Tetesi: Je, bei ya petroli nchini kuongezeka?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,121
SERIKALI, KAMATI YA BAJETI KUJADILI ONGEZEKO BEI YA PETROLI

petrol-300x197.jpg

Na MAREGESI PAUL-DODOMA

SERIKALI imekubali kukutana na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili kuangalia jinsi ya kuongeza Sh 50 katika bei ya petroli na dizeli ili zipatikane fedha za kutekeleza miradi ya maji nchini.

Makubaliano hayo yalifikiwa bungeni juzi, wakati wabunge walipokuwa wakihitimisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, iliyowasilishwa mwanzoni mwa wiki na Waziri wa Wizara hiyo, Gerson Lwenge.

Katika maelezo yake bungeni, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji, alisema Serikali ililazimika kufikia uamuzi huo baada ya wabunge kuonyesha umuhimu wa kuongezwa kwa tozo hiyo katika mafuta, ili kukabiliana na uhaba wa maji nchini.

“Wabunge, maji ni muhimu na ni siasa, kama alivyosema Selasini wakati akichangia hapa.

“Kuhusu pendekezo la kuongeza tozo la shilingi 50 kwa kila lita ya mafuta, tutakaa sisi, Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na Kamati ya Bunge ya Bajeti, ili tuangalie njia sahihi ya kupata fedha za kutatua kero hiyo,” alisema Dk. Kijaji.

Awali, wakati mjadala huo ukihitimishwa, Mbunge wa Hanang, Dk. Mary Nagu (CCM), aliitaka Serikali ieleze jinsi itakavyopata fedha za kukabiliana na uhaba wa maji, huku akiwataka wabunge wenzake wamuunge mkono katika hoja hiyo.

Naye Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, aliunga mkono hoja hiyo kwa kuwa hakukuwa na sababu za kupunguza fedha za maendeleo za bajeti hiyo kutoka zaidi ya Sh bilioni 900 zilizopitishwa na Bunge katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi Sh bilioni zaidi ya 600 za mwaka huu wa bajeti.

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paleso (Chadema), aliunga mkono hoja hiyo na kusema hakuna njia mbadala ya kupata fedha za kutatua kero ya maji nchini kama tozo ya Sh 50 haitaongezwa katika mafuta hayo.

Naye Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), alisema lazima Serikali ikubali kuongeza fedha hizo ili kuwaondolea kero ya maji wanawake ambao ndio waathirika wakubwa.

Wabunge wengine walioonyesha kutoridhishwa na uhaba wa maji nchini kabla Bunge halijapitisha bajeti ya wizara hiyo, ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF) na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (CCM).

SOURCE: Mtanzania
 
Wangeongeza hata shilingi 100 ili kupata fedha nyingi zaidi kwa ajili ya kutatua kwa haraka kero za maji kwa wananchi.
 
Tuna Bahati mbaya Sana kuwa Na wanasiasa wajinga namna hii, yes.. I mean it...

Hivi kwa akili ya kawaida kwanini serikali haipanui wigo wa kodi?
Wanachi mil 50, wanaolipa kodi hawafiki 10%, bado unawapa elimu bure Na bla bla kibao...

Kwanini tusiboreshe Kilimo tukatoa kodi huko, vile vile kuruhusu export ya mazao?

Bado Kuna suala la kuimarisha diplomasia Kama ilivokuwa zamani, Kwan tukiendelea kuomba wakati tunajipanga wwnyewe Kuna tatizo gani?
Mbona tunaomba hela za reli SA?
Bado makamuzi kwenye bidhaa za kawaida yaliovuka viwango, and yet uongeze gharama za usafiriahaji, just by mere sitting like f@@ls.
Kilichobaki ni kutuuza Tu sasa......
 
Hii nchi ni ya maajabu 8 ya dunia petron ina uhusiano gani hapo ukipandasha petrol ni kuwa umepandisha kila kitu

Hii dhana ya kuachia wamachinga wauze vitu holela barabarani na kuchafua mazingira bila kulipa kodi ndo inatufikisha huku kisa eti wanatetewa wanyonge sasa kodi alipe nani
 
Tunaonewa tu, roadlisense iko juu, petrol inapanda kila kukicha...kwanini tunauana?
Si waachane na mbio za mwenge ili wazibe pengo?
Petrol ikipanda, usafiri na usafirishaji unapanda, bidhaa za kiwandani zitapanda na bei ya mazao itapanda kutokana na gharama za usafirishaji.
 
Hata hayo maji yatapanda bill
Sijui hao wabunge wanafanya nn mle
 
Tuna Bahati mbaya Sana kuwa Na wanasiasa wajinga namna hii, yes.. I mean it...

Hivi kwa akili ya kawaida kwanini serikali haipanui wigo wa kodi?
Wanachi mil 50, wanaolipa kodi hawafiki 10%, bado unawapa elimu bure Na bla bla kibao...

Kwanini tusiboreshe Kilimo tukatoa kodi huko, vile vile kuruhusu export ya mazao?

Bado Kuna suala la kuimarisha diplomasia Kama ilivokuwa zamani, Kwan tukiendelea kuomba wakati tunajipanga wwnyewe Kuna tatizo gani?
Mbona tunaomba hela za reli SA?
Bado makamuzi kwenye bidhaa za kawaida yaliovuka viwango, and yet uongeze gharama za usafiriahaji, just by mere sitting like f@@ls.
Kilichobaki ni kutuuza Tu sasa......

Una mawazo mazuri lakini ni vizuri ukafafanua.
Unajua serikali ipo kila mahali hata humu ndani kuna wahusika wanahitaji mawazo ya kujenga nchi.

Ni kweli Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa hili.

Wakati wa Serikali ya Mkoloni Africa ilikua ni sehemu muhimu sana kwa kilimo.
Leo Africa wanataka kurukia viwanda bila kuwa na chakula cha kutosha na malighafi.
Hata maarifa ya kutosha kwenye viwanda hatuna. Tunataka tuwe na viwanda vitakavyoendeshwa na wachina.
Kwa akili yangu kuliko kuwa na viwanda kwenye ardhi ya Tanzania halafu vimilikiwe na kuendeshwa na wachina ni Bora vingebaki huko kwao tukanunua bidhaa.

Ni lazima pia tuangalie Athari za kimazingira zinazosababishwa na viwanda. Ghara za kulinda mazingira yatakayoharibiwa na viwanda ni kubwa mno.

Yani nchi yetu kwa kweli imekosa viongozi wabunifu na wenye kutambua waanzie wapi. Nadhani ni kwa sababu ya ukubwa wa nchi na kuwa na watu wachache wanaolazimisha kujua kila kitu na kuwa wao ndio wanaopanga kila kitu.

Nadhani watanzania wangeelewa umuhimu wa serikali za majimbo au Mikoa yenye mamlaka na bajeti zake kamili bila kuingiliwa na serikali kuu basi tungeweza kusogea kwa kasi hapa tulipo.
Mfano sasa hivi Halmashauri nyingi zimezuiwa kisiasa zisitoze ushuru wa mazao badala ya kusimamia matumizi ya zile fedha zitoe huduma kwa wananchi wao wamazuia utozaji . Tatizo sio utozaji bali matumizi ya hizo fedha.
Ni mwananchi gani anayeweza kukataa kuchangia maendeleo yake mwenyewe kama anayaona?

Pia upande wa kuchangia gharama za shule. Ada zimefutwa ,eti elimu bure brashi. Kwa uchumi upi wa kutoa elimu bure!! Bure ni ghali. Sasa elimu inaporomoka kwa kasi kubwa. Walimu walikua wanajitahidi kufundisha kutokana na kuwa walikua wanaweza hata kupata fedha za stationary lakini kwa sasa hali ni ngumu kifedha.
Elimu ilitakiwa iwe shirikishi kama ilivyokuwa. Hata kanisani watu wanatoa sadaka kama njia moja wapo ya kuendesha gharama za injili.
Je, serikali ilishindwa kupata takwimu ya watoto wanaotoka familia maskini sana ambao hawana uwezo wa kulipa ada hata sh. 2000 kwa mwaka ili wajulikane kuwa ni wangapi halafu kama kweli hawana uwezo wa kuchangia hata 2000 kwa mwaka basi wasome bure?
Kwa nini shule za serikali zisigawanywe kulingana na uwezo wa wazazi. Wale wasio na uwezo wa kulipa ada kabisa ndio wasome shule za bure kabisa. Wale wenye uwezo wa kuwasomesha watoto wao na kuwapa chakula na vifaa muhimu basi wasome shule zao. Kila mtu anatafuta maisha ya baadae ya mtoto wake hivyo kuzifanya shule zote ziwe bure na kutoa elimu duni ni kuathiri future ya jamii nzima.
Vijijini wapo pia wazazi wenye uwezo wa kuwasomesha watoto wao kwa kuwalipia ada alimradi tu wapate elimu bora. Iweje Mzazi anayekosa ada ya shule ya Msingi ya sh. 15,000/- kwa mwaka aambiwe kuwa ajilipie ada ya chuo ya mil. 2.5.? Yani Elimu ya msingi bure brashi halafu chuo hata akiomba mkopo anaambiwa ajilipie eti serikali haina pesa za kuwakopesha?Haingii akilini unapotoa elimu ya msingi na ya sekondari bure halafu ushindwe kuwakopesha ada wataalam vyuo wanaotakiwa kulikomboa taifa kwa elimu wanayoipata na tafiti zao.

Leo hii hao hao wazazi wa watoto wanaosoma bure wanashinda kwenye pombe za kienyeji huko vijijini. Wanamiliki simu na kila siku wanaweka sh. 500/- kwa mwezi ni sh.15,000 /- Kwa Mwaka ni Sh. 180,000/-.
Kitu gani kiliangaliwa wakati wa kuja na hii sera ya Elimu Bure!!? Bila shaka ni Kura? Watu waliangalia maslahi yao binafsi ya kupata kura na kutawala tu! Asiye na ufahamu anaona kuwa ni uzalendo ulitumika. Ni Maslahi ya kupata uongozi na kushika dola.

Suala la Maji Bado tunarudi pale pale kwenye kwenye siasa na mipango mibovu. Labda tuangalie awamu hii ya Tano kama itaachana nambo ya kulenga kura tu. Wakati JK alipokuwa anamaliza muda wake bajeti ya maji ilikua kubwa sana. Lakini ukiangalia ilikuwa imelenga maslahi binafsi. Hii miradi mikubwa inawanufaisha watu wachache ndio maana wanaipenda lakini haiwafikii wananchi wengi japo inatumia mabilioni ya fedha.

Hebu tujiulize mvua zinazonyesha mpaka mafuriko tulijiandaa vipi kuyatumia hayo maji ambayo kufikia mwezi wa kumi nchi iliyokuwa imejaa maji kila kona itakua kame.
Maji yote yamekimbilia baharuni na ardhini. Unaweza ukadhani hiyo nchi haina binadamu wanaoishi.

Yapo maeneo yenye maji ya chemchem za asili zenye maji mengi na mito ambayo hata hazihita teknolojia kubwa kuyapeleka kwa wananchi hasa wale wa vijijini.

Iko wapi miradi ya kujenga Mabwawa ya kukinga maji ya mvua?

Iko wapi miradi ya kujenga matenki makubwa kwenye hospitali zetu za vijijini ambazo hata maji ya chooni hakuna lakini mvua zinanyesha na maji yanatirika kwenye mabati na kuelekea ardhini.

Ipo wapi miradi ya kujenga matenki makubwa kwenye majengo ya shule za vijijini ambapo wanafunzi wanatembea na vichupa vya maji mwaka mzima na maji ya mvua yanatirika kuelekea ardhini.
Ukiwauliza wanakuambia hawana fedha za kufanya miradi hiyo. Hiyo sio sababu.Wafungwa wapo,majeshi yetu yapo, wanavijiji wapo ,wangeweza kufanya hiyo niradi kwa gharama nafuu sana. Ukweli mi kwamba Wakubwa hawapendi kuwaza na kubuni vimiradi vidogo vidogo mana havina fedha wakati wa kufanya zabuni au manunuzi.

Tuone Labda hilo la kuongeza bei ya mafuta litasaidia mana maji yamekua kero kila mahali.
 
SERIKALI imekubali kukutana na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili kuangalia jinsi ya kuongeza Sh 50 katika bei ya petroli na dizeli ili zipatikane fedha za kutekeleza miradi ya maji nchini. SOURCE: Mtanzania
Ikibidi waongeze tu, maji muhimu kuliko petroli, maji ndiyo asilimia 85 - 90 ya miili yetu.
Tatizo liko kwa wanauchumi wetu, kwanini hatawatafuti njia mbadala wa kupata hela ya kufanya haya, zaidi ya kuongeza kodi kwenye petroli, vinywaji, sigara n.k.?! Je ndiyo vichwa vya mazuzu? Au tena elimu zao zina mashaka? Twavuna tunachopanda, raia wakipiga kelele kuhusu mikataba ya rasilimali zetu zote naona serikali hailewi, bado kulindana na kuogopa kuambiana ukweli kuwa mwenzangu ulikosea, turekebishe hapa na pale nchi na raia wafaidike, kwani ukiweka mikataba wazi itakuwaje? Nini cha kuficha? Wamlinda nani hasa? Hapo ndipo sisi uswahilini twashangaa, unaficha mikataba kwa faida ya nani hasa?!
 
Hapa serikali ilipunguza bajeti ya maji kuendana na program ya miradi ya maji 2017/2018. Hamna haja ya kutenga fedha nyingi mwisho inaishia mifukoni mwa miradi mibovu. Kulazimisha kuongeza kodi ya mafuta ni udhaifu wa wabunge kwa watu wanaowakilisha maana yangu mnawaongezea mzigo wananchi.
Serikali ilipanga bajeti hii kufuatana na makusanyo yake ya kodi wabunge wanapolazimasha kuongeza bajeti hii ni kesho kuja kuilaumu serikali. Wabunge pia wasiwe na lawama kwani program ya miradi ya maji inaenda kwa awamu haiwezekani serikali iliyopo madarakani ikatekeleza miradi yote ya maji nchini hapa nchini kwa mwaka mmoja.
 
Tuna Bahati mbaya Sana kuwa Na wanasiasa wajinga namna hii, yes.. I mean it...

Hivi kwa akili ya kawaida kwanini serikali haipanui wigo wa kodi?
Wanachi mil 50, wanaolipa kodi hawafiki 10%, bado unawapa elimu bure Na bla bla kibao...

Kwanini tusiboreshe Kilimo tukatoa kodi huko, vile vile kuruhusu export ya mazao?

Bado Kuna suala la kuimarisha diplomasia Kama ilivokuwa zamani, Kwan tukiendelea kuomba wakati tunajipanga wwnyewe Kuna tatizo gani?
Mbona tunaomba hela za reli SA?
Bado makamuzi kwenye bidhaa za kawaida yaliovuka viwango, and yet uongeze gharama za usafiriahaji, just by mere sitting like f@@ls.
Kilichobaki ni kutuuza Tu sasa......
Mkuu nakuunga mkono sana
 
Nchi yetu inabahati mbaya sana ya kutokuwa na wanasiasa wabunifu, kuna maeneo mengi sana ambayo kama yatafanyiwa kazi fedha za miradi zitapatikana za kutosha kama vile kwenye kilimo, madini, maliasili n.k, wote wamekariri eneo moja la nishati ya mafuta. Poor Tanzania
 
Tunaonewa tu, roadlisense iko juu, petrol inapanda kila kukicha...kwanini tunauana?
Si waachane na mbio za mwenge ili wazibe pengo?
Petrol ikipanda, usafiri na usafirishaji unapanda, bidhaa za kiwandani zitapanda na bei ya mazao itapanda kutokana na gharama za usafirishaji.

wapunguze posho za wabunge hata mishara yao ni mikubwa sana nayo ipunguzwe.
 
Back
Top Bottom