Leo nimefikiria swali moja; Je, mimi ni mwili au ni roho?
Nimefikiria kinachotokea mpaka mtoto anazaliwa nimeshindwa kupata jibu.
Hebu fikiria kama nilivyofikiri mimi. Utagundua mwili ni kama gari umepewa uendeshe ila kuna baadhi ya vitu huwezi kuvifanya na vinatokea vyenyewe.
Mimi najiuliza tunapozaa watoto inakuwaje waitwe wa kwetu wakati hatujashiriki kuwatengeneza ila miili yetu yenyewe ndo imetengeneza?
Concept yangu ni hii, ikiwezekana wanasayansi wakaweza kutengeneza mwili sawa na wa binadam na wakawa na uwezo wa kuhamisha roho kutoka mwili mmoja kwenda mwingne basi tutakuwa tumekikwepa kifo.
Binadamu, ni mkusanyiko wa vitu vitatu.
i. e BINADAMU = MWILI + NAFSI + ROHO.
MUNGU alipo kuwa akiumba mwanadamu, kutoka mavumbini hakukumilika, hadi alipo mpulizia pumzi hai.
Roho ikitoka, na ikabaki mwili peke yake inakuwa si binadamu tena, jina litabadilika na kuitwa marehemu,maiti n. K
Roho ikibaki peke yake, unakuwa katik dimension nyingine kabisa na unakuwa hakuna tofauti ni viumbe wengine, na endapo utakuwa accessable duniani, utaitwa Mzimu n.k
Nafsi ikitoka, ikitolewa kwa ujuzi wa nguvu flani, ikashikwa na kufungiwa sehemu, kwa matumizi yao flani, hapo utakuwa MSUKULE, na ili kuulinda mali yao ambayo ni wew, usije ukatafutwa ndipo hapo utangeneza picha ya kifo, uonekane uliwahi kufa, na kukuweka katika dimension nyingine ili watu wa kawaida wasikuone.
MUNGU ameweka huwezo katika binadamu, kuongezeka na kupiga kopi zao, ili uzao uendelee, ametoa mandatory hiyo automatically. Mbinu na huweza wa kimungu, japo wapo wanaojaribu kuelezea kisayansi na kibaolojia, lakini "Energy can neither be created nor destroyed... " Life ni energy na hizi MUNGU kaziweka ndani yetu. Ukiuza mamlaka yako, wapo wataoweza access energy zako na kuamua kukupiga pin usizae, au uzae wachukue.
" watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"
"kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa..."