Je, CHADEMA Inaimeza CUF, kwanini CUF hajapewa Umeya?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kuna mjadala mkubwa umeendeshwa jana wadau wengi wakihoji kwa nini CUF haikuachiwa umeya wa jiji wakati yenyewe ndiyo ina madiwani wengi? Wengine wamefika mbali na kutamka kuwa CUF inamezwa na CHADEMA. Kama mtu nayefuatilia kwa ukaribu masuala ya siasa za nchi, za vyama n.k. ukiachilia mbali kuwa kwangu karibu na viongozi wa UKAWA na UKAWA yenyewe, niliona nisaidie kutoa ufafanuzi ufuatao;

Kwanza, chama chenye madiwani wengi katika jiji la DSM ni CHADEMA, huwenda madiwani wa chama hicho ni wengi karibia mara mbili ya wale wa CUF.

Pili, utaratibu wa kutoa meya wa manispaa au jiji ni mchakato wa maridhiano baina ya vyama vya UKAWA. Hatujasikia popote viongozi wa chama chochote cha UKAWA wakilalamika kuwa hawakutendewa haki kwenye michakato hiyo, kwa hiyo nadhani aliyegombea alipitishwa na pande zote.

Tatu, katika jiji CUF imeachiwa itoe mgombea wa Unaibu Meya wa JIJI atakayemsaidia Meya. CUF imeshamteua Mhe. Mussa Swedi Kafana, diwani wa kata ya Kiwalani iliyoko jimbo la Segerea.

Nne, utaratibu wa kumchagua Naibu Meya wa Jiji hufanyika mara baada ya uchaguzi wa Meya wa Jiji. Naibu Meya hapigiwi kura na kusanyiko la madiwani wote wa jiji bali yeye huchaguliwa kwenye kikao rasmi cha Baraza la Halmashauri ya Jiji la DAR ambalo huwa na wajumbe kama 25 hivi, wajumbe hao wanatokana na uwakilishi wa madiwani wachache kutoka kila Manispaa zinazounda jiji, uchaguzi huu wa Naibu Meya wa Jiji bado haujafanyika.

Tano, watu wengi hupenda kuonesha namna gani ambavyo hakuna USAWA ndani ya UKAWA na namna gani CHADEMA imevipiku vyama vingine na wengi huishauri CUF na NCCR visikubali na ikiwezekana vijitoe, Ukweli ni kuwa ndani ya UKAWA kuna changamoto zake na kadri muda utakavyokuwa unasonga zitakuwa zinajitokeza n.k. Jambo la msingi ni viongozi wa UKAWA kuendelea kuzishughulikia ili zisijirudie.

Sita, mafanikio ya vyama vya upinzani vya Tanzania leo hii yanatokana na UKAWA na kama kuna chama kimoja kitajitia "wazimu" kijitoe UKAWA kitajuta. Siasa zimebadilika sana na bila muungano "mnapigwa tu". Changamoto zilizomo ndani ya UKAWA ni chache sana kulinganisha na faida za moja kwa moja na zisizoonekana ambazo vyama vilivyomo na hata wananchi wanavyonufaika kidemokrasia.

Saba, hata siku moja, Vyama vinavyoongoza dola haviwezi kufurahia muungano wa vyama vya upinzani, kokote kule! Wapinzani wanapoungana ni "kitisho" kikuu cha anguko la vyama dola. Ndiyo maana siyo ajabu kukuta vijana wanashinda mitandaoni wakieleza namna gani UKAWA haipaswi kuendelea. Kwa tunaoamini kwenye demokrasia ya kweli tunaona ni heri UKAWA yenye changamoto kuliko utengano wa vyama utakaoirahisishia CCM kazi ya kutawala.

PICHA; Mhe. Mussa Swedi Kafana, mgombea wa Unaibu Meya wa Jiji kupitia CUF/UKAWA (Uchaguzi wake bado haujafanyika).
 

Attachments

  • IMG-20160323-WA0023.jpg
    IMG-20160323-WA0023.jpg
    26.2 KB · Views: 41
Mara hii watakubali tuu. Walizowea kugawana hii nchi kama ukoo sasa UKAWA inakwenda kuwaonyesha Tanzania ni ya wote na siyo ya familia fulani. Yaani huwa najiuliza unaposikia familia ile ile tangu Uhuru ndio wanao pewa mamlaka ya kuongoza hili Taifa na jiuliza hivi hakuna wengine wenye akili au utashi wa uongozi zaidi yao? Yaani Utasikia Malecela, Kawawa, Mwinyi, .........Msekwa, .Makamba etc
 
Mara hii watakubali tuu. Walizowea kugawana hii nchi kama ukoo sasa UKAWA inakwenda kuwaonyesha Tanzania ni ya wote na siyo ya familia fulani. Yaani huwa najiuliza unaposikia familia ile ile tangu Uhuru ndio wanao pewa mamlaka ya kuongoza hili Taifa na jiuliza hivi hakuna wengine wenye akili au utashi wa uongozi zaidi yao? Yaani Utasikia Malecela, Kawawa, Mwinyi, .........Msekwa, .Makamba etc
Asante sana
 
DUA LA KUKU.........MMEISHAPATA UONGOZI WA NCHI KWA NIA YA HARAMU TULIENI . WAACHENI UKAWA WANA MAKUBALIANO KWA KILA HATUA.
 
CUF iko vizuri mbona, mleta hoja anaishi wapi huyu? au tuanze kumwuliza maswali ya Gwajima.......
 
Chadema imeua NCCR na sasa CUF, kupitia mwavuli wa ulaghai UKAWA, wahusika wapo kimya wanapiga matarumbeta kuusifu UKAWA, while chadema ikibenefit kilaghai, vyama vingine visipokua makini vitaishiia juu ya mawe kama screpa, na CCM tutapata nafasi ya kuimaliza Chadema vizuri kikibakia chenyewe...
 
Back
Top Bottom