kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Shinzō Abe ataka kufanya mazungumzo na Kim Jong-un wa Korea Kaskazini
Mei 20, 2019 10:06 UTC
Kwa mara nyingine Waziri Mkuu wa Japan, Shinzō Abe ametaka kufanyika mazungumzo na Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini kwa ajili ya kutatua suala la Wajapani waliotekwa nyara.
Abe ameyasema hayo mjini Tokyo katika kikao cha familia za watu hao waliotekwa nyara ambapo pamoja na mambo mengine ameongeza kwamba, ameazimia kufanya mazungumzo na kiongozi huyo kijana wa Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote. Kabla ya hapo pia Waziri Mkuu wa Japan alitangaza kwamba licha ya Korea Kaskazini kufanya majaribio ya makombora ya masafa mafupi, lakini Tokyo inapendelea kufanya mazungumzo na Pyongyang bila ya sharti lolote.
Hii ni katika hali ambayo hadi sasa viongozi wa Korea Kaskazini bado hawajatoa jibu lolote kuhusiana na ombi hilo la Japan. Serikali ya Japan inaituhumu Korea Kaskazini kwamba ilihusika na utekaji nyara wa raia wake 17 uliojiri mwishoni mwa muongo wa 1970 na mwanzoni mwa muongo wa 1980. Wakati huo huo raia wa Japan wamekaribisha msimamo wa Shinzō Abe wa kutaka kufanya mazungumzo na Kim Jong-un bila ya masharti yoyote. Matokeo ya uchunguzi wa maoni yanaonyesha kwamba karibu asilimia 61 ya watu walioshirikishwa katika uchunguzi huo, kuhusiana na msimamo wa Waziri Mkuu wa Japan wa kufanya mazungumzo na Kim Jong-un, wamekaribisha pendekezo hilo. Aidha uchunguzi huo umeonyesha kwamba asilimia 30/2 ya Wajapan wanapinga suala hilo. Shinzō Abe, Waziri