Je, hakuna hujuma ya makampuni mengine ya cementi dhidi ya Dangote? Waziri wa Uwekezaji toa neno

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Tumeshuhudia mitandaoni ikisambaa clip kuhusu figisu alizokumbana nazo Dangote katika kiwanda Cha cement Mtwara.

Tuhuma nyingi zinaelekezwa kwa watumishi wa Umma ambao wanamaslahi binafsi kuliko maslahi ya Taifa.

Kuondoka kwa Dangote kusipuuzwe maana jina lake linaclick masikioni mwa matajiri wa Dunia. Jina lake linaitangaza Tanzania vibaya nje

Siamini Kama Dangote aliingia TZ kwa dili, naamini aliingiza Kama serious investor na anataman kuona matunda ya uwekezaji wake.

Toka awali serikali haijawahi kutoka adharani kuanika mapungufu yake, Wala mapungufu ya Dangote..imebaki minongono.

Waziri mpya wa uwekezaji unalo jukumu la kuuambia umma Nini kinakwamisha Dangote kuendelea na uwekezaji nchini? Hawa wazalishaji wengine wanaouza cement bei ghali wanawezaje kuendelea kuwepo sokoni huku Dangote akishindwa? Je hatuoni kama ni muda wa kuruhusu ushindani? Dangote alishusha cement Hadi 11000 leo imefika 17000 Nani yupo nyuma ya huu mchezo mchafu?
 
Back
Top Bottom