao wenyewe ni matajiri! Mfano mjukuu wa Bakhresa akisoma shule ya umma naye ni bure? Mtoto wa Magufuli au kikwete kwanini wasilipie? Kama tunatumia kodi ya wananchi kuwalipia hata watoto wa matajiri then hakuna maana kukusanya kwa wote na kuwalipia wote, lazima huduma za lazima za bure ziende kwa wale wasiojiweza pekee!
Cha msingi, ni kuwa tuhoji, tuulize, tuchangie na kuboresha Yale yaliyomema na tukemee Yale ambayo hayana tija!