Steven Jibe
Member
- Jul 31, 2014
- 17
- 4
Serikali ya Gabon imetangaza kuwa, wanajeshi waliohusika na jaribio la kuipindua serikali ya nchi hiyo wametiwa nguvuni.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Gabon imesema kuwa, hali ya mambo nchini humo ni shwari na waliohusika na jaribio hilo wamekamatwa.
Ripoti zinasema utulivu umerejea tena katika aghlabu ya maeneo ya mji mkuu wa Gabon, Libreville na kwamba vikosi vya jeshi na polisi ya nchi hiyo vimesambazwa katika mitaa na maeneo mbalimbali ya mji huo kulinda usalama.
Mapema leo idadi kadhaa ya wanajeshi wa Gabon walivamia jengo la Kituo cha Redio ya Taifa ya nchi hiyo na kukidhibiti. Kundi hilo pia limetangaza kuwa limeunda baraza la taifa la marekebisho.
Wanajeshi waliofanya jaribio la mapinduzi Gabon
Kundi hilo la wanajeshi waliofanya jaribio la mapinduzi limesema, haliridhishwa na hali ya kiafya ya rais wa nchi hiyo Ali Bongo anayeendelea kupatiwa matibabu nchini Morocoo baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi.
Rais Ali Bongo, mwenye umri wa miaka 59 alilazwa hospitalini nchini Saudi Arabia mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kupatwa na kiharusi. Lakini tangu mwezi Novemba amekuweko nchini Morocco akiendelea kupatiwa matibabu.
Katika hotuba aliyotoa kwa mnasaba wa kuingia mwaka mpya wa 2019, kiongozi huyo alikiri kwamba hali yake ya afya si ya kuridhisha lakini akasema anaendelea kupata nafuu.
Chanzo: www.parstoday.com