Je hamasa hii itatafsiri into kura? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je hamasa hii itatafsiri into kura?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mlalahoi, Sep 19, 2010.

 1. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli kuna mwamko na hamasa kubwa baada ya ujio wa Dr Slaa.Kwa sie tulio mbali na huko nyumbani kipimo kidogo ni comments katika tovuti za magazeti na nyinginezo.Binafsi nimekuwa nikifuatilia comments katika tovuti ya Mwananchi,ambapo yayumkinika kuhitimisha kuwa zaidi ya asilimia 90 ni watu waliochoshwa na usanii wa Kikwete na CCM yake,huku wengine wakimwona Dkt Slaa kama ufumbuzi wa matatizo ya Tanzania.

  Sina hakika kuhusu hali ilivyo mitaani,vijiweni,maofisini,nk.Iwapo huko nako ni kama ilivyo mtandaoni basi yaliyotokea kw a KANU yanaweza kuikumba CCM mwaka huu.

  Kama kuna mwana-JF anayeweza kutupa independent,objective assessment ya mahala alipo basi tunaweza ku-project ushindi matokeo kabla ya kura.Hii ni muhimu kwani huwatia uoga wezi wa kura.Na inaweza kuwa ndio sababu ya Redet kufyata mkia huku Synovate wakikwepa kumtaja nani anaongoza kura za maoni hadi sasa.
   
 2. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Heache is: Je wajitokezao kwenye umati wamejiandikisha?? Hilo ndiyo tumaini kubwa la CCM kuwa wale ambao wamejitokeza basi wasiwe wamejiandikisha!!
   
 3. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mlalahoi,
  Hongera kwa wewe na wenzako mlio ughaibumi lakini hamuachi kufatilia habari za nyumbani.
  Ukweli ni kwamba wale wote wenye access ya mtandao majority ni wale waelewa wanaojua atlest dunia inaendaje. Hawa wote wamechoshwa na CCM na ndio hao ambao 80-90% will vote for Slaa. Tatizo kubwa ambalo CCM wana advantage sana ni majority ya kule vijijini, japo yapo majimbo ya vijijini ambayo CCM watapoteza, lakini sehemu nyingi watu bado wanawaona upinzani ni maadui wa nchi, watu wameridhika na umasikini na wataichagua CCM kwa sababu ya kupewa kanga na elfu tano tano. Vijiweni story zipo kwa chinichini, watu wanaipenda CHADEMA hata sehemu za kazi hapa mjini lakini wengi hawapendi kujionyesha kama ilivyo kwa supporters wa CCM na hii ndio disadvatage iliyo kwa CHADEMA, wengi wanaogopa kujitokeza japo ni kweli watawapigia kura. Naipa CCM uwezo mkubwa wa kushinda Urais na kuwa na majority bungeni. Ila CHADEMA watakuwa na idadi ya viti vingi kuliko ilivyokuwa 2005.Mwaka 2005 CCM hawakuwa na hofu na nguvu ya upinzani kanda ya ziwa lakini mwaka huu CHADEMA ni tishio kwa CCM Dar,Kaskazini,Mbeya,Kanda ya Ziwa. Maeneneo ya kusini na Tanzania kati bado CCM wana nguvu na hili litawapa advantage. Uwezekano wa kikwete kuendelea ni mkubwa japo wabunge wa CHADEMA wataongezeka, nalazimika kuamini hivi japo binafsi najitahidi kupiga kampeni na kumsaidia mbunge wa kinondoni atoke CHADEMA,kwenye ubunge kwa Dar mabadiliko yatakuwa ni makubwa sana japo kwenye kura ya urais, i am worried na majority ya wale wanaokaa vijijini ambo CCM inafanya ujinga wao kuwa ndo mtaji kwao.
  NB: Huu ni mtazamo wangu binafsi, ni vile ninavyoona mimi.
   
 4. M

  Masauni JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani CCM inaweza kupata kura nyingi vijijini. Ebu fikiria Lowasa, mramba ambao wametuhumiwa kufanya ufisadi na kila kitu kiko wazi wamepita kugombea ubunge kwa kishindo,wananchi wanatishwa kwamba wapinzani wataleta vita, hii hali si ya vijijini tu hata mjini uelewa wa wananchi bado mdogo kuhusu vyama vya siasa. Nakumbuka siku moja mwandishi wa habari wa star TV alikuwa anamuhoji lipumba kwamba nyinyi mtawezaje kuongoza nchi wakati hata mmeshindwa kujenga barabara ya lami ya kilometer 10!! Sasa fikilia mwandishi wa habari anashindwa kutofautisha serikali na chama cha siasa what about those from villages
   
 5. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwaka huu, kuna muujiza utatokea!! Mi nahisi kuna anguko kubwa kwa CCM. Ni jana tu nilikuwa nimekaa mahala na mtu mkubwa serikalini anayefaidika kwa kiwango kikubwa na system ya sasa, halafu tukaongelea uchaguzi. Akashangazwa na msimamo wangu wa kuunga mkono mabadiliko na tukaanza ubishi wa nani zaidi. Mke wake anammunga mkono Dr. Slaa na atampigia kura. Mimi mtoto wangu anasoma nje ya tanzania ameniomba nimtumie nauli aje kupiga kura kwa Dk. Slaa tu, nilikwenda kwenye gereji fulani hapa Dar ambako ni kijiwe kikubwa wote wanasema huu ni mwaka wa mabadiliko.
  kwa kweli katika siku za karibuni sijakaa mahala halafu nikakuta Kikwete ndilo chaguo la watu!! hata nilipokwenda kwenye mashindano ya miss tanzania na mrembo ktkt kujibu swali akamtaja kikwete alizomewa sana!
  Sijui huko vijijini, lakini kwa kauri ile ya kikwete ya kutokuhitaji kura za wafanyakazi na kusahau kuwa wana influence kubwa kwa wananchi, mambo yatakuwa magumu sana kwa chama cha kijani mwaka huu!!!
   
Loading...