KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Macho na masikio ya watanzania na dunia siku ya jana vilikuwa nikutaka kusikia stori ya shutuma ya Tundu Lissu dhidi ya serikali yake ina-balance kwa kusikiliza upande wa pili ambao ni serikali baada ya kiongozi wa serikali ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki prof. Kabudi kuhojiwa na kituo kilekile ambacho Tundu Lissu alikitumia kuishutumu serikali juu ya shambulio lake. Kwa shirika kubwa kama BBC kushindwa ku-balance shutuma hizo kwa kusikiliza utetezi wa serikali inatupa picha ya maswali yafuatayo:
- Kama kweli BBC wana weledi wa kitaaluma na kazi zao, moja ya kazi hizo ni ku-balance stori kwa pande zote kwa kusikiliza utetezi wa upande mwingine. Je, kushindwa kusikiliza serikali hili kuondoa ile sintofahamu si kwenda kinyume na taaluma yao? Je, wameamua kuiamisha dunia kwamba Lissu kaongea ukweli kwa kwenda kinyume na taaluma? Au ni kwamba Lissu wamempuuza na shutuma zake?
- Kama ni kweli shutuma za Lissu wamezipuuza, kwa nini wamepuuza? Huo si ni ushahidi wa kutosha kwamba Lissu kapuuzwa baada ya dunia kuona alikuwa anapotosha?
- Mkoloni atabaki kuwa mkoloni tu na ukoloni wa BBC kwa Tanzania umeenda mbali Zaidi kwa wao kuanza kututawala kifikra hivyo ni jukumu letu sisi watanzania kusimama kwa ajili ya nchi yetu wenyewe.
- Tumeona na kushuhudia weledi wa vyombo vya kimataifa juu ya nchi za Afrika na nina hakika ingekuwa ni Marekani imeshutumiwa hivyo BBC ingejitahidi kuihoji serikali ya Marekani ili ku-balance stori lakini kwa nchi za Afrika no balancing of story, shutuma tu zinatosha.
- Hongera sana Prof.Kabudi na Rais Magufuli, heroic leaders of this generation and history makers of the future generations na mimi binafsi nina amini katika uzalendo, uadilifu na umakini wenu.