Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,430
Haka kamsemo kakusema Vyuma Vimekaza kamejipatia Umaarufu Sana Mwishoni mwa Mwaka Jana, Kakiwa na maana ya kusema maisha magumu....
Lakini Kama Na wewe Ni Miongoni mwa wa walioathirika na Kauli Hii Basi Fuatana nami kwa Ufupi Katika Somo Hili....
Nafikiri Huu ni mwaka Mwingine kabisa, Huna Sababu ya kuendelea kulalama vyuma Vimekaza Kwa Sababu nimegundua Siri Ya kuvipoteza kabisa hivi vyuma kwenye USO wa Dunia....
KUMBUKA
Maisha Kwa kawaida Ni Magumu..
Na Maisha Hayo hayo, Hayana Mpango wa kuwa Marahisi...
Nadhani Utakuwa na Kumbukumbu nzuri Kweli Ya mwaka Jana...
Wakati wewe unalia vyuma vimekaza Kuna MTU alipita na tipa la mchanga akiwa Anaenda kuanza ujenzi kwenye Eneo Lake..
Pia Utakumbuka Kipindi Wewe unasema vyuma Vimekaza Kuna jirani yako alikuwa anafanya maandalizi ya kufunga ndoa ya kifahari na Yule Binti...
Hayo yooooote yanatosha kukuonesha kuwa tatizo sio vyuma, ila tatizo ni wewe mwenyewe...
NDIYO TATIZO NI WEWE
Tatizo Lako Ni Hili
Yeremia 17:5
Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
Hilo ndo Kosa lako....
Kwani kuna siku Uliwahi Kufanya KAZI ukaacha kulipwa
Au Ndo Mazoea ya zile bahasha za kaki
usipopona katika eneo Hili tutakusikia Ukisema vyuma vimepata kutu maana Havikubali hata Grisi....
Sasa Tusome maandiko haya chini Uone
Yeremia 17:7:8..
Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana ni tumaini lake.
Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.
Kwa mujibu wa maandiko Hayo inatosha kutudhihirishia kuwa, Shida sio vyuma Bali shida Ni wewe....
Maandiko yapo wazi kabisa kuwa ukimtegemea Mungu utachanua tu Haijalishi Hali ya uchumi ikoje.....
Cha kufurahisha zaidi ni kuwa Mungu Naye Anajua kuwa kuna vyuma kukaza..
JE MUNGU ANASEMAJE KUHUSU KUKAZA KWA VYUMA
Tupitie Haya Maandiko uone
Isaya 45:2-3
Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; *nitavunja* vipande vipande milango ya *shaba* , na *kukata* - *kata* mapingo ya *chuma* ;
nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Hiyo mistari inaashiria kuwa Hata Mungu Anajua kuwa kuna vyuma kukaza
Kwa Hiyo Huna sababu ya kuendelea kulalamika juu ya vyuma kukaza Bali Tafuta kumkaribia MUNGU ambaye atakufanya ustawi katikati ya mazingira Magumu...
TAFUTA KUMJUA MUNGU NA SI KUUNDA VIKUNDI VYA KUMLALAMIKIA MTU..
Mungu Akubariki Sana. Ujumbe Huu upate Kibali ndani yako Kwa Msaada Wa Roho Mtakatifu ili Uweze Kufanya mabadiliko kwenye Aina ya Maisha Unayoishi...
Ayubu 22:21
Mjue sana Mungu, Ili Uwe Na AMani; Ndivyo mema yatakavyokujia.
Ameni.