Mdukuzi ni mtu anayechukua data zako bila wewe kuridhia, lakini kwa Facebook; ulivyo jiunga tu ukawapa ridhaa zote bila hata kusoma Terms of use zao; ukiipa location access app yao jua umewapa ruhusa kukutrack, uki upload picha yako ushawapa ruhusa kuiweka kwenye facial recognition data base zao, ukikubali app yao ya Messenger kuacess contact zako ndio basi tena hapo n.k. Kwahiyo Facebook sio wadukuzi sababu ya wewe kuwapa ridhaa yako. Kumbuka "when something is free, know that you are the product."
Facebook ni biashara ambayo wewe unaipa personal information zako (itayowauzia watu wengine) in return wanakupa service hiyo ya Social networking (upate mademu, uuze bidhaa zako, upost kinacho kujia akilini na upate likes n.k.)