Jasusi wa kirusi na waziri wa uk

Jasusi wa kirusi na waziri wa uk

Kubingwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2010
Posts
505
Reaction score
69
Jamani hivi inawezekanaje waziri kule UK (sio Ukonga,naongelea mamtoni) afanye kazi kwa waziri hadi igundulike ndo ajiuzulu uaziri?
 
Mkubwa yaani inawezekanaj jasusi afanye kazi za ndani kwa waziri,imegundulika kuwa jasusi alikuwa anafanya kazi kwa waziri na akiwa na uhusiano wa mambo flani na watu wa nje ya UK,WANYATUZI KULIJUA HILO ILIBIDI WAZIRI APIGE NYAMA CHINI
 
Mleta mada hebu kwanza pata habari kamili ndiyo uilete humu. Huyo dada hakuwa mfanyakazi wa ndani wala huyo jamaa hakuwa waziri Uingereza.
Habari sahihi ni kwamba huyo jamaa alikuwa mbunge ambaye alimuajiri huyo dada Mrusi kuwa msaidizi wake kwenye ofisi yake ya bunge. Mrusi huyo alimlenga jamaa kwa sababu alikuwa kwenye kamati ya ulinzi bungeni na kwenye lililokuwa jimbo lake ndiko kilipo kituo kikubwa cha jeshi la majini la Uingereza. Kwa sababu hizi mbili ilikuwa rahisi kwa huyu dada kupata siri za masuala ya ulinzi ya Uingereza na kuzituma Urusi.
 
Umeona Maadili yaani tabia zake zimechemsha kiasi kuwa yeye mwenyewe Mr Mike Hancock imekula kwake ingekuwa bongo angepandishwa cheo toka ubunge mpaka Urais.Mzee mwenye miaka Sabini na kuwa na mahusiano na binti wa miaka 27 kama sio uchafu na ujinga uliopitiliza ni nini?

MHancock_415.jpg
MP Liberal Democratic Mr Mike Hancock

article-1335986-0C5DB95F000005DC-261_634x427.jpg
Russian Spy Girl Katia Zatuliveter [Miaka 27] Mp's Lover
 
DSN sikatai hata kidogo kuwepo kwa maadili mazuri au mabaya na tabia nzuri au mbaya. Nachosema ni kwamba morals na manners hazichagui mfumo wa uchumi. Wapo wajamaa wenye tabia nzuri na mbaya hali kadhalika wapo mabepari wenye tabia nzuri na mbaya.
Haya ni masuala ya utashi na busara za mtu yanayoongozwa na moyo.
 
Jamani hivi inawezekanaje waziri kule UK (sio Ukonga,naongelea mamtoni) afanye kazi kwa waziri hadi igundulike ndo ajiuzulu uaziri?

Kubingwa jaribu kujipanga mkuu ukitaka kuingia hapa JF .
 
Umeona Maadili yaani tabia zake zimechemsha kiasi kuwa yeye mwenyewe Mr Mike Hancock imekula kwake ingekuwa bongo angepandishwa cheo toka ubunge mpaka Urais.Mzee mwenye miaka Sabini na kuwa na mahusiano na binti wa miaka 27 kama sio uchafu na ujinga uliopitiliza ni nini?

View attachment 39470
MP Liberal Democratic Mr Mike Hancock

View attachment 39471
Russian Spy Girl Katia Zatuliveter [Miaka 27] Mp's Lover
Hata paka mzee bado hupenda kunywa maziwa.
 
Back
Top Bottom