A; Babu Babu, January Makamba jina lake limekatwa kwenye mbio za Ubunge,
Je Rais Samia na Kikwete wanamchukia au wana matumizi naye kwa mipango mingine?
B; Mjukuu wangu baada ya jina lake kukatwa Januari Makamba kwenye maelezo yake ya kwanza kwa waandishi wa habari na umma je alikuwa katika hali ya hasira, huzuni, masikitiko au alikuwa Normal?
A; Babu mimi sijasoma sina hata elimu ya Saikolojia, ila kwa haraka haraka alikuwa ktk hali ya kawaida licha ya kutengenezea movie ya kwamba waandishi wamemvamia kumhoji bila kuwaita na kujidai kupandisha ngazi za ghorofa kwa miguu kisha kutengeneza presh ya kupumua
B; sawa mjukuu wangu, kama alifanya press akiwa ktk hali ya kawaida, nyuma ya pazia ni Kikwete amemweka kuwa karata yake ya pembeni plan B, kama ikitokea la kutokea Januari awe mgombea wa kiti cha urais,
Plan A ikifaulu basi Januari atapewa cheo kikubwa kikubwa serikali au Chamani.
Mjukuu wangu kitu ambacho kitafanya uamini kuwa Kikwete na Samia wana kazi naye ni pale atakavyoshiriki kampeni za uchanguzi mkuu kwa ukamilifu kumnadi mgombe wa ccm iwapo atakuwa huyu wa sasa........