Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,067
Nimetoka kuitazama video ya wimbo mpya wa Mkongwe wa Hiphop Bongo, Jumanne Mohammed Mchopanga aka Jay Mo. Nitasema machache.
Mule ndani, pamoja na mabalaa mengine yaliyofanyika, nimependa jinsi Mr. Famous alivyobadilika mpaka kufikia hatua ya kucheza kwa maringo kama wafanyavyo Wasafi Dancers kwenye nyimbo zao.
Ahmad/Hamadi Ali alivyosema ''Si ulimwiga Basta (Busta Rhymes)? Mwenzio sasa anaimba, fala badilika fasta, utue mzigo wa ujinga'', akapokea mashambulizi, lakini watu makini kama Profesa Jay na Joh Makini wakayachukua na mambo yakajipa.
Sasa mzee mzima Mchopanga nae ameona isiwe shida, katia nywele maji.
Hii mimi naiita Bongo Flavour Revolution. Yaani ukiona mpaka Jay Mo amelegeza ujue kweli mwana kakua.
Shime Platnumz, nimeskia tetesi za WCB kumsajili Joh Makini, plz muongeze na huyu nguli ili muziki wake upate thamani inayostahili.
Endeleeni kuwafundisha biashara ya muziki hawa watu.