January mkamba: Tunahitaji vyama vya upinzani imara.

January mkamba: Tunahitaji vyama vya upinzani imara.

mkude kibwana

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
348
Reaction score
27
Leo hii tunapoadhimisha rasmi miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ujumbe wangu kwa wanachama wake ni ule ule nilioutoa kupitia kitabu cha ‪#‎TanzaniaMpya‬ kwamba:


"Lazima tuendelee kusimama kidete kuwasemea na kuwatetea Watanzania, hasa wanyonge wa hali ya chini. Chama chetu ni lazima kiendelee kupambana na kukemea vitendo vya rushwa na maovu kwa nguvu zote. Vitendo vya rushwa na ubadhirifu vinavyofanywa na wachache vinakiharibia sifa Chama chetu. Tusikubali hata kidogo wanachama na viongozi wetu ambao sio waadilifu wachafue sifa, heshima na imani waliyonayo wananchi kwa chama chetu".

Niliongeza kusema:


"Chama chetu kinahitaji mabadiliko makubwa ya kiutendaji na kiuendeshaji ili kikabiliana na zama mpya za ushindani mkali wa kisiasa na mazingira mapya na changamoto mpya za ndani ya jamii. Ufahamu na uwezo wa kuleta hayo mabadiliko vijana wengi tuliolelewa na kukulia na kupata uongozi wa juu wa CCM tunao."


"Amani, utulivu, umoja na maendeleo ya nchi yetu, salama yake iko mikononi mwa CCM. Lakini kwa uimara wa demokrasia hapa nchini, tunahitaji vyama vya upinzani imara lakini sio wajibu wa CCM kuimarisha vyama vya upinzani."

Kusoma kwa kirefu zaidi, tazama majibu yangu kamili ya swali la 33 kupitia tovuti ya kitabu ya www.tanzaniampya.com



 
Ni kweli kinahitajika chama au vyama vya upinzani imara. Wasiwasi wangu ni kuwa baada ya uchaguzi mkuu huu ujao CCM itakuwa bado moja bila kugawanyika na kuwa chama cha upinzani imara?
Nimeona pamoja na mwenyekiti wao Taifa kujaribu kuwaweka sawa ili wajiandae "Kisaikolojia" lakini imekuwa ngumu kwao kujiandaa namna hiyo.
 
Back
Top Bottom